CORONAVIRUS: Naongeza miluzi ya tahadhari lockdown iharakishwe

All in all hadi sasa tz wagonjwa 6...

Tukubali tukatae huu ugonjwa kwa africa its not a big deal sema umekuja kutafuta kick tu za bure.

Ingelikuwa kwel huu ugonjwa unasambaa kwa kasi africa nadhan robo ya watu sasa hivi wangekuwa washapoteza maisha maana si mchezo kabisa unavyoua...
Usichokijua ni kwamba hizi nchi ambazo zina umasikini wa akili takwimu ambazo huwa wanatoa ni geresha tu!
 
Pambana na khali yako,serikali haijaleta corona na wala haipendelei kuona watu wake wakifa au kuugua

Sent using Jamii Forums mobile app
Ila inaweza kuzuwia isienee kwa kasi na kuuwa watu wengi au sivyo?
Nachukua ushauri wako napambana kivyangu kujitahidi kujitenga na hatari, hapa nipo ndani kwangu.
Sina hakika 100% ya usalama wangu sababu bado natoka nje kutafuta huduma muhimu na huko nje kuna wageni toka kwenye nchi zenye huu ugonjwa.
 
Viongozi wetu wa kisiasa wanajali mapato zaidi kukamilisha miradi mikubwa ya miundombinu, afya imewekwa kando.
 
Wewe sababu una kaajira ndo Mana unashadadia lock down,ss ambao hatuli mpaka tutoke hujatufkiria kwenye hio lock down yako,Sasa ukifunga mtaa ni Yale Yale tu kama hatutakufa kwa Corona njaa vp itatuacha, think more jombaa

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu tuanze na maeneo ya starehe, nyumba za ibada, sherehe za harusi n.k.
Tuzuwie watu toka nchi zilizo athirika na janga hasa za Ulaya.

Tufunge mpaka wetu na nchi jirani zenye COVID-19 turuhusu kusafirisha mizigo tu kati ya nchi zetu.
 
Tatizo hatuna maabara tosha za kupima, huko ambako unaona number ipo ubwa wanapima kila mtu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa hiyo usipopima hufi?

Kama wagonjwa tunao wengi ila shida ni ukosefu wa maabara tu maana yake vifo vya kutisha tungeshavishuhudia mitaani zaidi ya Italy na Spain wenye maabara.

Wito wa mtoa mada ni muhimu sana badala ya kusubiri maafa,hata Italy alianza mgonjwa mmoja!!
 
Mkuu upo serious kweli?! Unafahamu kuwa kwenye hizi nchi ambazo ni masikini wa akili huwezi kupata takwimu sahihi?Kama unasubiria kupewa takwimu za vifo kwa kifupi ni kwamba huna akili kabisa!!


Kama hata population yetu haijulikani itakuwa wanaokufa
Watu wanaleta mzaha kweli


Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Kuna mahali nimesoma, korona inaambukiza mara nne zaidi ya mafua, watu wahimizwe kutumia mask hasa kwenye mikusanyiko kama sokoni, ndani ya daladala, kwenye migahawa, na kwenye enclosures mfano vyumba vya ATM au ofisi zinazotumiwa na watu wengi, na pia swala la kunawa mikono lizingatiwe kila mahali.
 
Mimi siamini Kama corona virus inaweza kuingia kanisani,
Shime nawaomba jumapili tukutane mito ya baraka tukemee hili gonjwa corona
 
Back
Top Bottom