Count down to election day!...... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Count down to election day!......

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mkandara, Oct 18, 2010.

 1. M

  Mkandara Verified User

  #1
  Oct 18, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Zikiwa zimebakia siku chache kufikia uchaguzi mkuu ningewaomba viongozi wote wanaogombea URAIS kuacha siasa za majitaka na badala yake kuzungumzia vision yao ktk Tanzania ya kesho ktk maswala nyeti ya Utawala.

  Nimegundua kwamba hizi siasa za majigambo are little more than just a pursuit of primitive accumulation na hazitaweza kuwasaidia wananchi wala taifa letu zaidi ya ahadi hewa ikiwa viongozi wetu hawana vision inayojenga ramani ya msingi wa ahadi hizo.

  Ni wajibu wetu wanachi kuwauliza viongozi wetu maswali magumu kuliko kuendelea kusikiliza ahadi zao kwani tunachoweza kumtambua mbwa mwitu ktk kundi la kondoo sii kwa ngozi yake, umbo lake wala miguu yake bali malengo yake kuingia ktk zizi..

  Tanzania tunahitaji visionary leadership. Kuahidiwa shule na Afya bure au kutujengea mabarabara, madaraja, na hata miji mipya haiwezi kuwa central of attraction kwa wananchi ikiwa vitu hivyo pekee havina malengo yatakayo boresha zaidi maisha na maendeleo ya nchi yetu. Tunahitaji zaidi ya ahadi, tunahitaji vision zao ktk ujenzi wa dira maendeleo yetu.

  Tunakumbuka rais wetu Kikwete aliwahi kuulizwa swali kwa nini Tanzania ni maskini? na kama sikosei alisema hata yeye hajui..Sasa sielewi kama wagombea wengine wanajua jibu na kama wanajua sidhani kama tumewahi kuwauliza!..Na kama tutawapa ridhaa zetu kutuongoza wataweza vipi kutuondoa ktk Umaskini ikiwa hili sio swali la msingi?..

  Tanzania is one of the richest country in Africa, if not the world (in terms of both natural and mineral resources). Yet the populations are the among poorest..
  hadi leo hii tunaendelea kushawishika kulaumu Ukoloni, Utumwa na hata Utandawazi n.k wakati tumeshindwa kujinyooshea kidole sisi wenyewe wakati wote. It has become fashionable..

  Hawa viongozi wanapokuja kuomba kura zetu huja kwa unyenyekevu mkubwa kama wao sii Wakoloni na exploiters lakini wakisha fika IKULU na kukalia kiti kikubwa utaona wakianza ku concentrate on power and wealth..we only find ourselves and all resources exploited for their own lavish enrichment.

  Tumechoka na Hatudanganyiki... tunahitaji Mdahalo tuwaulize maswali magumu kwani hili sio ombi ila ni lazima wao kujibu ili wapate ridhaa zetu...Ni sisi wananchi tulopewa nguvu na mamlaka ya kuchagua viongozi wetu.
   
 2. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #2
  Oct 18, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135


  Ati umesema???? Sasa hapo tayari wagombea wengine wameshajitoa maana hilo dudu mdahalo linatisha. hahah ahahaha

  Anywayz Mkandara, you have said it. Na kinachosikitisha hizi siasa za majiotaka ndiyo zinazo -carry a day. So far unakuta bado hakuna mipango madhubuti inayozungumzwa na kuwekwa hadharani (hasa kutoka chama tawala) kutuondoa hapa tulipokwama na kutupeleka pale say in the coming ten years.
   
 3. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #3
  Oct 18, 2010
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Wengine mkuu hawafanyi maji taka kabisa huwatendei haki hapo
   
 4. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #4
  Oct 18, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Mimi wananishangaza sana badala ya kunadi sera za chama wanaanza siasa za majitaka. Lakini kukimbia mdahalo kwa kweli hawatutendei haki kabisa.
   
 5. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #5
  Oct 18, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Makamba anasema sisi m wala kikwete hawahitaji mdahalo maana wao ni maarufu sana. Wananchi wanafahamu waliyofanya na hivyo hawaoni umuhimu wa mdahalo.

  Lakini Makamba hatuambii kwa nini sisi m imekusudia kutumia 50+ billion kwenye kufanya kampeni tu. Hatuambii kwa nini Kikwete atumie helicopter 3 kufanya kampeni wakati anafahamika kwa wapiga kura na tena wanafahamu tayari yale serikali ya sisi m wamefanya.

  Makamba hatuambii kwa hakika kwa nini Jakaya anatembea usiku na mcha na familia yake kwa pesa ya serikali wakifanya kampeni.

  Hatuambii kwa nini kama sisi m inafahamika kwa wananchi kiasi cha kutohitaji mdahalo kwa nini wamehonga vyombo vya habari mbali mbali mamilioni na mamilioni ya pesa ili vitangaze habari za sisi m tu na vingine viachwe bila kutangazwa habari zao.

  Sisi m hawana hoja tena za kutetea kuendelea kuwepo madarakani. Hawana namna ya kufanya zaidi ya kutughiribu kwa maneno matamu ya jukwaani waliyoyapanga kwa ustadi mithili ya hotuba walizoandika juu ya karatasi. TUWAKATAE
   
 6. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #6
  Oct 18, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Mkandara,

  Tungekuwa na independent na strong media, Kikwete angeshikiwa bango hadi kieleweke. Kwa sasa media zetu hizi za walamba miguu ya Kikwete, hakuna anayedai vitu muhimu kama hivi. So sad....
   
 7. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #7
  Oct 18, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  KWA KWELI mIDAHALO INGEKUWA MUHIMU SAAANA INGAWAJE NAJUA MZEE WANGU ANGEUMIA KWA KUSHINDWA KUJIELEZA!
   
 8. k

  kingwipa1 JF-Expert Member

  #8
  Oct 18, 2010
  Joined: Jul 2, 2008
  Messages: 335
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Watanzania wandai kitu cha haki lakini wakoloni wanakimbia na kudai wao ni maarufu..... maarufu wa kuiba na kukandamiza maslahi ya nchi. maarufu wa kukwepa mzani sawa ili kila mmoja ahukumiwe kwa kipimo kimoja.

  nimefanya kampeni na ninaendelea kufanya kampeni ili kuinusuru nchi kumezwa na familia ya jmk na maswahiba wake. mpaka sasa nimeshamnyangánya kura mia moja na ninatumaini nitakuwa nimeshatengeneza kura zaidi ifikapo tar 30 Oct, 2010. Uliikataa kura yangu nami naondoka na kura yangu pamoja na za familia yangu na za ndugu zangu na marafiki zangu. Hapo ndipo ninapokuchinjia mr. kiwete (BA) na kumpeleka Slaa (PhD) ikulu.
   
 9. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #9
  Oct 18, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Hivi bado mpo nyie?
   
 10. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #10
  Oct 18, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,018
  Likes Received: 417,506
  Trophy Points: 280
  Asiyehudhuria mdahalo amejitupa nje mwenyewe bila ya zengwe
   
 11. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #11
  Oct 18, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  NN... watu walikuwa wanakutafuta sana hapa friday.
   
 12. M

  Mkandara Verified User

  #12
  Oct 18, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Swala la Mdahalo ni letu sisi wananchi kupanga sio swala la JK au Makamba. Kama CCM watajitoa wajitoe lakini mdahalo ni lazima kwani napenda sana kusikia hawa wagombea wakipigwa maswali ya nguvu kutoka kwa wananchi. Tuwaeleze sisi tunatakja nini na kiongozi gani na jinsi gani kila mmoja wao atayashughulikia maswala hayo.

  Kwa hiyo hatra kama CCM wakijitoa bado viongozi wengine watapata nafasi ya kujitambulisha kwa wananchi na kuzungumzia sera zao huku wakiulizwa maswali kulingana na sera hizo..

  Shalom,
  Mkuu wangu siwezi kuwatendea haki Chadema kwa sababu naamini kabisa kwamba wapo watu wanaonadi pia siasa hizi kupitia jina la Chadema. Kikwete na viongozi wa CCM waliopo madarakani wametukanwa kwa majina yote mabaya unayoweza kufikiria...Hata mimi nimezungumza mengi kuhusiana na JK na CCM ambayo wao wanayaona kama ni majitaka..It all depend na wewe umesimama upande gani. Lakini pamoja na machungu yetu nadhani ni muhimu zaidi tukiwaweka kitimoto wakajibu chuki zetu badala ya sisi kuwachagua wao kutokana na ahadi zao..
   
 13. M

  MgonjwaUkimwi JF-Expert Member

  #13
  Oct 18, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 1,288
  Likes Received: 521
  Trophy Points: 280
  Kwa mtazamo wangu kila chama kinafanya assessment katika kampeni zake kujua njia zipi zina faida na njia zipi zina hasara. CCM wameona hawahitaji mdahalo, na kwa mtazamo wangu kura za CCM hazitegemei swingers kama ilivyo kwa vyama vya upinzani. Hivyo basi mdahalo hauna tija kwa CCM ingawa unaweza kuwa na tija kwa taifa. Maoni yangu binafsi ni kwamba CCM inapigana kutunza wapiga kura wake wakati wapinzani wanapigana kuchota wapiga kura wa ccm, hivyo basi hata kama CCM wataibuka washindi wa mdahalo (assuming this is possible) ccm itakuwa imeweka rehani baadhi ya wapiga kura wake kwa sababu wata create swingers. Kwa maneno mengine MDAHALO UNAWAGAWA WAPIGA KURA na hili halina tija kwa ccm (hata kama wangekuwa washindi wa mdahalo). Mdahalo una tija kwa wapinzani tu ambao lengo lao ni kuona wapiga kura wa ccm wanagawanyika. CCM wameliona hili na wamekataa kuingia mtegoni.
   
 14. M

  Mkandara Verified User

  #14
  Oct 19, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mkuu wangu swala la demokrasia halina tija kwa vyama husika isipokuwa kwa wananchi na Taifa. Demokrasia ninawapa nguvu wananchi kuchagua na sii chama kutawala wapendavyo wao.

  Ikiwa fikra za CCM kwamba ushindi wao utatokana pasipo mdahalo sasa hizo sera za nini?..kuepa mdahalo ina maana wanapuuza wananchi kwani sisi hatununui sera majukwaani (mbuzi ktk gunia) ila sisi wananchi tuna haki kabla hatujawachagua hao viongozi kuuliza kama kweli hizi sera ni mbuzi au wanatufungia nyama ya Kunguru. It's not about them, demokrasia inawapa wananchi uwezo wa kuchagua chama kutokana na sera zake na sii sura au umaarufu wa mtu.

  Ni wakati wa kuondoa fikra za Ushabiki wa chama (Yanga na Simba) kisha swingers ni wale wasiopenda siasa za ushabiki. hali hii haitusaidii sisi tofauti na nchi za Ulaya au Amerika ambao wanajiunga na vyama kutokana na itikadi zao.

  Mkuu wangu ifike wakati vyama vyetu vifahamu kwamba maana kamili ya uchaguzi ni wao kuuza sera zao kwa wananchi kama vile tunavyopeleka mazao yetu ktk soko huria with a standard inayotakiwa na sii kulazimisha wateja wanunue kile tulichonacho. Fikra kama hizi ndio zile za Kikomunist ambazo tulikua nazo wakati wa Nyerere tukilazimishwa kuchagua mgombea au ukuta, na hakuna tofauti na fikra za viongozi wa CCM leo hii.
   
 15. O

  Ogah JF-Expert Member

  #15
  Oct 19, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Dude....i see de true sub of life brought you back..........lol
   
 16. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #16
  Oct 19, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  hata pale ambapo viongozi walipata nafasi ya kujieleza kwa vyombo vya habari, walijieleza kwa maneno mengi mno, wakieleza mengi mno kwa wakati mmoja bila ya kutusaidia kwa visual aids kiasi cha kuwa maelezo yao yalishindwa kueleweka kwa wapiga kura.

  kampeni hizi zimeingia dosari kubwa kwa kukosekana maelezo ya kina ya namna sera zilivyoainishwa zitakavyoweza kufikiwa na badala yake zimekuwa zikionekana kama kampeni za ahadi hewa.
   
 17. M

  MgonjwaUkimwi JF-Expert Member

  #17
  Oct 19, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 1,288
  Likes Received: 521
  Trophy Points: 280
  Mkuu, heshima. Naona unachanganya mambo kidogo hapa: Demokrasia na Midahalo. Midahalo ya wagombea sio preliquisite ya demokrasia. Chama chochote kina haki ya kukataa au kushiriki katika midahalo, kushiriki au kutoshiriki kamwe hakukuzi wala kudidimiza demokrasia. Tusichanganye dhana ya demokrasia na mijadala/midahalo/debate.

  Na ndio maana kwa maneno yako mwenyewe humesema hivi
  Hujasema kwamba MIDAHALO ndiyo inayowapa wananchi uwezo wa kuchagua chama (Na ningekushangaa kama ungesema ni midahalo ndiyo inayowapa wananchi uwezo wa kuchagua chama). Sasa sera za chama hazipatikani kwenye midahalo ya masaa 2 au kwenye majukwaa, bali zinapatikana kwenye ilani ya vyama husika.  Mkuu, bado unatatizo la kuwianisha sera na midahalo. Chama kinapoundwa lazima kiwe na sera zinazoandikwa kwenye ilani au katiba ya chama. Hizi ndio bidhaa za chama mara kinaposhiriki katika kampeni. Katika kampeni ndiko zinakouzwa sera za vyama. Midahalo ni njia moja kati ya nyingine nyingi za kampeni wala sio sera! CCM wana njia zao za kuuza bidhaa zao (sera zao) na wameamua kwamba hawataki njia ya midahalo. Very simple.

  Swali tunalojiuliza ni kwanini CCM wamechagua kutouza sera zao kwenye midahalo? Fikra za CCM, ambazo nakubaliana nazo kwa 100%, ni kwamba midahalo itawagawa wapigakura wa CCM kwa sababu wapinzani ndio wanaotegemea swing-voters na sio ccm. CCM ni kama mama kuku anayewafunika vifaranga wake (wapiga kura wake) dhidi ya shambulio la mwewe. Tendo la ccm kushiriki katika mdahalo kuna expose wapiga kura wake, hivyo basi hata kama CCM watashinda mdahalo kwa kuja na sera nzuri tayari watakuwa wamegawa vifaranga kadhaa (wapiga kura) kwa mwewe (wapinzani).

  Wengi wetu JF tunazani kwamba kwasababu CCM imeboronga au kwasababu JK sio mzungumzaji mzuri ndio sababu ya CCM kukataa mdahalo. SIO KWELI. Sababu ni kama nilivyotaja hapo juu, kwamba mdahalo una hasara nyingi kuliko faida kwa CCM. CCM inategemea wapiga kura wasiotanga tanga na midahalo itatoa vishawishi vya wapiga kura wa ccm kutanga-tanga na hivyo kunyakuliwa na wapinzani.

  Mkuu, swali au issue ya msingi uliyozungumza ni, je wananchi wanaotaka kupiga kura kutokana na kulinganisha uwezo wa wagombea wakueleza sera zao kwa wakati moja wametendewa haki kwa tendo la CCM kukataa midahalo? Jibu ni kwamba hawajatendewa haki. Lakini CCM wako tayari kukubali hasara hii kuliko hasara ya kushiriki midahalo, na wako tayari kuwaeleza wapiga kura wa namna hii kwamba wapinzani ndio wanaotaka midahalo ili kuuza sera zao, sio CCM kwasababu sera za CCM zinapimika pasipo midahalo. CCM wana kisingizio kwamba hawataki longo longo kwasababu sera zao zinapimika kwa kipindi cha utawala wao. Na ndio maana JK kila anakopita anawakumbusha wananchi mambo ambayo ccm wamefanya.

  CHADEMA, CUF, na wapinzani wengine watajinyonga kisiasa endapo watashiriki midahalo pasipo CCM. Na midahalo itakayoendeshwa pasipo ushiriki wa CCM itainufaisha CCM kuliko wapinzani, UNLESS wapinzani WANAUNGANA. Very simple, kwenye mdahalo wananchi watapenda kujuwa kwanini waendelee kukipa kura chama tawala, kutokuwapo kwa chama tawala kwenye mdahalo kunaikinga ccm na kujenga uadui miongoni mwa wapinzani kwasababu hawatakubaliana na "common enemy" (CCM) na namna ya ku-deal naye (CCM).

  Ni hitimishe kwa kusema kwamba tendo la ccm kukataa mdahalo lina faida kwao. Na tendo la upinzani kuomba ccm washiriki lina faida kwa wapinzani. Wapinzani wakifanya mdahalo bila ccm watajinyonga kisiasa kwasababu maswala ambayo yatakosa majibu au maswala ambayo wapinzani hawatakubaliana kwa pamoja katika mdahalo huo yatajibiwa na CCM kwenye kampeni au yatawafanya wananchi wasioridhika na mdahalo kuendelea kukipigia kura CCM.
   
 18. M

  Mkandara Verified User

  #18
  Oct 19, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  MgonjwaUkimwi,
  Mkuu waonyesha unapenda sana Ubishi pasipo hata kuwa na sababu ilimradi tu ubishane!. Nimesha kwambia kuuza sera ktk mjukwaa ni sawa na kuuziwa mbuzi ktk gunia. Sasa kama wewe unaweza pima na kununua mbuzi kutokana na uzito au maelezo ya muuzaji pasipo kupewa nafasi au muda wa kuuliza huo ni mtazamo wako wewe..Demokrasia haiwezi kuishia ktk misingi na haki ya wananchi kuchagua chama pasipo kuutazama utaratibu unaomwezesha mwananchi huyo kufikia maamuzi ya kuchagua..
   
 19. J

  JokaKuu Platinum Member

  #19
  Oct 19, 2010
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,751
  Likes Received: 4,973
  Trophy Points: 280
  ..mwaka 1995 mdahalo ndiyo uliomuinua Mkapa na kumuangusha Mrema.

  ..anything can happen katika mdahalo. mgombea unayedhani anaweza kufanya vizuri mambo yanaweza kumuendea kinyume na kufanya vibaya.

  ..kwenye nchi za wenzetu, mdahalo ni sehemu muhimu sana ya mchakato mzima wa uchaguzi. ukikimbia mdahalo ni sawa na umewaambia wananchi kwamba huhitaji kura zao. Sara Palin had to attend the VP debate pamoja na kwamba Republicans walijua ni "mweupe pee" na atashindwa vibaya.

  ..inasikitisha kwamba uchaguzi wa mwaka 2010 utakuwa ni wa nne kufanyika bila kuwepo kwa mdahalo wa wagombea Uraisi. kwangu mimi tunarudi nyuma badala ya kusonga mbele.
   
 20. Consultant

  Consultant JF-Expert Member

  #20
  Oct 19, 2010
  Joined: Jun 15, 2008
  Messages: 5,788
  Likes Received: 6,301
  Trophy Points: 280
  Hivi kama JK/CCM wamejitoa, vyama vingine hawawezi kufanya huu mdahalo? - Dr. Slaa, Prof. Lipumba na wale wengine hata majina yao siyajui...

  Inawezekana udhaifu huu wa waandaaji wa mdahalo huu au udhaifu wa vyama vingine vya siasa katika kuhakikisha mdahalo unafanyika ndio unaowapa kiburi CCM kusema hawataki Mdahalo.
   
Loading...