COVID - 19: CHADEMA, Taasisi za kijamii na vyama vingine vya upinzani fanyeni haya kuwasaidia watanzania

Uncle Jei Jei

JF-Expert Member
Jan 7, 2011
1,684
2,157
Nimengi mmeshauri, nimengi mmeonya, nimengi mmependekeza na pia nimengi mmekemea na mengi pia mmeasa.

Hata hivyo katika mengi yote hayo mliyofanya kwa nafasi yenu kuna mengi huenda hayajafanyiwa kazi au kupokelewa kabisa kulingana na matarajio yenu

Ni kweli kabisa unaposhauri, unapoonya, unapopendekeza na kufanya mengine yanayofanana na hayo linabaki jukumu la kuyapokea au kuyapuuza kwa yule anayeshauriwa.

Watanzania tunafahamu nyie hamna dola, hamna serikali, hamna wafanyakazi wala hamna hazina wala hammiliki benki. Hata hivyo hiyo haiwazuii kufanya kitu kwenye jamii kwa kile mlichonacho na kupitia kwa wadau wenu

Janga limetukuta wanaoumia kihisia na kwa uhalisia ni watanzania wote bila kujali chochote.

Nawaomba mfanye yafuatayo:-

i. Kama kuna yeyeto anamiliki Hoteli kubwa au ana uwezo wa kukodi kisha aitoe kwa serikali kwa muda itumike kama kituo mahususi cha kuhudumia wagonjwa wa Covid - 19 katika mkoa wowote ulioathilika sana

ii. Kupitia wadau wenu, vipato vyenu na wafadhili mbalimbali jichangeni mpate vifaa vya kisasa vyenye hadhi ya WHO vya kuhudumia wagonjwa wa Covid- 19 haafu vitumike kwenye hicho kituo

iii. Hakikisheni kituo kinakuwa bora, chenye vifaa bora, na kitakachokuwa na mazingira mazuri na rafiki sana kwa watoa huduma na wagonjwa watakao kuwa pale

Baada ya kukamilisha, muiteni Waziri Mkuu au Waziri wa afya mwambieni tunakukabidhi kituo hiki hadi hapo tatizo hili la korona litakapoisha ndipo mtaturudishia hoteli yetu

Wakati wa makabidhiaono pendekezeni idadi ya wagonjwa watakoa faa kuhudumiwa hapo na idadi ya watoa huduma itakayofaa kwenda kuhudumia pale.

Kisha toeni ahadi kwamba wakishawapa madaktari na wahudumu wengine wa afya nyie kazi yenu ni kutoa vifaa tiba na vifaa kinga kwa hao watoa huduma na kuhakikisha huduma zinaenda sawa. Posho na mishahara yote hiyo itakuwa gharama ya serikali.

Kwa kufanya hivyo naamini mtakuwa mmetoa mchango mkubwa kwa serikali na kwa jamii ya watanzania

Kama hilo ni gumu, basi kwa wingi huo huo nilioutaja hapo juu, jichangeni mnunue mashine za kusaidia kupumua (ventilators) angalau mia moja (100) pelekeni kwenye mamlaka husika zijiridhishe, zikague halafu fanyeni makabidhiano hadharani.

Kuendelea kutoa ushauri usio pokelewa na kufanyiwa kazi ni kupoteza muda tu. Badala yake fanyeni vitendo ili wakikataa tujue nia yoa ni nini.

Asanteni sana kwa kunisoma
 
Wabunge wa Chadema ni matajiri sana ila sijasikia wakirudisha kwa jamii
 
Back
Top Bottom