Course ipi ni nzuri kati ya hizi kwa SUA?

Mtanzanyika

JF-Expert Member
Feb 12, 2015
370
424
Wakuu Salaamu..!!

Ningependa kufahamishwa course gani kati ya nitakazozitaja hapa chini ni nzuri katika Chuo Cha kilimo cha Sokoine - SUA na pia upatikanaji wa ajira kwa course hizo. Kozi zenyewe ni:

1. Bsc in Biotechnology and Laboratory science.

2. Bsc in Family and consumer studies.

3. Bsc in Food science and Technology.

4. Bsc in Human nutrition

Karibuni kwa mawazo yenu kuhusu ubora wa kozi tajwa hapo juu na kuhusu upatikanaji wa ajira baada ya kumaliza masomo.
 
Kuna jamaa zangu wamesoma food science and technology wote wamekula shavu TFDA.... I suggest usome hio pia.

Ila kwa course yeyote utakayosoma hakikisha unaanza kujitengenezea "connection" mapema kabla hujahitimu masomo yako hususani Sehemu utakazo kwenda kufanya field practical.....mambo ya ajira siku hizi bila connection ni msoto mkali.
 
Kwahiyo utumishi(sekretarieti ya ajira) sifa wanazopewa ni za nini kama mambo ya connection bado ndo mchongo mkubwa?
 
Kwahiyo utumishi(sekretarieti ya ajira) sifa wanazopewa ni za nini kama mambo ya connection bado ndo mchongo mkubwa?
Ndugu yangu hii dunia we iache tu Kama ilivyo.

Miongoni mwa watu wanaoitwa kwenda kufanya interview za utumishi huwa Kuna watu wenye "vimemo" vyao kitambo tu yaani wanaenda kufanya interview Kama geresha tu na kuwapoteza maboya wengine lakini wao hata wafeli hizo interview connection zinawabeba hivyo kazi wanapata na kuwaacha wenye vigezo vyao wakipiga miayo tu.

Jeipiemu atafanikiwa kukomesha rushwa katika sekta zingine lakini katika sekta hii ya ajira hao "wanyonge" wake anaowatetea wananyongwa kweli kweli.
 
Kuna jamaa zangu wamesoma food science and technology wote wamekula shavu TFDA.... I suggest usome hio pia...
Sio connection field performance ina mchango mkubwa kupata ajira namfahamu mmoja anasoma marketing chuo akiwa mwaka wa pili alienda field kampuni ya mafuta akatafuta soko la mafuta tenda ya mwaka ya bilioni tatu kampuni ikapata kampuni ilimpa ajira straight wakamrudishia ada zote wazazi walizolipa from first year sasa anasoma kama mfanyakazi wa kampuni akilipiwa kila kitu na kampuni ikiwemo mshahara.

Hakuandika barua kuomba kazi lakini kapata !!! Don't play with field!!!
 
Sio connection field performance ina mchango mkubwa kupata ajira namfahamu mmoja anasoma marketing chuo akiwa mwaka wa pili alienda field kampuni ya mafuta akatafuta soko la mafuta tenda ya mwaka ya bilioni tatu kampuni ikapata kampuni ilimpa ajira straight wakamrudishia ada zote wazazi walizolipa from first year sasa anasoma kama mfanyakazi wa kampuni akilipiwa kila kitu na kampuni ikiwemo mshahara
Hakuandika barua kuomba kazi lakini kapata !!! Don't play with field!!!
Huwa nawambia hili vijana wenzangu wanafikiri najikweza ila ndio ukweli usio jificha toka enzi
 
Huwa nawambia hili vijana wenzangu wanafikiri najikweza ila ndio ukweli usio jificha toka enzi
Uko sahihi na usiache kusema wengi wanadhani field ni kwenda kuandika andika tu vi report kumfurahisha mwalimu akupe marks afaulu mtihani wanasahau kuwa client anapofanyia field anamkodolea mimacho kumwangalia kama ni potential kwake amchukue
 
Na madogo wakija makazini uku huwa wabishi wajuaji huwa nawapatia Marks zao waondoke mana ni vurugu tupu.wao ni kuchezea simu kulewa
Mwisho wanakuomba uwajazie logbook kishikaji
 
Back
Top Bottom