JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 625
- 938
Watu wenye Ulemavu wanasema hali inakuwa ngumu sana kwao kwa sababu wengi walikuwa wakitegemea biashara za Ujasiriamali ambazo kwa sasa ama zimefungwa au hazifanyi vizuri.
Umoja wa Furaha ya Wanawake Wajasiriamali kwa Viziwi Tanzania (FUWAVITA) umesema zinahitajika barakoa zinazoonesha sehemu ya mdomo kwani kama hakuna Mkalimani wa kuzungumza kwa ishara wao husoma midomo ya mzungumzaji.
Baadhi ya Viziwi wametolea mfano wakiwa sokoni ambapo watu wote wamevaa barakoa inakuwa shida kwao kuwasiliana na wauzaji lakini pia shida hii waanaipata kwa Utingo (Makondakta) wa usafiri wa Umma.
Aidha, wameomba msaada wa chakula, barakoa na Sanitizer kwasababu wao kwa sasa ni ngumu kupata mahitaji hayo.