Covid-19: Gharama za matibabu zitabebwa na nani?

Mfikirishi

JF-Expert Member
Jan 16, 2012
7,489
8,533
Tunatangaziwa kuchukua tahadhari, lakini pamoja na ilani zote hizo kama taifa tumejipanga vipi kugharamia matibabu ya wote watakaokumbwa na hili janga la Covid-19, kuanzia vipimo na kadhalika?

Je, huko kwa Mkemia Mkuu uwezo upo wa kupima sampuli nyingi kiasi gani?

Je, hospitali zetu zina sehemu maalumu kuwaweka wagonjwa hawa?

Wataalamu wetu wa afya wana vitendea kazi vya kutosha?

Au bado tunajipa moyo kuwa hili tatizo haliwezi kumdhuru Mtanzania?
 
Serikali ipo, itabeba maana hili ni janga,,,kwani kipindupindu huwa anabeba nani cost?
 
Kama China yenyewe wagonjwa mpaka sasa hawajifikia 100,000. Say na sisi wafikie 100,000, serikali haiwezi shindwa kuwahudumia. Hofu ni kama tutaweza ponyesha wagonjwa wengi kama China.

Kama vipimo tu ni shida, nina wasiwasi na uwezo wa serikali kukabiliana na changamoto waliyoitengeneza wenyewe, hii ya kuanza kutafuta washukiwa.
 
Back
Top Bottom