Corona Virus: Watanzania hawata wasamehe ugonjwa huu ukifika nchini

guzman_

JF-Expert Member
Jan 27, 2016
1,255
2,073
Katika harakati zangu nimezunguka viwanja vya ndege vitatu vinavyopokea sana wageni toka nje, hali niliyoikuta Mungu atusaidie.

In short, kinachosemwa na viongozi na yanayotendeka huko ni mbingu na ardhi. Nimeshuhudia raia zaidi ya 200 kutoka Uchina wakipita airport bila kupimwa wala kukaguliwa kama tunavyoaminishwa.

Kitu pekee wanachoangalia kama amevaa mask basi. Ujumbe wangu kwa wahusika Tanzania haitawasamehe kwa huu ujinga mnaofanya.

Bado nafanya uchunguzi kama kweli tuna vifaa vya kutosha kupima huu ugonjwa mipakani. Ila nasema siku ugonjwa huu ukifika Tz ndipo tutajua tuna watu wenye dhamana hovyo kiasi gani na itakuwa muda umeisha. Ni suala la muda tu.
 
Tanzania kama Ethiopia..yaani wanathamini pesa kuliko watu wake..huu ugonjwa unaweza kutuvamia Mungu apishe mbali sana.

jana nimeangalia mjadala ITV juu ya Corona kuna daktari mmoja alikuwa anaongea kama mwanasiasa tu niliogopa sana kuona hata madaktari ambao ndiyo tunawaita wasomi.

Lakini anaongea kama mwanasiasa kwenye mambo ya msingi niliumia sana, baada ya kuogea uhalisia wa tatizo yeye anaongea yaleyale ya boss wake Ummy Mwalimu kuwa tumejiandaa vya kutosha.

Nchi kama Marekani ambayo tuliiamini mwanzoni kuwa ndiyo mwamba na suluhu ya mambo magumu kama haya leo inalia leo daktari wa TZ anajiamini kuliko waliotutangulia. Nahisi ipo siku ugonjwa huu utatuvamia Mungu apishe mbali sana na kitakacho tuua ni tamaa za viongozi wa kisiasa tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Black Mirror, Inasikitisha sana mkuu yani swala la Professionalism linachukuliwa simple tu Siasa kila sehemu imevamia kuficha matatizo huwezi kutofautisha mtaalamu n mwanasiasa wote ni Bla bla tu.
 
Inshort corona ipo nchini nikwamba inachelewa kuonyesha dalili kwenye mwili wa binadamu after 1 to 2 weeks ndo tutaelewana iran nao ilikuwa hivi hadi waziri alikula vyake

Sent using Jamii Forums mobile app

Sasa umejuaje kama ipo wakati inachelewa kuonyesha hivyo viashiria...?

Kuna case yeyote iliyorepotiwa kuonyesha huo uwepo wake hapo Tanzania?




Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Cha maana sisi tuombe tu wenye akili wapate dawa au chanjo mapema kabla ugonjwa huo haujasambaa hapa kwetu maana vinginevyo tutatafutana humu nchini. Hatuna uwezo wala ujanja wa kupambana na tatizo kama hilo.
 
Black Mirror,

ukija wanafikiria misaada kutoka WHO na nchi kubwa hapo ndipo wapate kushibisha matumbo yao


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Back
Top Bottom