COSOTA, CMEA kuanza kulipa mirahaba kwa wanamuziki kuanzia Januari mwakani

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
attachment.php

Chama cha Hakimiliki Tanzania (Cosota) kwa kushirikiana na kampuni ya kusimamia kazi za wanamuziki nchini Copyrights Management East Africa Limited (CMEA) wataanza kulipa mirabaha ya wanamuziki na wadau wake kuanzia mwakani.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Cosota, Doreen Sinare alisema kuwa wanamuziki, watunzi na maproducer watalipwa asilimia 60 kwa kila wimbo au video itakayochezwa katika redio na televisheni yoyote ndani na nje ya nchi kwa kutumia vifaa bora vilivyowekwa na kampuni ya CMEA.

Doreen alisema kuwa manamuziki, msanii alitakiwa kupata asilimia 70 ya kazi yake, lakini asimilia 10 itakatwa katika malipo hayo na kuingia katika mifuko ya jamii kwa mahitaji yake ya baadaye.

Alisema kuwa wanamuziki ni sawa na wafanyakazi wengine na asilimia 10 hiyo itamwezesha kujipatia kipato chake kama ilivyo kwa wafanyakazi wengine katika taasisi mbalimbali.
attachment.php

Kwa mujibu wa Sinare alisema kuwa ili kuhakikisha kila mwanamuziki anafaidika na kazi yake, watashirikiana na vyama vingine vya Hakimiliki katika nchi mbali mbali kwa kutumia hati ya malipo zinazotokana na bei za matangazo kwa televisheni na vituo vya redio.

Alisema kuwa Cosota na CMEA pia watawapa ushirikiano vyama hivyo ili nao waweze kupata haki za malipo ya wanamuziki wao kwa vituo vya televisheni na redio vitakavyotumia kazi za wanamuziki wa nje.

Lengo la Cosota na CMEA ni kuona wasanii wanafaidika na kazi zao, mirabaha ya kwanza tutaanza kulipa Januari 2 na kwa sasa tupo katika hatua za mwisho kukamilisha jinsi tutavyolipa, ndiyo maana tumetoa semina kwa wanamuziki, lengo ni kuwahamasisha kujisajili, alisema Sinare.

Afisa Mtendaji Mkuu wa CMEA, Paul Matthysse alisema kuwa mbali ya wanamuziki, kampuni yao itawawezeha pia watayarishaji wa muziki na wasanii wengine pamoja na vyombo vya habari kupata kufahami takwimu sahihi za nymbo zilizochezwa kwa siku, wiki, mwezi na kwa mwaka.

Matthysse alisema kuwa kampuni yao imewekeza mitambo ya kisasa inayowezesha kuchapisha na kuhakiki nyimbo pindi zinapochezwa hewani na televisheni na redio na kutoa ripoti za aina mbalimbali zinazohitajika kutumika kwa malengo maalum.

Pia tunapokea na kuhifadhi nyimbo kwenye mitambo maalum kwa matumizi ya uhakiki, na kudhibiti kiasi cha mirabaha ambacho Cosota kupitia vyombo vya habari inatakiwa kuwalipa wasanii kulingana na idadi kamili ya urushwaji wa kazi zao, alisema Matthysse.

Alisema kuwa wanamuziki na wasanii wengine ambao hawatakuwa na usajili, watakosa haki zao pamoja na CMEA kuendelea kurekodi kazi zao zinazochezwa katika redio na televisheni mbali mbali. Ni muhimu kwao kujisajili, kutojisajili ni kupoteza haki zao zinazotokana na kazi yako, alisisitiza.

Chanzo: Michuzi
 
Attachments

  • 5.JPG
    5.JPG
    29.1 KB · Views: 1,204
  • 6.JPG
    6.JPG
    36.4 KB · Views: 1,171
Baada ya muda mfupi hakutakuwa na free2air tv/radio!!. Na wasanii ili kupata promo itabidi nao walipie!!! Lets wait!!
 
Kazi ipo, nimekuwa nikiwasikia wasanii hasa chipukizi wakilalamika kwamba nyimbo zao hazichezwi kwenye media hadi watoe rushwa sasa ndio maana hawafanikiwi hali itakuwa je, kuna vipindi vya wasikilizaji/watazamaji kuomba wimbo fulani uchezwe hii nayo itabidi wajipange upya kwa kuweka bajeti ila Ni vizuri wasanii watapata haki zao wapewe tu hakuna namna
 
Baada ya muda mfupi hakutakuwa na free2air tv/radio!!. Na wasanii ili kupata promo itabidi nao walipie!!! Lets wait!!

Wasanii wanafurahi sasa hivi ila hili jambo likiingia katika utekelezaji wao ndio watakaoumia zaidi.
 
Salaaama!?

jamani.. huu mpango wa kuwalipa wasanii radioni unaua mziki wetu naongea kwa uchungu.. coz juhudi zote zilizofanywa na wasanii zinakwenda kufa.

Kwanza kwa sasa industry yetu inatawaliwa na mziki wa nigeria south africa marekani na kwingineko sasa kama WAANDISHI WA HABARI WA KUJITOLEA BADO WENGI Tanzania unamlipaje msanii na kumuacha muandishi..
Album:
Kwakua bado industry yetu ndio kwanza inakua ilibidi soko la album lirudishwe kwenye mstari ili nyimbo za wasanii zisipotee bure kama vile nyimbo za hisia na kuelimisha jamii ambazo kwasasa msanii anarecord lakini haziachii hewani,
Sasa hii inataka nyimbo kupigwa bila limit ili kumtangaza msanii na kumfanya brand ndipo alipwe bila kua na shaka.

Sasa hili la kulipwa watafaidika wasanii wasiozidi 10 na wengine wote wataumia sanaa maana wasanii walio kama brand kwa sasa ni wachache..

Je! Huu mchakato ulimuhusisha nani hadi kukamilika ulihusisha watu wa media zote au kakikundi tu ka watu.. very bad

Je! Itakuaje kwa wasanii wachanga..?
Je! Media zote zikiamua kukomaa Nigeria na us nani wakulaumiwa.
NAPINGA WASANII KULIPWA COZ HATUJAFIKA HUKO BADO. . Serikali itusaidie tuuze album na tulipwe vizuri kwenye show na si huu utaratibu utakao tuzuia kujibrand.. sorry wadau
Nawasilisha.
 
Nakuunga mkono!!!
Je wamiliki wa vyombo vya habari wameshirikishwa vyema!!?
 
Wasanii wanafurahi sasa hivi ila hili jambo likiingia katika utekelezaji wao ndio watakaoumia zaidi.

porojo tu hzo,media nyingi msingi wa vipindi vyao ni bongo fleva,na bongo fleva ni sehemu ya maisha ya wa tz,acha kupiga bongo fleva uone nani atakupa atakupa sikio na jicho lake
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom