CoronaVirus: Vipimo vya mara ya pili ya RC Mghwira vyaonesha hana maambukizi ya COVID19

Jay One

JF-Expert Member
Nov 12, 2010
16,851
16,748
Habari watanzania wote, upendo na amani vitawale.

Usiku saa 2, taarifa ya habari ya Azam TV, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro kasema yeye alikuwa na maambukizi ya Corona baada ya kupima, na alianza kutumia majani ya mmea ambao ni ule wa Madagascar wanautumia, alikuwa anatafuna na akataja jina lake kwa kichanga unavyoitwa, na akasema ni mchungu, na hiyo mimea iko mingi Moshi, na akapima mara nyingine amekutwa negative, yaani hana maambukizi, nimepata matumaini sana sana kusikia hilo. Yaani furaha imenijaa.

Ningeomba serikali yangu sikivu, ifuatilie kwa ukaribu sana mmea huo tena kwa speed kubwa sana, Mungu tusaidie. Mama Anna atusaidie tuujue vema huo mmea.

Mungu mbariki Mh. Rais wetu, John Pombe Magufuli, Mungu ibariki Tanzania.

2400690_IMG-20200508-WA0001.jpeg
 
Back
Top Bottom