Counselling ya nguvu inahitajika - hakuna utani jamani. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Counselling ya nguvu inahitajika - hakuna utani jamani.

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by WomanOfSubstance, Oct 21, 2009.

 1. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #1
  Oct 21, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  "Kwako Mpendwa baba/mama ushauri,
  Pole kwa majukumu ya ujenzi wa taifa.Naomba ushauri kuhusu haya yafuatayo.Niko katika uhusiano imara kwa muda sasa.Sote hatujapanga kuoana ila tunapendana sana.Sijataka kuolewa kwa vile kuna kikwazo .Ndugu wa pande zote wamekataa katakata kuturuhusu kuoana.Sisi tumeona haina haja kubisha wala kuharibu mahusiano ya kifamilia kwa vile ndoa siyo ya mtu mmoja bali ya familia zote mbili.

  Kwa vile tunapendana kupita kiasi, mwenzangu anataka nimzalie angalau mtoto mmoja kama kumbukumbu ya penzi letu.Mimi nina wasiwasi kwa vile najua fika hakuna uwezekano wa kuoana na huyu mkaka.Isitoshe sitataka kubeba jukumu la kulea peke yangu hata kama nitaingia gharama za kumlea mwanangu.Huyo mkaka anasisitiza kuwa atafurahi sana kama nitamzalia na atamkubali mtoto na kuwajibika ipasavyo.Hili kwa kweli linanipa tumaini lakini bado nina wasiwasi.
  Naomba ushauri, Nimkubalie? Nitahakikishaje hatabadili mawazo mbele ya safari"
  Sister L.


  Jamani wale magwiji wa counselling Mbu, Nyamayao, MTM, BAK, MJ1, Za10, Agika, Msindima, FL, Shangazi, Pretty, na wengineo.....hebu msaidieni huyu mwana dada.
   
 2. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #2
  Oct 21, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,646
  Likes Received: 1,472
  Trophy Points: 280
  Nikiwa kama mwingineo, naomba kusema hivi,

  Kwanza angesema kikwazo hasa ni nini kinachoiwafanya wasioane, hao wazazi hawawezi kukataa tu hivi hivi

  tukishakijua then tutamshauri namna ya kukivuka hicho kikwazo ili wafunge ndoa na waepukane na 'kuzaa mtoto tu kama kumbukumbu'

  kama wanapendana kweli hakuna kitakachoshindikana, so

  Kikwazo ni nini?
   
 3. J

  Joyceline JF-Expert Member

  #3
  Oct 21, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 1,010
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  kikwazo ni nini?
   
 4. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #4
  Oct 21, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  Mhhhhhhhh.
   
 5. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #5
  Oct 21, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Ndugu wa mwanaume hawamtaki huyo dada kwa vile alishawahi kuolewa akaachika.Wanataka ndugu yao aoe msichana.Ndugu wa mwanamke nao kusikia hivyo wakaja juu kwamba kama ndugu wa mwanaume hawakutaki, basi kaa hivyohivyo.
   
 6. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #6
  Oct 21, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  ujinga mtupu.....
  Ndugu ndugu ndugu.......

  Kwani lazima waishi tanzania?????si waende kuishi mbali na ndugu........
   
 7. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #7
  Oct 21, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Boss bana!
  Yani unawashauri waende nje ya nchi? Kama hawana uwezo huo je?
   
 8. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #8
  Oct 21, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  I am missing ur PMs!
   
 9. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #9
  Oct 21, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  nje sio lazima ulaya....waende uganda,au kenya au malawi au popote mbali na waswahili

  hata mkoa wa mbali na ndugu pia.....
   
 10. M

  Mtu B JF-Expert Member

  #10
  Oct 21, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 921
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Sister L,

  Kwanza futa hayo mawazo ya 'kumzalia' mtu, kwani we ni ng'ombe, kwamba kakufuga anataka angalao ndama achume faida?

  Binadamu huzaa watoto, hawamzalii mtu yeyote watoto. Mpaka hapo tu nakutahadharisha kuwa utatumika kama ng'ombe tu! Yaani 'umzalie' halafu uchape mwendo kwa kuwa haiwezekani kukuoa? Na wewe unataka kukubali?

  Funguka macho wewe, itakula kwako! Shauri yako.
   
 11. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #11
  Oct 21, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,019
  Likes Received: 23,745
  Trophy Points: 280
  Ndugu wa mume nawapa big up. Kitendo cha kuachika kinamuelezea huyo mdada na ujinga wake. Mwanamke akiachika ni ujinga wake mwenyewe, si mvumilivu na ameshindwa kuilinda ndoa yake mwenyewe. Mwambieni huyo jamaa afuate ushauri wa ndugu zake, aachane na vitu used.
   
 12. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #12
  Oct 21, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,646
  Likes Received: 1,472
  Trophy Points: 280
  Okay, kama kweli ni watu wazima na wanaelewa utaratibu hicho sio kikwazo,

  kama wameachana kwa talaka halali na kisheria inatambulika kuwa ameachika, basi anaweza kufunga ndoa bila kulazimika kuwa na makubaliano na hao ndugu WABAGUZI

  Huyo mwanaume auvae uanaume amshike mkono wapelekane kwa DC ama msikitini ama kanisani wamalize mambo..wanahitaji mashahidi wawili na sidhani kama watawakosa.

  wakimaliza , wachape mwendo wa maisha kama kawa. Hao ndugu watakuja kujutia ushauri wao mbeleni...ila cha muhimu wahakikishe kweli wanakaa pampja na kupendana kiukweli kweli.....
   
 13. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #13
  Oct 21, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,646
  Likes Received: 1,472
  Trophy Points: 280
  dah..mkulu apa umepiga chini ya belt....nilidhani jukumu la kulinda ndoa ni la watu wawili na sio mwanamke peke yake.....

  kisha huku duniani kuna mwanamke au mwanaume asiyekuwa used? hao wapo kwa nadra sana...ndo maana nnimemwambia mkulu fiksiman achangamkie kale ka 16 yers lol
   
 14. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #14
  Oct 21, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Jamani hivi huwa inakuwagaje wale wanaooaga huku ndugu zao wakipinga kuhudhuria harusi zao? Yaani mimi hapa naona asiyekuwa na msimamo ni huyo mwanaume kwani kama alishaolewa akaachika sasa akimuoa ataolewa na hao ndugu?? Huyo mwanaume hajampenda tu msichana kwani yeye ndo mwenye uamuzi wa mwisho wa kuoa au kuacha asisingizie ndugu

  Dada usikubali kuzaa na huyo mwanaume hadi aonyeshe uanaume wake, anapangiwaje maisha na ndugu?
   
 15. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #15
  Oct 21, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Wewe hata sijui unatokeaga wapi kuja kurespond mada kha!!
   
 16. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #16
  Oct 21, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,019
  Likes Received: 23,745
  Trophy Points: 280
  Unajua kuna kitu used ambacho mtumiaji hakujulikana. Lakini hili la used na mtu rasmi! Lol! Tena unaweza kuta alikuwa used for more than ten years.

  Hiyo red hiyo: Biblia inasema mwanamke mpumbavu ataivunja nyumba/ndoa yake mwenyewe.
   
 17. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #17
  Oct 21, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Biblia kweli inasema hivyo but to tell you the truth its more than that!

  Ina maana hao wanawake wanaoachika siku zote huwa ni makosa yao? Yaani lijitu likukere tu, liwe jinga, likutende usiliache kisaa utaitwa mpumbavu lol.
   
 18. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #18
  Oct 21, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Kwanini ukimbie nchi/mtaa/mji/kijiji/nyumba yako? kisa wazazi hawakipendi kitu unachokipenda? Boss, sorry sikubaliani na wewe hapa!

  Suala la msingi ni kujiridhisha kuwa hao wawili wanapendana kweli? au wanatamaniana tu kwa ajili ya kumegana sasa? je, wanapendana ile ya damu damu, kwamba mume anamjua yule mwanamke in and out na yupo ready kumpokea hivyo hivyo alivyo au ni tamaa tu za sasa? kama wanapendana ile ya dhati.......let them do what they think is right to them, wale wazee wao washaoana huko hakuna aliyeingilia issues zao bana!

  But hii kitu ilivyokaka nastuka kidogo......eti ananipenda sana....bac nimwachie alama ya mtoto......what? hapa ndipo wizi upo, huyo bwana hampendi huyo bibie, anamtamani tu pengine ammege na labda azae nae mtoto, then amdamp! Angekuwa anampenda kweli hangesema hivyo, yeye angemwambia potelea mbali mi nakupenda, twende church/msikitini etc wanaosema wacha waseme....duniani kila mmoja huibuka alone na huptea alone.....tuoane no matter what! Wanawake wengi huwa wanadanganywa kirahisi hivihivi.......amwambie no official marriage, no womb ya kumtunzia mtoto wake for 9 months....atafute official chupa za kuzalishia watoto vinginevyo!
   
 19. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #19
  Oct 21, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  mpendwa hebu twambie ni nini kimefanya familia za pande zote mbili zisikubaliane na mahusiano yenu ?
   
 20. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #20
  Oct 21, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,646
  Likes Received: 1,472
  Trophy Points: 280

  hhehe kiongozi mi ni hapo tu,,kwamba mtumiaji unamjua ndo roho inauma? je pale mnapoendesha gari wawili kwa wakati mmoja bila kujuana inakuwaje? si bora huyo aliyetangaza kabisa kuwa sasa ni basi
   
Loading...