COSOTA kuanza kuchaji mirahaba desemba mwaka huu

dope bwoi

JF-Expert Member
Feb 25, 2009
234
591
COSOTA imesema wasanii watapata 70% na serikali itachukua 30% ya mirahaba itakayokusanywa kutoka kwenye vituo vya redio, TV na maeneo mengine yanayocheza nyimbo za wasanii kuanzia Desemba 2021. Serikali imeeleza hiyo 30% itaiwezesha kufika maeneo mengi zaidi kukusanya fedha hizo.
 
Wasanii wengi wanahonga hizi media ili nyimbo zao zipigwe. Ama muziki utashuka, au wasanii hawatapata wanachostahili.

Ni vema serikali ingechunguza kabla ya kuamua.
Kwani hadi dunia hii ya leo bado watu wanaotegemea radio kusikiliza mziki.. Mimi wangesema habari sawa mziki
 
Ata sijaelewa naomba msaada jaman wa ufafanuzi zaidi. Ni kwamba wamiliki wa hizo stations wanatakiwa kulipia wimbo kabla ya kupiga kwenye vituo vyao ama?
 
Kwani hadi dunia hii ya leo bado watu wanaotegemea radio kusikiliza mziki.. Mimi wangesema habari sawa mziki
Wanasema si redioni tu ni maeneo yote ya kibiashara yanayo cheza muziki.
Kwa mfano salon, hoteli au migahawa n.k
 
utaratibu wao si rafiki na utawaumiza zaidi wasanii wachanga, wao wangeunda mfumo ambao ungewaregister wachoma miziki wote wa kitaa kisha wakawa wanakatwa asilimia kadhaa kwa kila wimbo maana hawa ndo wanafanya biashara kubwa ya muziki bila kulipia chochote.
 
Wasanii wengi wanahonga hizi media ili nyimbo zao zipigwe. Ama muziki utashuka, au wasanii hawatapata wanachostahili.

Ni vema serikali ingechunguza kabla ya kuamua.
Kwenye tozo za miamala na kodi za nyumba hawajafikiria kweli watafikiria hiyo 30% ya msanii
 
Hakuna wimbo wa msanii mchanga utakaopigwa, nyimbo za nje zitapa airplay zaidi.
Producers asilimia yao ni ngapi kwani wao ndio watengeneza beats ambazo haswa ndiyo muziki kabla hata muimbaji hajaingiza maneno yake.
Artists watawekeza nguvu zaidi kwenye digital platforms ila najua hii serikali na huko lazima itawazamia ili iwe inachota asilimia za kutosha.
 
Wasanii ni wapumbavu sana, sio kila kitu wanaiga tu. Yani radio stations zitaacha kupiga nyimbo za baadhi ya wasanii ndio watakoma.
 
Back
Top Bottom