#COVID19 Corona: Vituo vya Chanjo vinapatikana wapi?

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,226
35,151
Ni jambo la kheri kuwa sasa hatma ya maisha yetu iko wazi zaidi ndani ya gonjwa hili hatari.

Tufahamishane vilipo vituo vya Chanjo hii pendwa kutoka kwake beberu mwingi wa huruma kuliko wenzetu wazaliwa nasi.

Mkoa kwa mkoa, wilaya kwa wilaya, tarafa kwa tarafa, kata kwa kata au hata kijiji kwa kijiji itapendeza zaidi.

Mwamko wa ndugu na jamaa kuipata chanjo hii ni mkubwa sana. Itasaidia mno kuwepo kwa maelekezo ya wazi ya wapi pa kuipata kwa urahisi na kadri inavyowekana.

Chonde chonde ka kanzidata uchwara ka vilipo vituo vya chanjo nchi nzima itapendeza sana. Alimradi mtu yuko safarini, nyumbani, matembezini, nk kazi iendelee.

Maelekezo kamili ya wapi na kuanzia lini huduma hii inapatikana ni muhimu. Watu wasiende mahospilalini kuulizia.

Vinginevyo kuna ya hatari ya watu kwenda mahospitalini kufuata Corona badala ya chanjo.

Tuna mengi ya kufanya, lakini hili kwanza. Bila maisha kwanza, mengine yote ni ubatili mtupu.

Ninawasilisha.
 
Jaribu kuingia kwenye website ya wizara ya afya search unaweza kukuta la ziada maana bado hawajafafanua vizuri bado.
 
Jaribu kuingia kwenye website ya wizara ya afya search unaweza kukuta la ziada maana bado hawajafafanua vizuri bado.

Nimeperuzi na kurambaza vilivyo katika website ya wizara ya afya:


Sina hakika kama ni mpangilio mbovu wa taarifa au ni yale yale mapuuza yetu yaliyotufikisha kwenye nyungu na mikaratusi.

Hakuna maelekezo ya wapi na kuanzia lini huduma hii inapatikana. Ingependeza twende mahospitalini kuchanjwa na si kuulizia kuhusu kuchanjwa tusijejikuta tunafuata corona badala ya chanjo.
 
Naomba kujua mahala/vituo inapotolewa chanjo ya CORONA hapa Dar Es Salaam, na taratibu zake.
 
Naomba kujua mahala/vituo inapotolewa chanjo ya CORONA hapa Dar Es Salaam, na taratibu zake.

Nina tatizo kama lako nikipokea dodoso kama hizo tokea mikoani pia:

 
Wizara ya Afya iratibu hili zoezi la chanjo vizuri ili watanzania wengi waweze kupata chanjo kwa urahisi.

tupo tayarai mara baada ya kumuona Rais wetu mpendwa akichanjwa nasi tumeamini kuwa hii chanjo ni salama kwetu.
 
Soon is not good enough
Usambazaji wa chanjo kwenye vituo si jambo rahisi mkuu, challenge kubwa ni utunzaji wake (below zero temperature), hata nchi zilizoendelea hii kitu inawasumbua sana, Hope our government wamejipanga kwa hilo, 1 million vaccines is no joke
 
Usambazaji wa chanjo kwenye vituo si jambo rahisi mkuu, challenge kubwa ni utunzaji wake (below zero temperature), hata nchi zilizoendelea hii kitu inawasumbua sana, Hope our government wamejipanga kwa hilo, 1 million vaccines is no joke

Tangu chanjo kuwasili tokea kwa beberu leo siku ya 3 inakwenda. Kwamba hizo logistical issues hazikuwa tayari tangia chanjo zilipoanza kutumika duniani?

Kweli mtu pori alikuwa mzigo haswa.

Hata beberu aliyetupa chanjo hizo bure, bila shaka anatushangaa. Kwa mwendelezo huu, kwa hakika bado nyuzi mbili hizi ni muafaka sana:

1. Majaliwa, Jaffo na Vigogo Afya Waachie Ngazi

2. Mawaziri waachie Ngazi kutoa Nafasi kwa Mwanzo Mpya

Chanjo zimeanza kutumika duniani tangia mwaka jana. Hadi tumepewa chanjo bure bado tuna logistical issues. Hata siku ya tatu leo tangu kupewa chanjo:

(a) haijulikani lini chanjo zitaanza kutolea
(b) haijulikani nani watakuwa eligible kupata chanjo
(c) haijulikani chanjo zitatolewa wapi

Bado watu wako ofisini na gonjwa linaendelea kama vile hatuna akili nzuri.

Kwa hali hii, si ajabu kuwa nyungu, maombi, mikaratusi, michai chai, malimao yalikuwa tiba rasmi yenye uratibu kamili wa serikali.
 
Nasaha za MAGUFULI bado zipo vichwani mwa watanzania aliwafumbua vichwa kwelikweli

Kwamba aliwafumbua au aliwafumba vichwa wajinga na wenye njaa zao kweli kweli.

IMG_20210711_205649_038.jpg


Nakazia:

"Aliwafumba vichwa machinga, wapiga debe, vibaka, sungu sungu, mama lishe, baba lishe, boda boda, na wa namna hiyo."

Kwa hakika aliwafumba "vichwa panzi na wenye njaa zao" vichwa kweri kweri!

Watu wangapi wamepoteza maisha yao katika zama zake hizo za porojo ambao wangekuwa hai leo?


Pumzikeni kwa amani ndugu zetu ila washirika waliopo wak ee hatutawaacha kana kwamba hakuna lililotokea.

Habari ndiyo hiyo.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom