Corona: Wazee na wenye magonjwa mengine tupaze sauti

Hayo mapambano ya wengi bado hayajapata BARAKA kutoka juu!;, je tukae tu?? au tuendelee kuomba hizo baraka hadi lini??--- hiyo ni sawa na kumpigia gitaa beberu.

Shida Watz ni mazwazwa, hatuna hamasa, hatujitambui na tumejaa ujinga na woga, wewe unadhani kama kila mtu mmoja mmoja tukiamua kuvaa barakoa nk, nani atatuzuia??!---- tatizo ni Watz na sio Serikali.
Acha uongo wewe hata wazungu walisubiri tamko la serikali zao ndo wakapata miongozo serikali ikawa inatoa elimu kwa wananchi wake.. wewe mwenyewe usingejua umuhimu na mbinu bila serikali za kizungu kufanya campain za kuelimisha
 
Mi nakushauri wwe beba wapendwa wako mkaishi huko unakoona Serekali zao zinachukua hatua sahihii kwenye ugonjwa wa Corona,msije mkafa bure alafu mkailaumu Serekali ya Magufuli bure!!
Wewe serikali ikitoa tamko unachoumia nini wewe barakoa ungezijua bila serikali za hao waliofuata hatua stahiki yani unakaa unaumia mwenzio anavotoa wazo ambalo ni zuri kwa kipi au serikali ni ya babako wewe..unataka Mtanzania asilindwe na serikali yake una akili kweli wewe? Unajua kazi ya serikali kwa raia wake boya wewe?
 
Haka kajamaa toka corona inaanza kila uzi ni hilo tu!

Hebu fikiria tangu april mwaka jana kanaongela corona tu.

Sasa anataka sijui wakipaza sauti corona ndio inaondoka?

Tatizo watu kama hawa tukiwaita wapumbavu mods wanakimbilia kitufe cha ban
Sas we inakuuma nini wewe ndo serikali au ukoo wako ndo serikali
 
Mabibi na mabwana hali inaendelea kuwa si hali. Sisi tulio hatarini sauti zetu lazima zisikike. Kwa mwelekeo uliopo ndiyo tumeshatolewa kafara hivyo.

Jana tumemzika kigogo wa BOT (Joachim Sayi Nsunga) RIP, huko Dutwa Bariadi, Simiyu. Huyu bwana alikuwa mhasibu mkuu BOT makao makuu, Dodoma.

Amefariki juzi pale Benjamin Mkapa. Hakuwa mtu mdogo kwani angalau aliweza kutumia ventilator.

Pana mwelekeo kabambe wa kudhibiti taarifa za vifo. Kuzifanya taarifa za vifo vya vigogo kuwa ni nyara za serikali.

Wazee na wenye magonjwa mengine, sisi pia kama walipa kodi ni muhimu sana tukapaza sauti zetu vilivyo. Hatustahili kutelekezewa janga. Tunayo haki ya kuishi kama ilivyo kwa watu wengine.

Sisi tunalipa kodi na wengine wetu tumelipa sana kodi labda kuliko hata hawa ambao leo wanawashwa sana na pilipili wasizo zila kutusemea sisi.

Propaganda za vijiweni kuwa ugonjwa huu hauuwi ila hofu. Ugonjwa huu tiba yake ni mazoezi. Ugonjwa huu tiba yake ni lishe, malimao na tangawizi. Ugonjwa huu tiba yake ni nyungu n.k.

Yote hayo tokea vijiweni hayatusaidii sisi tulio wahanga zaidi.

Wito kwa serikali:

"Sisi tulio wahanga wa kesho wa ugonjwa huu tunaidai haki yetu ya kuishi. Tunawaona wenzetu wanavyopukutika. Kama mnatu 'kana' tukiwa hai, nasi tuta 'wakana' ninyi tukiwa hai."

Tafadhalini sana waachieni wataalamu wa afya kushika hatamu za uongozi wa vita dhidi ya ugonjwa huu. Kwanini ombi hili ni kubwa mno kwenu?

Hadi tufe wangapi?

Kwanini nyie msiokuwa katika hatari ya ugonjwa huu mmekuwa sana wa kutusemea, hali kufa twafa sisi?

Mara ooh mliona mwana michezo kafa kwa Corona? Jibu ni kuwa hatujui. Kwani hazipo takwimu hizo kama ambavyo hatujui pia hata kama kuna machangudoa wamekufa kwa Corona.

Hivyo pia hatuwezi kusema kuwa uchangudoa ni kinga ya Corona.

Hivi ni wapi palipo na wana michezo wazee au wenye magonjwa mengine? Mbona kuchezana shere hivi?

Hebu tusitoane kafara mchana kweupe namna hii.

Ninawasilisha.
Sasa unataka ufanyiwe nini? Au ndo unataka tukubali chanjo wa majaribio? Huoni huko walikochanjwa wanavyopukutika!? Kifupi covid-19 ni ugonjwa ambao mpaka sasa hauna tiba! Hata chanjo zilizopo sasa duniani hazijaonyesha uwezo wake hata tu wa kuzuia maambukizi! Kilichopo ni matangazo ya biashara!
Ushauri: Kama unapenda kuishi kiasi hicho, basi fuata maelekezo hayo uliyoyataja mwenyewe, na pia mkaribie zaidi Mungu kwa sala na dua!
Pia Muamini Mungu, maana kanachoua siyo covid-19 tu, bali yapo ma akina malaria, ajari, kipigwa roba, kufumaniwa, utamu uliozidi kwenye yale mambo yetu ya kiutu uzima hasa mzee ukijichanganya na damu changa😜! Nk, nk!
"Bwana asipo ulinda mji, yeye alindaye akesha bure!"
 
Wewe serikali ikitoa tamko unachoumia nini wewe barakoa ungezijua bila serikali za hao waliofuata hatua stahiki yani unakaa unaumia mwenzio anavotoa wazo ambalo ni zuri kwa kipi au serikali ni ya babako wewe..unataka Mtanzania asilindwe na serikali yake una akili kweli wewe? Unajua kazi ya serikali kwa raia wake boya wewe?
Swala la kujilinda linaanza na wwe mwenyewe,mbona Binaadamu nyie ni wagumu sana kuelewa! Naona hata huko kwa michepuko yako Serekali ndiyo inakulinda!!
 
Acha kujidanganya wewe huu ugonjwa ni ushirikiano wa mtu zaidi ya mmoja kwasababu we unajilinda lakini kama mwenzio hajilindi hamna unachofanya..Na vipi kuhusu kuongezeka kwa elimu ya kujikinga na tiba..Hivi leo hii wazungu walivo magenius still wanatoa elimu kwa watu wao Unataka wewe ambae kazi yako mara nyingi ni kuamka asubuhi kushika jembe kulima kurudi kulala au kulewa usipewe elimu
Naomba nikuulize swali! Are you working for billgate foundation!?
 
Hakuna ujinga hapo watu ukweli unabaki pale pale serikali inatakiwa ifanye kazi..

Serikali inafanya kazi kwa kusema kwamba Tz hakuna CORONA, wewe unataka ifanye kazi gani wakati inadai CORONA hakuna!!!
 
Barako ya kibongo ukivaa wewe mwenzio asipovaa akiwa nao anakuambukiza au hujui hilo?

Sasa tufanyeje mkuu???, wewe unalalamika tu bila kutoa ushauri, Serikali ndo imeshasema Tz hakuna CORONA, sisi tunaona CORONA ipo sasa sisi tunaoiona hiyo Corona walau tufanyeje ???-- tukae tu kusubiri kifo???!!
 
Acha uongo wewe hata wazungu walisubiri tamko la serikali zao ndo wakapata miongozo serikali ikawa inatoa elimu kwa wananchi wake..

Acha upuuzi wewe, unataka muongozo gani kutoka serikalini???--- Muongozo wa serikali ni huu; "TZ hakuna CORONA".

au wewe sio Mtz???
 
Mabibi na mabwana hali inaendelea kuwa si hali. Sisi tulio hatarini sauti zetu lazima zisikike. Kwa mwelekeo uliopo ndiyo tumeshatolewa kafara hivyo.

Jana tumemzika kigogo wa BOT (Joachim Sayi Nsunga) RIP, huko Dutwa Bariadi, Simiyu. Huyu bwana alikuwa mhasibu mkuu BOT makao makuu, Dodoma.

Amefariki juzi pale Benjamin Mkapa. Hakuwa mtu mdogo kwani angalau aliweza kutumia ventilator.

Pana mwelekeo kabambe wa kudhibiti taarifa za vifo. Kuzifanya taarifa za vifo vya vigogo kuwa ni nyara za serikali.

Wazee na wenye magonjwa mengine, sisi pia kama walipa kodi ni muhimu sana tukapaza sauti zetu vilivyo. Hatustahili kutelekezewa janga. Tunayo haki ya kuishi kama ilivyo kwa watu wengine.

Sisi tunalipa kodi na wengine wetu tumelipa sana kodi labda kuliko hata hawa ambao leo wanawashwa sana na pilipili wasizo zila kutusemea sisi.

Propaganda za vijiweni kuwa ugonjwa huu hauuwi ila hofu. Ugonjwa huu tiba yake ni mazoezi. Ugonjwa huu tiba yake ni lishe, malimao na tangawizi. Ugonjwa huu tiba yake ni nyungu n.k.

Yote hayo tokea vijiweni hayatusaidii sisi tulio wahanga zaidi.

Wito kwa serikali:

"Sisi tulio wahanga wa kesho wa ugonjwa huu tunaidai haki yetu ya kuishi. Tunawaona wenzetu wanavyopukutika. Kama mnatu 'kana' tukiwa hai, nasi tuta 'wakana' ninyi tukiwa hai."

Tafadhalini sana waachieni wataalamu wa afya kushika hatamu za uongozi wa vita dhidi ya ugonjwa huu. Kwanini ombi hili ni kubwa mno kwenu?

Hadi tufe wangapi?

Kwanini nyie msiokuwa katika hatari ya ugonjwa huu mmekuwa sana wa kutusemea, hali kufa twafa sisi?

Mara ooh mliona wapi mwana michezo kafa kwa Corona? Jibu ni kuwa hatujui. Kwani hazipo takwimu hizo kama ambavyo hatujui pia kama kuna machangudoa wowote wamekufa kwa Corona.

Hivyo pia hatuwezi kusema kuwa uchangudoa ni kinga ya Corona.

Hivi ni wapi palipo na wana michezo wazee au wenye magonjwa mengine? Mbona kuchezana shere hivi?

Hebu tusitoane kafara mchana kweupe namna hii.

Ninawasilisha.
Mkuu as long as siku yako imefika utakufa tu.
 
Mkuu as long as siku yako imefika utakufa tu.

Kwanini hupendekezi kufunga hospitali zote tu. Kwa sababu siku yako ikifika si utakuwa tu?

Au haya ya siku ni kwa Corona tu?

Really?
 
Heko mama Samia kwa kukitambua na kukifanyia kazi kilio cha wahanga hawa.

Inapenda kuwa tume ya Corona i njiani kukuletea ripoti kamili ya kuwa tunatoka vipi.

Hakika wewe ni chaguo la Mungu maisha ya watu ni kipaumbele chako. Ushirikina shirikina tupa kule.
 
Back
Top Bottom