CoronaVirus: Unawezaje kujiandaa na kukaa Karantini au zuio la kutotoka ndani?

Status
Not open for further replies.

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
625
938
Watu wanashauriwa kukaa Karantini kwa siku zusizopungua 14 huku muda wa zuio la watu kutotoka ndani likitegemeana na uamuzi wa Serikali katika nchi husika

Kwa kuzingatia uwezekano kwamba watu wengi zaidi Ulimwenguni watatakiwa kukaa ndani, kuandaa nyumba yako kwa ajili ya tukio hilo ni jambo muhimu

1. Hakikisha una bidhaa zisizoharibika kwa muda mrefu na muhimu kama vinywaji, tambi, mchele, unga, nafaka, na vyakula vilivyokaushwa pamoja na sukari na majani ya chai

2. Unashauriwa kuwa na vifaa muhimu vya huduma ya kwanza na dawa hususan za maumivu. Dawa za dalili za awali za #COVID19 kama kukohoa na kutuliza homa unashauriwa uwe nazo. Ni muhimu kuwa na hifadhi ya dawa ya walau mwezi mmoja

3. Vifaa kwa ajili ya usafi wa mwili na mazingira pia ni muhimu zikiwemo sabuni kwa ajili ya kuogea, kunawa mikono, kufulia na kufanya usafi. Bila kusahau dawa za kuulia vijidudu (Disinfectants)

4. Lakini pia ni muhimu kuandaa vitu vitakavyokuwa vikifanywa na Mwanafamilia kwa kwa wakati huo ikiwa ni orodha ya vitabu vya kusoma, au orodha ya mazoezi au hata michezo ya aina mbalimbali

Aidha, Shirika la Afya Duniani (WHO) lilieleza kuwa ugonjwa huu unaweza kuleta mawazo mengi kwa baadhi ya watu, hivyo ikikutokea jaribu kuacha kusoma, kuangalia na kusikiliza kwa wingi taarifa kuhusu #CoronaVirus
 
Nawaza tu ni watanzania wangapi wanaomudu haya??
Mungu atunusuru na hili janga tu

Sent from my Infinix X559C using Tapatalk
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom