COSOTA ilikuwa sahihi kuwa chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara

Interest

JF-Expert Member
Apr 11, 2015
3,434
7,055
Nimesikia COSOTA inahamishiwa Wizara nyingine, na tamko hilo lilivyotoka Wasanii wakashangilia sana. Ni dhahiri kuwa hawajui hata wanachokishangilia.

Tatizo sio nini kipo chini ya nini, bali huko huko kilipo je, kinawezeshwa kwa kiwango kipi?!

Hebu ngoja tuwekane sawa kidogo...

COSOTA ni Copyright Society of Tanzania. Ikimaanisha ni chombo kinachosimamia HAKIMILIKI. Hakimiki ni "Haki ya mwenye kitu cha Ubunifu kiuhalali kukitumia KIBIASHARA" yeye au kwa kumruhusu mwingine kwa makubaliano.

Hivyo ni sawa kuwa chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara.

Copyright inamlinda sio Msanii tu, bali hadi Prodyuza, muandishi wa vitabu, mbunifu wa vipindi vya Luninga, Filamu, Tamthilia, etc.

Ni ubinafsi wa hali ya juu, kwa sisi Wanamuziki kujiona kama Cosota ni yetu peke yetu, na hivyo basi ipelekwe kule tunapotaka sisi ilimradi tu.

Muziki una sura nyingi; SANAA, UTAMADUNI, BURUDANI, BIASHARA.

Ni sahihi kwa muziki kusimamiwa na taasisi tofauti tofauti kulingana na sura husika.

Sasa kuhamishia aspect ya Biashara chini ya Wizara ambayo inaweka emphasis on Utamaduni na Sanaa, kweli jamani?!

Kisa BIMA, LESENI, GARAGE, PETROL STATION na CAR WASH vinahusiana na "Gari", haimaanishi kuwa lazima vyote viwe sehemu moja ila mambo yaende.

Cha msingi ni popote huko vilipo basi vifanye kazi kwa ufasaha.

Cha kuchekesha sidhani hata kama 40% ya artist wamejiandikisha COSOTA.

Alafu haya mambo ya kuchanganya Utamaduni (na Sanaa) juu ya Biashara, ndio yanadumaza ukuaji wa muziki wetu kibiashara. Biashara ya Sanaa imekuwa "global", "urban" na "cross-cultured". Ila sisi tunasingizia MAADILI ya Kitanzania kila siku, na kubana Artistic Expressions. It's Sad

COSOTA hata iwekwe Wizara ya Fedha (and same goes for BASATA), hazitofanya vizuri kama hakutokuwa na fungu lililotengwa la kuwezesha utendaji wa taasisi hizo.

Shida yetu sio Cosota na BASATA zipo wapi, bali ZINAFANYA NINI na KWA UWEZESHWAJI UPI.

Je vipaumbele vyetu ni VIPI?!

Ikumbukwe kuwa COSOTA haina ofisi mikoani na ndio maana pia tupo chini ya Wizara ya TAMISEMI, sababu Maafisa Utamaduni (Serikali Za Mitaa) ndio hutumika kukusanya Mirabaha yetu. Had COSOTA been properly funded, that wouldnt be the case.

Wasanii vipaumbele vyetu ni vipi ?!

Ni vyema ku-address changamoto zetu za msingi kwanza, badala ya kufanya kitu cha "kisiasa" ambacho hakina manufaa direct ya kiuchumi kwa Wasanii.

• Malipo Hafifu
• Mirabaha
• Mfuko Wa Hifadhi
• Bima ya Afya
• Standardized Venue
• Music Academy
• Local Playlist
• Archives

Kiukweli, na hizi ni rai zangu; Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo imepewa majukumu mengi na makubwa sana kwa wao kuweza kufanikisha majukumu efficiently & effectively.

Zivunjwe na kuwa "HABARI" na "MICHEZO NA BURUDANI" badala ya kuongeza aspect ya Biashara ndani yake.

Leo kuna sherehe ya kuhamishia COSOTA huko Wizara nyingine, ila ukweli ni kwamba hiyo sio solution hata kidogo.

Wasanii hawajui vipaumbele vyao, na wengi wao hata hiyo move hawajui ina implications gani. Nimalizie tu kwa kusema...

"ULIMBUKENI WA WASANII NI MGODI WA WANASIASA".

Imeandikwa na Webiro Wasira (WAKAZI) - Msanii wa muziki na Mwanasiasa.
 
Na kiwanda kizima cha wasanii wamekimbilia kuchukua fomu wanataka kwenda bungeni.

Back
Top Bottom