Coronavirus: Magereza yazuia Wafungwa na Mahabusu kutembelewa

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Jeshi la Magereza Nchini Tanzania limesitisha huduma zote za kutembelea Wafungwa na Mahabusu kutokana na kutangazwa kwa uwepo wa Virusi vya Corona (COVID-19)

Huduma hizo zikiwemo za Mahabusu kupelekewa chakula zimesitishwa kuanzia jana Machi 18, 2020 hadi hapo itakapotangazwa vinginevyo

Jeshi hilo limebainisha kuwa linaendelea kuchukua tahadhari na hatua kadri litakavyoona inafaa pamoja na kuzingatia miongozi iliyotolewa na Serikali dhidi ya Corona

58EA387B-07D0-44B0-8F6D-1D56CA34E2D8.jpeg
 
Askari magereza nao si wanaishi mitaani uki daah mungu saidia

yess BiShoo haswaaAaa
 
wabongo mmeumbwa na roho mbaya kuliko shetani, safi sana we umeona corona vipi kuhusu mahabusu wenye special diet, unavyowajua wewe magereza watapikia mahabusu kwa bajeti ipi???
Umemsoma vibaya mkuu. Ni safi kwakuwa inapunguza chances za maambukizi kuendelea kusambaa. Hayo mengine sio juu yake kuamua ni juu ya waliofikia hayo maamuzi kwasababu wanajua kuwa hao watu wapo wenye hizo special needs (diet).
 
Vp kuhusu wafungwa wapya na mahabusu wapya wanaotokea uraiani kwenye tetesi za corona, hawa watawafanyia utaratibu upi? Au na vifungo vitakuwa vya nje ili kuhofia/kuwalinda na maambukizi kwa wale walio magerezani nauliza tu..................
 
wabongo mmeumbwa na roho mbaya kuliko shetani, safi sana we umeona corona vipi kuhusu mahabusu wenye special diet, unavyowajua wewe magereza watapikia mahabusu kwa bajeti ipi???
Duuh mkuu umepanik sana af too bad hata sijui roho mbaya ina sura gani.
Sasa kwa akili yako unafkiri magereza watashindwa kuwapa chakula wafungwa wa hvyo ili wafe njaa au? Hadi wamefanya hivyo means wanajua watadeal vipi na wafungwa wenye special case, usalama kwanza.
 
Jeshi la Magereza Nchini Tanzania limesitisha huduma zote za kutembelea Wafungwa na Mahabusu kutokana na kutangazwa kwa uwepo wa Virusi vya Corona (COVID-19)

Huduma hizo zikiwemo za Mahabusu kupelekewa chakula zimesitishwa kuanzia jana Machi 18, 2020 hadi hapo itakapotangazwa vinginevyo

Jeshi hilo limebainisha kuwa linaendelea kuchukua tahadhari na hatua kadri litakavyoona inafaa pamoja na kuzingatia miongozi iliyotolewa na Serikali dhidi ya Corona

View attachment 1392912

Mkuu Influenza nadhani kwa kuanzia mahakama zote katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zingesimamisha shughuli zake kwa muda au kesi ziendeshwe kwa kutumia Video Conference (IT isaidie) ili kupunguza wafungwa kukutana na watu ambao sio wafungwa.

Ni vizuri serikali imesitisha kwa muda wafungwa kutembelewa na jamaa zao LAKINI nashauri iruhusu wafungwa wawasiliane na jamaa zao kwa kutumia video Conference (IT isaidie hilo).

Ahsante
 
Duuh mkuu umepanik sana af too bad hata sijui roho mbaya ina sura gani.
Sasa kwa akili yako unafkiri magereza watashindwa kuwapa chakula wafungwa wa hvyo ili wafe njaa au? Hadi wamefanya hivyo means wanajua watadeal vipi na wafungwa wenye special case, usalama kwanza.

Hii nakupa kutoka field na katika dunia ya ukweli hayo maneno ya wanasiasa yanaumiza watu tena wasio na hatia. Umeshawahi kwenda magereza lakini????? manake nikupeleke skuli kwanza, usalama sawa lakini afya ndio iwe kwanza. Usalama kwanza ndio kauli za kikatili za wanasiasa wa kibongo jifunze hatua walizochukua china ubinadamu na utu ndio ulikuwa mbele.

Wengine wanapelekewa chakula sababu ya mahitaji maalum na tusistuke kiasi cha kwamba hatua tunazochukua dunia isijetushangaa. Magereza waongeze huduma na waongezewe budget tena kwa dharura sasa hatujasikia hizi za kuongeza budget wala huduma sie tumesikia watu wasipeleke misosi huduma zingekuwepo watu wasingepeleka chakula.
 
Inshort hii ishu ya corona imeathiri na itaendelea kuathiri wengi sana, sababu kama nchi tulikua hatujajiandaa na jins ugonjwa unavyosambaa fasta hamna budi kufanya hivyo kulinda taifa, maana kwa wenzetu tunaskia kila siku watu wanavyokufa.

Sio tu mahabusu, kuna watu walikua wafanyakazi wa mashuleni na vyuoni wanategemea wawauzie wanafunzi chakula ndio wajipatie riziki zao, je hao nao wasemeje? Tusilaumu serikali, yenyewe inafanya wajibu wake wa kulinda raia, hayo mengine yatatafutiwa tu ufumbuzi kadri siku zinavyozidi kwenda. Kinga ni bora kuliko tiba.
 
Back
Top Bottom