Costa Mahalu awaaambia waandishi wa habari wasome Zaburi 17 kwenye Biblia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Costa Mahalu awaaambia waandishi wa habari wasome Zaburi 17 kwenye Biblia

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mamboleo, Aug 10, 2012.

 1. M

  Mamboleo Member

  #1
  Aug 10, 2012
  Joined: Oct 15, 2008
  Messages: 69
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 15
  Alipoulizwa maoni yake kuhusu hukumu ya mahakama dhidi ya mashtaka aliyokabiliwa nayo..Prof.Costa Mahalu aliwaomba waandishi wasome zaburi 17...(very powerful verse)

  [h=1]Zaburi 17[/h] 1 Ee Bwana, usikie haki, ukisikilize kilio changu, Utege sikio lako kwa maombi yangu, Yasiyotoka katika midomo ya hila.
  2 Hukumu yangu na itoke kwako, Macho yako na yatazame mambo ya adili.
  3 Umenijaribu moyo wangu, umenijilia usiku, Umenihakikisha usione neno; Nimenuia kinywa changu kisikose,
  4 Mintarafu matendo ya wanadamu; Kwa neno la midomo yako Nimejiepusha na njia za wenye jeuri.
  5 Nyayo zangu zimeshikamana na njia zako, Hatua zangu hazikuondoshwa.
  6 Ee Mungu, nimekuita kwa maana utaitika, Utege sikio lako ulisikie neno langu.
  7 Dhihirisha fadhili zako za ajabu Wewe uwaokoaye wanaokukimbilia; Kwa mkono wako wa kuume Uwaokoe nao wanaowaondokea.
  8 Unilinde kama mboni ya jicho, Unifiche chini ya uvuli wa mbawa zako;
  9 Wasinione wasio haki wanaonionea, Adui za roho yangu wanaonizunguka.
  10 Wameukaza moyo wako, Kwa vinywa vyao hutoa majivuno.
  11 Sasa wametuzunguka hatua zetu, Na kuyakaza macho yao watuangushe chini.
  12 Kama mfano wa simba atakaye kurarua, Kama mwana-simba aoteaye katika maoteo yake.
  13 Ee Bwana, usimame, umkabili, umwinamishe, Kwa upanga wako uniokoe nafsi na mtu mbaya.
  14 Ee Bwana, kwa mkono wako uniokoe na watu, Watu wa dunia hii ambao fungu lao li katika maisha haya. Matumbo yao wayajaza kwa hazina yako, Hushiba wana, huwaachia watoto wao akiba zao,
  15 Bali mimi nikutazame uso wako katika haki, Niamkapo nishibishwe kwa sura yako.
   
 2. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #2
  Aug 10, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,482
  Likes Received: 5,554
  Trophy Points: 280
  Mahalu bwana aliyekuepusha na hili usimuache kamwe!!!!!!!!!!
   
 3. K

  Kyachakiche JF-Expert Member

  #3
  Aug 10, 2012
  Joined: Feb 16, 2009
  Messages: 910
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  Duh! Hapo kamaliza kila kitu. Sijui ingekuwa busara mtu amprintie JK!!!!
   
 4. N

  NnyaMbwate JF-Expert Member

  #4
  Aug 10, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,398
  Likes Received: 524
  Trophy Points: 280
  Atamwomba Mzee M.a.k.a.m.b.a. amsomee na kum-tafsiria.
   
 5. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #5
  Aug 10, 2012
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Ni kupoteza tuu karatasi kumprintia, maana amesha printiwa vitu vingi sana, tumuachie Mungu atuepushe na majanga yanayoweza kuendelea kuliandama Taifa chini ya Utawala wa Kikwete. Kama ishu ya Ulimboka tuu anajifanya hausiki na Gazeti lilitoa ushahidi ameishia kulifungia bila kukanusha aliyoandika kwa maelezo ya kina.
   
 6. Chiwa

  Chiwa JF-Expert Member

  #6
  Aug 10, 2012
  Joined: Apr 17, 2008
  Messages: 1,281
  Likes Received: 584
  Trophy Points: 280
  kwa mazingira haya hata kama ulivuta mwisho wa siku uliomba msamaha kwa makosa uliyo fanya.ila lililokubwa zaidi ambalo nafsi yangu imependa ni jinsi ulivyokuwa karibu na Mungu na kumtegemea na kizuri zaidi ulikuwa karibu na familia na watu wako wa karibu. hivyo kama jamii tuna kitu cha kujifunza kwako lakini kama nchi tuna hasara ya kukulipa kwa kesi za kukurupuka kwa uzembe kwa kutokuwa makini katika manunuzi.
  najua umo humu na salamu zangu zitakufikia endelea kumtegemea Mungu zaidi si kwa shida na uwaelekeze wenzako kuwa haya maisha ya ufisadi hayana maana hata kidogo watende haki na wawaonee huruma watanzania wanateseka kwa ajili ya wizi wao.
   
 7. Zemu

  Zemu JF-Expert Member

  #7
  Aug 10, 2012
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 517
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Walitaka kumvisha Gamba Prof na Grace wakati wao ndo MAGAMBA wakuu, Mungu ni mwema sasa wameumbuka aisee. Zaburi hio inawafaaa MAGAMBA wote huko waliko.
   
 8. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #8
  Aug 10, 2012
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,100
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  M,kwere anatia aibu, yaani alitaka ampeleke Mahalu akaolewe jela wakati hana hatia kabisa
   
 9. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #9
  Aug 10, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,200
  Likes Received: 3,810
  Trophy Points: 280
  Mahalu ukweli unaujua wewe. mimi sina shaka uliliibia taifa hili. Nafsi yako itakusuta mpaka kaburini. Unanukuu vifungu vya biblia wakati unajua fika uliiba. Mahakama zetu hazina ukweli ukiondoa Court of appeal na kidogo high court. Kisutu ndio bure kabisa, we unajua! Weka hukumu tukupe mapungufu yake! Unajua!!
   
 10. A

  APAUKUNDI New Member

  #10
  Aug 10, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Mungu ni mwema huwalipa watu wake kwa uaminifu. Costa nakupongeza sana
   
 11. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #11
  Aug 10, 2012
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,100
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  M,kwere anatia aibu, yaani alitaka ampeleke Mahalu akaolewe jela wakati hana hatia kabisa.
  Fisadi ni yeye na mwanawe mpenzi Riz zero na wanataka waliingize taifa letu vitani ili waanze kuliuzia jeshi silaha.
  Hakika Riz Zero na baba yake wana mwisho mbaya
   
 12. NG'OMBE

  NG'OMBE JF-Expert Member

  #12
  Aug 10, 2012
  Joined: Mar 26, 2011
  Messages: 362
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Waovu hawatashindana na mwenye haki kamwe, JK aliweza kumkandamiza Babusea akaona inawezekana kwa kila mtu, wengine haiwezekani mzee.
   
 13. Mlangaja

  Mlangaja JF-Expert Member

  #13
  Aug 10, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 541
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Katika tafsiri nyingine za Kiswahili
  Habari njema
  1 Ee Mwenyezi-Mungu usikie kisa changu cha haki,

  usikilize kilio changu,

  uitegee sikio sala yangu isiyo na hila.

  2 Haki yangu na ije kutoka kwako,

  kwani wewe wajua jambo lililo la haki.  3 Wewe wajua kabisa moyo wangu;

  umenijia usiku, kunichunguza,

  umenitia katika jaribio;

  hukuona uovu ndani yangu,

  sikutamka kitu kisichofaa.

  4 Kuhusu matendo watendayo watu;

  mimi nimeitii amri yako,

  nimeepa njia ya wadhalimu.

  5 Nimefuata daima njia yako;

  wala sijateleza kamwe.

  6 Nakuita, ee Mungu, kwani wewe wanijibu;

  unitegee sikio, uyasikie maneno yangu.

  7 Onyesha fadhili zako za ajabu,

  uwaokoe kutoka kwa adui zao,

  wale wanaokimbilia usalama kwako.  8 Unilinde kama mboni ya jicho;

  unifiche kivulini mwa mabawa yako,

  9 mbali na mashambulio ya waovu,

  mbali na adui zangu hatari wanaonizunguka.

  10 Hao hawana huruma yoyote moyoni;

  wamejaa maneno ya kujigamba.

  11 Wananifuatia na kunizunguka;

  wananivizia waniangushe chini.

  12 Wako tayari kunirarua kama simba:

  kama mwanasimba aviziavyo mawindo.

  13 Inuka, ee Mwenyezi-Mungu,

  uwakabili na kuwaporomosha.

  Kwa upanga uiokoe nafsi yangu kutoka kwa waovu.

  14 Mkono wako, ee Mwenyezi-Mungu uniokoe kwa watu hao,

  watu ambao riziki yao ni dunia hii tu.a

  Uwajaze adhabu uliyowawekea,

  wapate ya kuwatosha na watoto wao,

  wawaachie hata na wajukuu wao.  15 Lakini mimi nitauona uso wako, kwani ni mwadilifu;

  niamkapo nitajaa furaha kwa kukuona.


  Tafsiri ya Neno
  1 Sikia, Ee BWANA, kusihi kwangu kwa haki, sikiliza kilio changu. Tega sikio kwa ombi langu, hayatoki kwenye midomo ya udanganyifu.
  2 Hukumu yangu na itoke kwako, macho yako na yaone yale yaliyo haki.

  3 Ingawa unauchunguza moyo wangu na kunikagua usiku, ingawa umenijaribu, hutaona cho chote, nimeamua kwamba kinywa changu hakitatenda dhambi.

  4 Kuhusu matendo ya wanadamu, kwa neno la midomo yako, nimejiepusha na njia za jeuri.

  5 Hatua zangu zimeshikamana na njia zako, nyayo zangu hazikuteleza.

  6 Ee Mungu, ninakuita, kwa kuwa utanijibu, unitegee sikio lako na usikie ombi langu.

  7 Uonyeshe ajabu ya upendo wako mkuu, wewe uokoaye kwa mkono wako wa kuume wale wanaokukimbilia kutokana na adui zao.

  8 Nilinde kama mboni ya jicho lako, unifiche chini ya kivuli cha mbawa zako

  9 kutokana na waovu wanaonishambulia, kutokana na adui wauaji wanaonizunguka.

  10 Wamefunga mioyo yao migumu, vinywa vyao husema kwa kiburi.

  11 Wamenifuatia nyayo zangu, sasa wamenizingira, wakiwa macho, waniangushe chini.

  12 Wamefanana na simba mwenye njaa awindaye, kama simba mkubwa anyemeleae mafichoni.

  13 Inuka, Ee BWANA, pambana nao, uwaangushe, niokoe kutokana na waovu kwa upanga wako.

  14 Ee BWANA, mkono wako uniokoe na watu wa jinsi hii, kutokana na watu wa ulimwengu huu ambao fungu lao liko katika maisha haya. Na wapate adhabu ya kuwatosha. Watoto wao na wapate zaidi ya hayo, hukumu na iendelee kwa watoto wa watoto wao.

  15 Na mimi katika haki nitauona uso wako, niamkapo, nitaridhika kwa kuona sura yako.
   
 14. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #14
  Aug 10, 2012
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Watanzania mbona tunakuwa wajinga kupindukia mtu kafanya ufisadi wa Euro 2 Milioni pesa za walipa kodi leo amekuwa shujaa kisa kawambia someni Zaburi 17 kwa nini sasa tunaangaika na kina Chenge, Rostam, Fisadi aibwaga serikali.
   
 15. Ufunuo

  Ufunuo JF-Expert Member

  #15
  Aug 10, 2012
  Joined: Jun 6, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  hawajatupa mistari ya kusoma neither katika quruan nor bible.
   
 16. M

  Mjenda Chilo JF-Expert Member

  #16
  Aug 10, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 1,425
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 145
  Tafakari kati yako na hao wengine nani mjinga, Hakimu kakwambia ukiacho Costa yule dada hakuwa na hata sababu ya kufunguliwa mashtaka, sasa kama ndivyo kwanini hakumtoa kwenye no case to answer? mashinikizo ni sooo!
   
 17. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #17
  Aug 10, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Hapa kuna nini kimejificha, mbona sielewi?
   
 18. J

  JokaKuu Platinum Member

  #18
  Aug 10, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,730
  Likes Received: 4,949
  Trophy Points: 280
  ..mimi nadhani huyu amewazidi wenzake ujanja ndiyo maana wamepeleka mahakamani.

  ..haiwezekani Balozi acheze michezo michafu hivyo bila serikali[raisi,waziri wa mambo ya nje, waziri wa fedha] kuwa na habari na kinachoendelea.
   
 19. Young Tanzanian

  Young Tanzanian JF-Expert Member

  #19
  Aug 10, 2012
  Joined: Mar 10, 2012
  Messages: 1,740
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  In god we trust..time will tell.
   
 20. m

  mwita ke mwita JF-Expert Member

  #20
  Aug 10, 2012
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 5,470
  Likes Received: 1,211
  Trophy Points: 280
  tafsiri nyingine ya kiswahili kwa zaburi ya 17
  [h=6]Sikia, Ee BWANA, kusihi
  kwangu kwa haki, sikiliza kilio changu.
  Tega sikio kwa ombi langu,
  hayatoki kwenye midomo ya udanganyifu.
  2Hukumu yangu na itoke kwako,
  macho yako na yaone yale yaliyo haki.
  3Ingawa unauchunguza moyo wangu na
  kunikagua usiku,
  ingawa umenijaribu, hutaona cho chote,
  nimeamua kwamba kinywa changu
  hakitatenda dhambi.
  4Kuhusu matendo ya wanadamu, kwa neno
  la midomo yako,
  nimejiepusha na njia za jeuri.
  5Hatua zangu zimeshikamana na njia zako,
  nyayo zangu hazikuteleza.
  6Ee Mungu, ninakuita, kwa kuwa utanijibu,
  unitegee sikio lako na usikie ombi langu.
  7Uonyeshe ajabu ya upendo wako mkuu,
  wewe uokoaye kwa mkono wako wa
  kuume wale wanaokukimbilia
  kutokana na adui zao.
  8Nilinde kama mboni ya jicho lako,
  unifiche chini ya kivuli cha mbawa zako
  9kutokana na waovu wanaonishambulia,
  kutokana na adui wauaji wanaonizunguka.
  10Wamefunga mioyo yao migumu,
  vinywa vyao husema kwa kiburi.
  11Wamenifuatia nyayo zangu,
  sasa wamenizingira,
  wakiwa macho, waniangushe chini.
  12Wamefanana na simba mwenye njaa
  awindaye,
  kama simba mkubwa anyemeleae
  mafichoni.
  13Inuka, Ee BWANA, pambana nao,
  uwaangushe, niokoe kutokana na waovu
  kwa upanga wako.
  14Ee BWANA, mkono wako uniokoe na
  watu wa jinsi hii,
  kutokana na watu wa ulimwengu huu
  ambao fungu lao liko katika maisha
  haya.
  Na wapate adhabu ya kuwatosha.
  Watoto wao na wapate zaidi ya hayo,
  hukumu na iendelee kwa watoto wa
  watoto wao.
  15Na mimi katika haki nitauona uso wako,
  niamkapo, nitaridhika kwa kuona sura
  yako.
  [/h]
   
Loading...