Countdown to Confederation of African Football (CAF) election, 16/03/2017

Yethero Mgale

JF-Expert Member
Apr 19, 2012
525
228
Ikiwa zimebaki siku 17 kabla ya kufanyika uchaguzi wa shirikisho la soka barani Afrika (CAF), mpaka sasa wagombea waliojitokeza ni wawili tu ambao ni Bw. Issa Hayatou ( Rais wa sasa wa CAF anayemaliza muda wake) na Ahmad Ahmad( Rais wa chama cha soka cha Madagascar) tofauti na uchaguzi wa mwaka 2013 ambapo Bw.Issa Hayatou alikuwa ni mgombea pekee wa uchaguzi.
Uchaguzi wa mwaka huu umevuta hisia za wapenda soka wengi hasa ikizingatiwa kuwa mataifa mbalimbali wanachama wa CAF yameungana na kutangaza hadhara mgombea wanayemuunga mkono kwenye uchaguzi wa machi 16 ili kutaka kuuondoa utawala wa Hayatou uliodumu madarakani tangu mwaka 1988 mathalani mataifa yote wanachama wa shirikisho la soka la nchi za kusini mwa Afrika( COSAFA) wametangaza kumuunga mkono Ahmad Ahmad, COSAFA ina nchi wanachama 14.
Vile marais wa mashirikisho ya soka kutoka vyama vya soka vya kanda nyingine wanamuunga mkono Ahmad Ahmad, miongoni mwao ni Amarju Pinnick( Rais wa shirikisho la soka la Nigeria, NFF) na Musa Bilith( Rais wa chama cha soka cha Liberia, LFA).
Stay tuned
ahmad.jpg
Issa_Hayatou_%28cropped%29.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom