Paparazi Muwazi
JF-Expert Member
- Dec 23, 2007
- 310
- 79
Count Down: Ripoti ya Tume ya Wahariri
Kama ambavyo tuliichambua ripoti ya Kamati ya Bomani sasa ni wakati wa kuichambua Tume ya Wahariri iliyoundwa kuhusu habari za kifo cha Wangwe.
1. Muundo wa Tume: je, wajumbe wake ni bora kiasi gani?
2. Hadidu rejea za Tume: kutafuta chanzo cha habari kufanana, kusibitisha kama habari zile ni za kweli. Kuwa palikuwepo Mapanga, Mashoka nk na kwamba Mbowe alitishiwa kukatwa. Na kwamba familia iliamua post mortem baada ya shinikizo la waombolezaji. Kwa kadiri ya Zitto-hapakuwepo mapanga, mikuki nk na wala Mbowe hakutishiwa kuuwawa kwa silaha hizo. Pia uamuzi wa kuahirisha ulifanyika katika kikao cha familia kabla kwa hiyo pale ilikuwa ni kwenda kutangaza tu. Kwa maneno mengine kelele za waombolezaji ziliingilia tu matangazo ya uamuzi ambao ulishafikiwa tayari?
3. Muda: Tume hiyo ina maliza kazi yake lini?
4. Ripoti: iweje, na itakabidhiwa kwa nani? Je itawekwa hadharani?
5. Hatua: nini kitafanyika baada ya ripoti hiyo?
Mimi nadhani ni vyema tume ikafanya upaparazi kubaini mambo mengine ya nyuma ya pazia na kuyaweka wazi. Mathalani, nani aliandika ile habari, nani alituma iandikwe, nani alilipa gharama, je, ni kweli habari iliandikwa kabla ya tukio? Je, ni kweli kulikuwa kuna kikundi kiliandaliwa kiende na mapanga na kwamba kwa bahati mbaya kikaenda na mabango tu wakati habari tayari ilishasema mikuki na mapanga? Je, ni kweli familia ilipewa na kigogo mmoja rambirambi ya milioni 30? Ni kweli Kepa Peter Wangwe, yule aliyekuwa mwenyekiti wa Halmashauri kupitia CCM na Kaka aliyekuwa mpinzani wa Marehemu wakati wote, alilipwa kuratibu zoezi zima la kutangaza kuwa kifo ni cha Risasi? Maana yeye ndiye aliyesema hadharani na pia ndiye aliyenyanganya bango toka kwa vijana na kulinyosha juu. Je, nini nafasi ya watu kama Waziri Waziri, Vedastus Mathayo(Mb), Mama Kabaka(Mb), Gachuma na Rostam Aziz katika tukio zima? Je, ni kweli msiba mzima ulitumika kama mkakati wa kuivunja CHADEMATarime na kuandaa kampeni za CCM kushinda jimbo hilo? Je, ni kweli viongozi wa TLP, NCCR na CUF walitumia msiba huo kuwapaka matope CHADEMA? Je, nini kinachoendelea Tarime kwa sasa, kwa maana ya habari za mambo yanayojiri? Nini athari za habari zilitolewa kwa wananchi wa Tarime? Hususani suala la Wachagga Vs Makabila mengine Tarime.
PM