Cosota Inahitaji Msaada

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
213
Kwa Tanzania haswa maeneo ya mijini ni kitu cha kawaida kabisa kukuta sehemu nyingi tu za kukodisha filamu kwa mfumo wa dvd , cd na kanda za kawaida biashara hii kwa sasa imekuwa sana na vijana wanajitahidi kufungua vibanda tu kadri wanavyoweza .

Ukiachilia kukodisha hizo dvd na cd vibanda vingi ndani yake wanakazi moja ni kutengeneza nakala zaidi ya hizi dvd na cd kama sio kutengeneza nakala basi wengine huhifadhi hizi filamu na miziki katika computer zao ili baadaye watu wakienda basi watengenezewe .

Kwa kawaida cd moja ya nyimbo karibu 12 kwa bei ni alfu 2 ukipeleka hela hiyo upata nakala yako ya audio , kama unataka mp3 basi hufikia mpaka alfu 4 au 5 , kutengeneza dvd ni alfu 350 mpaka alfu 5 kutegemea na maeneo .

Ukienda kule kariakoo katika maduka wanayouza hizi cd zinazoitwa ndio original utakuta mfano dvd ni alfu mbili miatano kwa bei ya jumla mitaani ndio wanauza alfu 4 mpaka 5 inategemeana wingi wa filamu katika dvd husika .

Kwa upande wa pili watu haswa wasanii wetu wamekuwa wanalalamika sana kuhusu kazi zao kuibiwa na kutengenezwa upya bila idhini yao bila kusikilizwa au bila watu wa upande wa pili haswa wanaohusika na ICT kuwasaidia kwa namna moja au nyingine .

Upande wa tatu chama cha hati miliki COSOTA nacho kimekaa kimya hakina jipya siku zote tunaona matangazo ya kazi katika magazeti hawa watu sijui huwa wanaacha kazi pale baada ya muda au sijui inakuwaje pengine COSOTA hawajapewa meno basi waombe .

Naamini tunaweza sana kuwabana wanaofuja hizi kazi za wasanii wa nyumbani hata wa nje kama tukiamua kushirikiana na wadau wa muziki kuna mbinu nyingi za kufanya na kutekeleza kuanzia COSOTA kwenyewe .

Huwa nashangaa sana niposikia nyimbo imetoka leo jioni unaikuta sehemu inapigwa au Fulani anayo tayari inatia uchungu sana ukiangalia gharama ambazo msanii ametumia katika kuandaa nyimbo hiyo na mambo mengine .

Tunapoamua kupambana na hali hii tuhakikishe pia katika hizi studio za kutengeneza miziki na ala za muziki napo wanakuwa na programu maalumu au vyombo maalumu vya kutengenezea hizi CD na DVD kutoka labda COSOTA kazi inapotengenezwa inawekewa aina Fulani ya ulinzi .

Mfano kuna baadhi ya CD za programu za computer zimewekewa alama Fulani ambapo ukiingiza katika deki ya kudouble haita onekana ni vitu kama nyuzi na hizi nyuzi computer nyingi hazina uwezo wa kuzisoma hii ni moja ya tekinologia hiyo .

Pili nyimbo hizi zinavyotengenezwa kuna uwezekano wa kuweka codecs ( ingawa kwa privacy ni mbaya ) nyimbo au video hiyo ukiiweka katika mtandao itatakiwa kudownload codecs kutoka katika tovuti ya COSOTA au sehemu yoyote ilipohifadhiwa sasa hapa codes zinaweza kuuzwa kwa njia ya mtandao ukinunua unakuwa umenunua kazi halisi .

Wale wote wenye tovuti zinazopiga au kuweka miziki na sanaa ya kitanzania wawe na na utratibu wao jinsi wanavyolipa kodi au kulipisha watu wanaopata huduma hiyo la sivyo wakate miziki hiyo vipande kama intro tu basi .
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom