Corona: Vita ya kiuchumi Tanzania dhidi ya nani?

Wewe nawe tumekuchoka na vi thread vyako, yani tangu mwaka jana wewe ni corona tu.

Acha ujinga na upumbavu kijana chapa kazi corona hiyo itaondoka na kukuacha maskini maana unaiogopa sana.

Halipo jambo la kheri na faraja kama kuchokwa wewe na wenzio ambao kimsingi mu hawa hapa:

IMG_20210218_174254_207.jpg


Ni wazi kuwa huyo anayeitwa adui yetu wapuuzi hawa nao bila shaka hawamjui. Ila wako vizuri.

Si mmtaje huyo adui yetu mamburula nyie kama mnamjua?

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
yup hadi wanaweka virusi kwenye barakoa huoni ni wivu huo?

Ilipendeza kuwajua kamili ni kina nani.

Ni vyema wanaotuaminisha kuwa tuna maadui kwenye hili hajajua kuwa wengine sisi, wengi tu hatuwajui.

Tunapigana vipi vita na adui ambaye wananchi wengine hawamjui?
 
Characteristics of a mad person:

1. Confused thinking
2. Denial of obvious problems
3. Delusions or hallucinations (seeing or hearing or believing things that are not really there)

Jiwe has all these characteristics

Siku moja kuwa na masaa 48 haikuwa ulimi kukosa mfupa.

Barakoa 12/person @ 4hrs signified further to that effect.
 
Mabibi na mabwana, kumekuwa na habari hii kuwa ugonjwa huu ni vita vya kiuchumi. Tena mlengwa ni Tanzania...
wenzetu wanapigana vita ya uchumi kwa kuongeza technolojia,kufanya protectiosm inapobidi,kusomesha watu wao hasa kwenye nchi zilizowazidi ili kuiba maarifa, kuwekeza mitaji kwenye makampuni yao,kutafuta resource nje ya nchi zao. Sisi tunapigana vita ya kiuchumi kwa kulalamika tu.
 
Mfugale flyover na zile ndege zilizonunuliwa cash zimetikisa dunia nzima haswa mabeberu na zahanati 361, viwanda 8000,ajira milioni 6, elimu bure, kushuka kwa mfumuko wa bei,stendi za kisasa, mabeberu yanahaha sana
Bila kusahau kupandishwa daraja la kusahau 7% ongezeko GDP kwa mwaka.
 
Wewe nawe tumekuchoka na vi thread vyako, yani tangu mwaka jana wewe ni corona tu.

Acha ujinga na upumbavu kijana chapa kazi corona hiyo itaondoka na kukuacha maskini maana unaiogopa sana.
Mbona hujajibu swali lake? Kama umechoka kwanini unasoma threads zake na ili hali huwezi kujibu hoja zake? Act like a grown up person.
 
Ungelikuwa unajua uchumi wewe, usingekuja na mada inayokuchora namna hii. Hii nikwa kuwa una upeo mdogo sana unaoishia kwenye kulima korosho na kusafirisha makinikia. Ninashauri Dr. Magufuli anzishe elimu ya ngumbaru kwa kujenga uelewa kwa wanaojua kusoma na kuandika.
Mkuu au na wew humjui adui mnayepambana naye? Acha maneno sema ni vita dhidi ya nani?
 
Ukikua utajua kwanini hii inaiwa ni vita ya kiuchumi, kwa sasa endelea kunywa uji.

Nyinyi mliokwisha kua ndiyo hawa hapa?

IMG_20210218_174254_207.jpg


Kwa sasa mmesha acha kunywa uji?

Ngumu sana kumtaja adui? Mbona vita vya Uganda adui alikuwa wazi: nduli Iddi Amini.

Vita vya Congo adui alikuwa wazi: M23.

Vita hivi adui ni nani ili sote tupambane naye kwa niaba ya mama Tanzania?

Badala ya kujibu swali waja na ngonjera kuwa wewe uko vizuri?

Ujinga unajulikana kuwa ni mzigo nao hubebwa kichwani tu kama wa kuni.
 
Hapo hujamsaidia mleta mada. Anatakujua huyo adui tunaepigana nae ni nani? Akimtambua itakua rahisi kwake nae kushiriki. Si unaona hata simba na yanga wanavaa jezi tofauti? Bila kumtambua adui tunaweza kugongana wenyewe mkuu. Huyo adui ni yupi?
Akukujibi ni tag mkuu, nina uhakika 100% hata yeye hamjui adui.
 
Back
Top Bottom