Corona: Vita ya kiuchumi Tanzania dhidi ya nani?

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
7,759
2,000
Mabibi na mabwana, kumekuwa na habari hii kuwa ugonjwa huu ni vita vya kiuchumi. Tena mlengwa ni Tanzania.

Habari hizi zimeendelea kuwapo ikisisitizwa kuwa vita vya uchumi ni ngumu zaidi kuliko vita nyingine zikiwamo tuli zowahi kupigana. Yaani vikiwamo tulivyowahi kushinda kama vya nduli Amini, au hata vya kuwasambaratisha M23.

Kwa bahati mbaya, matamshi haya ambayo wakuu wetu wamekuwa wakiyatoa mara kwa mara, yamekuwa hayana ufafanuzi wa kutosha kiasi kumekuwa na mkanganyiko, zaidi ya kuelewa.

Siri ya ushindi katika vita tulivyopigana tukashinda, ilikuwa ni uwazi wa viongozi wetu ambako ndiko kulikopelekea umoja wetu.

Mfano, sababu za wazi kabisa za kumpiga Amini zilikuwapo. Hivyo nia ikawepo, ikizingatiwa kuwa hata uwezo pia tulikuwa nao.

Katika vita hivi vya uchumi tunavyoaminishana kuwa vipo dhidi yetu, hivi adui yetu hasa ni nani? Tuna uhakika gani na hao tunaodhani kuwa kweli ni adui zetu?

Vipi nia, sababu na hata uwezo wa kuvipigana vita hivyo kama vipo?

Labda tungeanzia hapo kwenye kuwatambua adui zetu kwanza, ili tujengane kiuelewa kama watanzania wote kwanza, kabla ya kujishika kibwe kibwe kumpambania mama Tanzania tukiwa tumegawanyika?

Ninawasilisha.
 

Criterion

JF-Expert Member
Jan 8, 2008
10,771
2,000
Ungelikuwa unajua uchumi wewe, usingekuja na mada inayokuchora namna hii. Hii nikwa kuwa una upeo mdogo sana unaoishia kwenye kulima korosho na kusafirisha makinikia. Ninashauri Dr. Magufuli anzishe elimu ya ngumbaru kwa kujenga uelewa kwa wanaojua kusoma na kuandika.
 

Mr faru john

Senior Member
Dec 22, 2016
170
500
Adui mkubwa ni Mimi na wewe

Kwanini mtanzania awe adui?

Wengi wao hawana Imani na mwelekeo wa nchi kama nchi.

Ugumu wa maisha kwa mwananchi mmoja mmoja katika kupata nahitaji ya kila siku(uadui)

Wafanyabiashara wakubwa kwa wadogo kwa hofu na vitisho wanavyo pata kila wakati wakitekeleza majukumu yao(uadui)

Wafanyakazi serikalini ambao hawajapandishwa mishahara na madaraja yao kwa kipindi kirefu(uadui)

Ajira kwa vijana kundi hili ni kubwa na hatarishi kwani wako na wanaamini hawana cha kuppteza(uadui)

Kwahio kabla ya kuwa tuhumu watu wa nje tujitathmini sisi kwa sisi kwanza
NB:
Hakuna kitu kibaya kama mwizi anaingia ndani kwako anakuibia alafu anaondoka na thamani zako wakat huo huo jirani yako kabahatika kumuona ama kumsaidia mwizi huyo lakini kaamua kua kimya bila kukusaidi wala kukuelekeza ufanikiwe kupata Mali zako.
 

Nziiri

JF-Expert Member
Jul 23, 2020
338
500
Wewe nawe tumekuchoka na vi thread vyako, yani tangu mwaka jana wewe ni corona tu.

Acha ujinga na upumbavu kijana chapa kazi corona hiyo itaondoka na kukuacha maskini maana unaiogopa sana.
Hapo hujamsaidia mleta mada. Anatakujua huyo adui tunaepigana nae ni nani? Akimtambua itakua rahisi kwake nae kushiriki. Si unaona hata simba na yanga wanavaa jezi tofauti? Bila kumtambua adui tunaweza kugongana wenyewe mkuu. Huyo adui ni yupi?
 

Bambushka

JF-Expert Member
Jan 9, 2020
2,107
2,000
Huko duniani kote, wana CORONA, vita hii ya uchumi, iweje specifically kwa nchi isiyo na lolote zaidi ya blah blah za politicians.

Mchina mwanzoni, kiliitwa kirusi cha mchina hadharani na wapinzani wake kiuchumi, lakini hakutumia nguvu kwenye majukwaa na propaganda, akajidhatiti kudhibiti, na mpaka chanjo kishatoa.

Hizi nchi Trump alizipa nick-name for a reason.

Everyday is Saturday............................... :cool:
 

Heci

JF-Expert Member
Aug 14, 2016
2,317
2,000
IMG_20210211_163253.jpg
 

FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
22,397
2,000
Ni vita dhidi ya Marekani, Uingeleza, Ufaransa na marafiki zao dhidi yetu.

Wenzetu wanatumia Tshs Trillion 6 na ushee kwa mwaka kufanya uchunguzi wa sayari ya Mars uwezekano wa kuwepo uhai kule ambapo na sisi nasi tunatumia Tshs mil 120 kwa mwaka kununua madawati shule za msingi.

Hawa wawili wana vita vya kiuchumi.
 

Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
102,256
2,000
Wewe nawe tumekuchoka na vi thread vyako, yani tangu mwaka jana wewe ni corona tu.

Acha ujinga na upumbavu kijana chapa kazi corona hiyo itaondoka na kukuacha maskini maana unaiogopa sana.
Utaiheshimu siku imekugalagaza
 

Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
102,256
2,000
Mfugale flyover na zile ndege zilizonunuliwa cash zimetikisa dunia nzima haswa mabeberu na zahanati 361, viwanda 8000,ajira milioni 6, elimu bure, kushuka kwa mfumuko wa bei,stendi za kisasa, mabeberu yanahaha sana
Duuuuuuu ina mabeberu wamepagawa?
 

Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
102,256
2,000
Ungelikuwa unajua uchumi wewe, usingekuja na mada inayokuchora namna hii. Hii nikwa kuwa una upeo mdogo sana unaoishia kwenye kulima korosho na kusafirisha makinikia. Ninashauri Dr. Magufuli anzishe elimu ya ngumbaru kwa kujenga uelewa kwa wanaojua kusoma na kuandika.
Wewe mwenyewe ni ngumbaru tu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom