COTWU yapinga likizo bila malipo ATCL -Gazeti la habarileo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

COTWU yapinga likizo bila malipo ATCL -Gazeti la habarileo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pdidy, Feb 17, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Feb 17, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,464
  Likes Received: 5,707
  Trophy Points: 280
  Jumanne Feb 17, 2009  Habari za Kitaifa Habari zaidi!
  COTWU yapinga likizo bila malipo ATCL
  Basil Msongo
  Daily News; tuesday,February 17, 2009 @19:56

  Habari nyingine
  Waliokutwa na vyeti haramu Mzumbe wavisafisha
  Dawa mpya ya malaria yazinduliwa
  Anayedaiwa kuuza mtoto aenda kupimwa akili
  Gari lenye maiti laua mtu mmoja
  Viongozi Dodoma wapewa somo
  COTWU yapinga likizo bila malipo ATCL
  Tanzania yathamini misaada ya China
  Masha kushitaki magazeti ya IPP Media
  Mshitakiwa III alia na Zombe
  SMZ, China kuwawezesha wafanyabiashara

  Chama cha Wafanyakazi wa Mawasiliano na Uchukuzi Tanzania (COTWU) kimepinga mpango wa uongozi wa Kampuni ya Ndege (ATCL) kuwapeleka wafanyakazi likizo bila malipo, ingawa wako tayari kuachishwa kazi.

  Taarifa kutoka ndani ya kampuni hiyo zilisema leo kuwa uongozi wa Cotwu ATCL ulitoa msimamo huo kwa Mkurugenzi Mkuu, David Mattaka, katika mkutano uliofanyika leo Dar es Salaam.

  Mmoja wa viongozi wa juu wa Cotwu tawi la ATCL ambaye hakuta jina lake liandikwe gazetini, alisema hawakukubaliana chochote na Mattaka, hivyo walimwomba idhini ya kukutana na wafanyakazi leo, ombi ambalo alilikubali.

  Kwa mujibu wa taarifa kutoka katika mkutano huo, Mattaka aliwaeleza viongozi hao kwamba kinachofanywa na uongozi wa kampuni ni agizo la Serikali la kutaka kupunguzwa kwa idadi ya wafanyakazi ili iweze kujiendesha kwa ufanisi.

  Hata hivyo, wafanyakazi kupitia chama chao, walimweleza Mattaka kuwa wako tayari kuachishwa kazi lakini wanapinga kwenda likizo bila malipo kwa kuwa sheria za kazi hazitambui hilo. Gazeti hili halikuweza kumpata Mattaka kuzungumzia suala hili. Ijumaa iliyopita, wafanyakazi hao walipinga mapendekezo ya kutakiwa kwenda likizo bila malipo baada ya kuelezwa na uongozi kwamba kampuni haiwezi kujiendesha kwa idadi ya sasa ya wafanyakazi na haina fedha za kuwaachisha kazi.
   
 2. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #2
  Feb 17, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Sasa hawa wafanyakazi wa ATCL wanapokataa kwenda likizo bila malipo wanafikiri hiyo mishahara wanayopata kwa wafanyakazi 350 kuhudumia ndege ndogo mbili itatoka wapi?! Ndege zao hazizalishi mapato yakuweza kuwalipa mishahara wafanyakazi wote hao!! Serikali imeahidi bungeni kuwa muwekezaji wao Mchina atanunua ndege tisa kwahiyo mantiki ya kuwapeleka leave bila malipo ni kwamba kwa sas shirika halina uwezo wa kuwabeba wote,mara shirika litakapotengemaa watarudishwa kazini!! Wanaposema kwamba wao wanataka wawe retrenched maana yake wanataka kuliuwa shirika? Katika hali kama hii anayeamua nani aendelikizo au kuwa retrenched ni nani kati ya mwajili na mwajiriwa?? Ushauri wangu kwa menejimenti ni kuwa wawape barua za leave without pay wafanyakazi walioamua waende leave na kama hawakurudhiki na uamuzi basi waende mahakamani kuseek redress kuliko kuwaweka watu bila kazi wakingojea mishahara ya bure!! Ningeishauri bodi pia iangalie uwezekano wa kupunguza mishahara ya top mangement wakati huu inapochukua austerity measures kwa wafanyakazi wengine; haingii akilini kuendelea kumlipa CEO $ 11,000.oo kwa mwezi wakati kampuni ni mufilisi; haya ndio mambo yanyowafanya wafayakazi waichukie management kwani haioneshi kuwa nayo inabeba mzigo wa kinusuru kampuni!!
   
 3. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #3
  Feb 18, 2009
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Wafanyakazi wapo pale ATCL kwa mujibu wa sheria za kazi na mkataba walionao baina yao na mwajiri. Kwa vile kila jambo linahitaji lifanywe kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizopo basi ipo haja kwa ATCL iwajibike kwa kadri ya mkataba uliopo kati yake na wafanyakazi huku ikifuata sheria za kazi.
  Wafanyakazi wa ATCL siyo 'mbuzi wa shughuli' walisha-sacrify tangu EAA, ATC, ATCL-SAA sasa na bado mnataka kuwatosa katika ATCL-Mataka?

  Leo hii wafanyakazi waliokuwa watumishi wa EAC wanahangaika kupata haki zao lakini hakuna jibu lolote mwafaka, sasa iweje hao unaowataka kuwapeleka likizo kwa sababu tu huna uwezo wa kuwalipa kutokana na kutokuwajibika kwa kundi dogo la watu wachache (Viongozi)?

  Ninakumbuka wakati ATCL ilipokuwa-grounded wiki kadhaa zilizopita Mh Waziri wa Miundo Mbinu Shukuru Kawambwa alionesha kupwaya kabisa katika kufikia kufanya maamuzi hadi akapeleka issue kwa Prime Minister. Baada ya kutoka kwa Prime Minister, kama kawaida ikatafutwa njia ya kupoteza wakati kwa kuwa-engage wale maprofesa kupitia mambo kadhaa, lakini hadi leo ile ripoti haijatolewa kwa public na badala yake kuna maamuzi yanaendelea kama haya ya kutaka kuwapeleka wafanyakazi likizo, je Mh Waziri hayo ndiyo uliyauliza kutoka kwa maprofesa? Tatizo la ATCL linajulikana ni uongozi mbovu, sasa kulikoni Mh Waziri unaonekana huwezi kufanya maamuzi hadi Prime Minister aseme au Rais for this case, je ndiyo kusema kuwa huna uwezo 'unabebwa'?

  Ninachowashauri wafanyakazi wa ATCL wakumbuke ushauri niliowahi kuandika kupitia hapa JF kuwa ni wakati mwafaka kwao kuomba kuwa-retrench na kupatiwa haki zao na huyo anayetaka kuendelea na ATCL atafute au aajiri wafanyakazi wengine. wengi wa wafanyakazi wa ATCL hawako radhi kuendelea kufanya kazi na Mattaka, kwahiyo ni vema minority group (Rais na wasaidizi wake) ambayo ina nguvu ya kufanya maamuzi ifikirie kuwa haiwatendei haki majority (wafanyakazi) ambao hawana nguvu ya kufanya maamuzi .
   
 4. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #4
  Feb 18, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,464
  Likes Received: 5,707
  Trophy Points: 280
  mod,tunaomba kwa muda!!!
  Habari zilizotufikia hivi punde zinasema yale malalamiko yote yakupelekwa likizo bila mapo pale ATCL yametokana na maagizo ya mh waziri wa miundo mbinu mh THANKSKWAMBWA,taarifa tulizozipata hivi punde zinasemaa
  Mh mattaka alikuwa na kikao na chaama cha wafanyakazi,,kuhusu lini wafanyakazi waende likizo bila malipo,kabla ya hapo mh mattaka alikuwa na mkutano na wafanyakazi,na baada ya kubanwa sana na kuulizwa huu ni uamuzi wa nani ndipo alipomtaja MH THANKS-KAWAMBWA ndie aliemwambia na bado anaendelea kumshurutisha wafanyakazi wa atcl waende likizo bila malipo......anyway hayo ni mambo ya atcl ila swali langu labda kwa mh kawambwa

  1))
  Je kuna sheria ambayo inayoipa mamlaka muajiri kumpeleka mtu likizo bila malipo

  2)JE AONI SWALA LA KUMSHURURTISHA HUYU BWA MATATAKA NI KULIZALILISHA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO,MAANA ALISEMA KWA MDOMO WAKE AMEUNDA TUME AMBAYO MPAKA LEO HII AJAITOA HADHARANI

  3))JE MH MATTAKA AONI KITENDO CHA KULAZIMISHA WATU KWENDA LIKIZO BILA MALIPO NI KUINGILIA MAAMUZI YA MH WAZIRI,,MAANA MH WAZIRI AMESEMA BUNGENI AMESHAKABIDHIWA MAPENDEKEZO NA TUME,ANAYATOLEA MAJIBU MUDA SI MREFU...

  4)JE AONI KUNA UMUHIMU WA KUFANYA HARAKA KUTOA HAYO MAPENDEKEZO HADHARANI YASIISHIE KAMA TUME ZA SIASA ZILIZOKUWA
  ZIKUNDWA NA MWISHO KUISHIA KWENYE MAKABATI

  5())MH WAZIRI KAWAMBWA TUNATUMAINI UNAJUA TUME NZIMA ILIUNDWA KWA MADHUMUNI GANI,NA WAMETUMIA SEHEMU YA PESA ZA WALIPA KODI KATIKA KUFANIKISHA HILI,JE UONI KUNA UMUHIMU WA KUTOA ,AA,UZI YA HARAKA KUTOKANA NA MAPENDEKEZO YA HUMO NDANI ILIWATU WAWE NA IMANI NA WEWE

  USHAURI WA BURE MH WAZIRI:

  ---KAMA UNAKUMBUKA MGOGORO WA MASHIRIKALA POSTA,,NI VYEMA UKAENDA UKAWAONA WAFANYAKAZI WA ATCL NA KUWAHOJI MATATIZO YAO KABLA YA KUKIMBILIA KUTOA USHAURI WA KUWAPELEKA WAFANYAKAZI AJUMBANI.....]

  ---PILI UKIWA NA WAFANYAKAZI WATAKUELEZA WAZI TATIZO LA VIONGOZI WAO KULIKO KUSIKILIZA STORY ZA KWENYE BAR AMA ZA MITAANI...NA HILI NDILO LINALOCHANGIA SANA MAWAZIRI MENGI KUARIBU MASHIRIKA YAO HUSIKA

  Kwa kweli kama ni kweli habari iliyonenwa na mh huyu kuhusu kuwaumiza wafanyakazi hao,natumaini ulitakii mema shirika lako ,ama kuna hujuma kubwa ambayo inaendelea uko juu pasipo kushirikishwa wafanyakazi,,ndio maana nilisema sikumoja nikichangia atcl, kwa style ya mashirika ya bongo wacha nibebe mabox mpaka mwisho.......

  MWANANATURE
   
 5. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #5
  Feb 18, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,464
  Likes Received: 5,707
  Trophy Points: 280
  Re: wafanyakazi ATCL wapewe likizo bila malipo-WAZIRI KAWAMBWA

  --------------------------------------------------------------------------------

Loading...