Corona: Ugonjwa unaoua, uliogeuzwa fursa ya kisiasa Tanzania

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,823
35,829
Mabibi na mabwana tumwogope mola aliyetuumba sisi na wote wanaoitwa binadamu. Misahafu ya kikristo inatambua:

"Kumpenda jirani yako kama nafsi yako."

kuwa ndiyo amri iliyo kuu.

Hivi tutajibu nini Akhera sisi kwa udhalimu tunaowatendea wengine?

Leo tumefikia mahali pa kutumia nguvu kuhalalisha vifo vya wengine hata kama vinatokana na ugonjwa huu. Kutumia ulaghai kuhakikisha kujivua uwajibikaji wowote kwa wahanga hata kama majukumu yetu ya kwanza kabisa yalikuwa ni kuwahami wengine na dharura kama hizi.

Leo hii pana makada wa vyama fulani wanataka kutuaminisha kuwa eti wao ndiyo walio waumini wazuri zaidi kuliko hata viongozi wa madhehebu waliko wao kiimani.

Itamwingia vipi akilini mtu awaye yote ya kuwa yupo mtu angependa kutuaminisha ya kuwa yeye ni mkatoloki zaidi ya mapadre, maparoko, maaskofu na kuliko hata Papa huko Roman kwenyewe?

Jamani tuna mafikira ya kuwa watanzania watakuwa ni majuha kiasi hicho kweli?

Leo hii kuna makada wanataka kujifanya ni wa maana mno kuliko hata kina Bill Gates. Wakijishasha na vi propaganda uchwara visivyo na mashiko kuwa wao ni bora zaidi. Kwa lipi hilo jema ambalo majuha hawa waliloifanyia jamii ipi?

Ni vizuri makada uchwara hawa wakajua kina Bill Gates wameifanyia mema sana dunia hii na katu hata 0.1% yake wao hawataweza.

Jitihada za kina Gates kuisukuma mbele dunia hii kiteknologia yahitaji zezeta kutokuzifahamu.

Jitihada za kina Gates kupigana na maradhi ambayo hata kwao yalikuwa wala si issue; duniani kote, hazina kipimo.

Hivi makada hawa ambao hata kodi tu hapa nyumbani wengi wao hawalipi au zilizostahiki hawalipi, wanadhani nani aliyeelimika hata kidogo tu anaweza kuununua ulaghai uchwara wao huu?

Label za Chanjo za corona zilizoelekezwa Africa kwa kutambua ufadhili uliomo ili kutuwezesha na kina sisi kutufikia, eti imekuwa nayo ni agenda yao nyingine ya upotoshaji.

Hivi mbona umeme wa REA ni mahsusi vijijini kwa gharama za kuunganishwa na hata tarrifs?

Makada hawa wanataka leo kutuamimisha kuwa Hakuna usawa kwenye chanjo hii. Vinginevyo eti basi sisi tupewe zenye label ya Ulaya na Marekani na zile zenye ya Africa iende huko! 😂😂😂😂!

Ikumbukwe makada hawa na kina sisi tukiwamo wala hatuna mchango wowote katika utengezwaji na hata upatikanaji wa chanjo hiyo. Si kwa utaalamu wala kwa mchango wowote. Yaani ni mitoto mikaidi tu.

Yaani ni sawa na wale wajuaji wa vijijini kuukataa umeme wa REA kigharama na ki-tariff. Watake ule wa mjini na huu wa REA uende huko mijini. Ebooo! Hii ni akili au ni yale mananihii?

Haya si ndiyo maajabu ya Mussa mwenyewe basi?

Leo mataga wanadai mh. Rais kaeleweka, kuwa corona ipo ila tuchukue tahadhari. Jambo la kheri kabisa. Tuvae barakoa, tunawe na maji tiririka tuepuke misongamano. Wazee wabakie ndani:

Kwamba ghafla Magufuli si m-bia wa afya zetu! Tumwogopeni mola enyi kina mzee mwanakijiji. Kuweni japo hata na aibu kidogo hata kama utu nao hamna.

Wana thubutu kusema ukitemgemea Magufuli kuhusu huu ugonjwa, wafa na itakuwa imekula kwako na wapendwa wako.

Cha kujiuliza huyu Magufuli hana wajibu wowote kwenye hili?

Hao wanaoepuka misongamano, uchumi wao unakuwa je ukizingatia kodi zinaongezwa viwango na hata kwa wigo kila uchao?

Vipi kuhusu miradi ya serikali? Hiyo iko pale pale? Inaendelea tu?

Hivi, kweli tunauguliwa katika familia. Utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwamo kama ujenzi wa nyumba mpya unaendelea tu? Aaaah Wapi!

Au hata je, serikali inaitambua dharura hii na athari zake kwetu?

Haya yakiendelea, pia wakijifanya kuwa ni wasemaji wakuu wa kuihusu hii chanjo, hali wao labda kwa kujua au kutojua si sehemu ya wanaoihitaji chanjo hii kwa sasa:

Ninawasilisha.
 
Mkuu wakati una andika ulikuwa umekunywa kimpumu? nimejaribu kusoma lakini nashindwa kuelewa ulichoandika,umenikumbusha miaka ya nyuma nikisoma sekondari ,wengine walikuwa wanaandika insha ndefu na wanapata maksi 10 kwa mia na wengine wanaandika kidogo wanapata maksi kuanzia 90%.
 
ASHAKUM SI MATUSI.

Umeandika kwa hisia sana ila bado umeandika ujinga, na unatumia hisia zako ili ueleweke katika upuuzi wako.

NB: mimi naamini hao mabeberu wangekua wana nia ya kutusaidia wangeleta hiyo chanjo bure, maana here we are talking about the survival of the human race!, hiyo chanjo nyi mnaisikia tu lakini ni very expensive! refere SOUTH AFRICA,.

Pia kisa tulipokea chanjo zingine haimaanishi ndo tupokee zote, nadhani katika huu ugonjwa(corona) umekaa kisiasa na maslahi sana ndo maana hata raisi amechukua maamuzi magumu katika matamko aliyoyatoa(sio kazi rahisi kua raisi) .

MUAMAR GADDAFI AMEWAHI KUYATABIRI HAYA YOTE, kipindi cha uhai wake! kua yatakuja magonjwa ya virusi na tutauziwa chanjo zaidi na zaidi!

USISAHAU KUNAWA MIKONO KWA MAJI TIRIRIKA, KUVAA BARAKOA NA KUJITAKASA MIKONO YAKO KWA SANITAIZA, pia fanya mazoezi na kula matunda kuboresha kinga ya mwili, Huku ukiendelea kuchapa kazi kukuza kipato chako kwa ajili ya wanao na taifa kiujumla!

kumbuka:- Afya yako ni jukumu lako namba moja, usiibebeshe serikali kwa asilimia kubwa!.
 
MUAMAR GADDAFI AMEWAHI KUYATABIRI HAYA YOTE, kipindi cha uhai wake!..

USISAHAU KUNAWA MIKONO KWA MAJI TIRIRIKA, KUVAA BARAKOA NA KUJITAKASA MIKONO YAKO KWA SANITAIZA, pia fanya mazoezi na kula matunda kuboresha kinga ya mwili, Huku ukiendelea kuchapa kazi kukuza kipato chako kwa ajili ya wanao na taifa kiujumla!

kumbuka:- Afya yako ni jukumu lako, usiibebeshe serikali!.
Afya yangu serikali haiusiki ila kodi inayotokana na kipato changu inahusika sivyo?. Akili za mataga hizi.
 
Afya yako ni jukumu lako namba moja, hizo kodi ni za kutumika katika usalama wako na kurahisisha maisha kiujumla, aghalabu miundombinu, huduma nafuu za kimaisha kama umeme, afya(hospitali) n.k japo bado hawajafanikiwa kwa asilimia mia ila nina imani mambo yatakuja kua mazuri huko mbeleni haijalishi ni nani atakaekua madarakani!

Huwezi kuacha kulinda afya yako kisa ukijua kua serikali itakuja kukulindia na kukutibu!.
 
Mkuu wakati una andika ulikuwa umekunywa kimpumu? nimejaribu kusoma lakini nashindwa kuelewa ulichoandika,umenikumbusha miaka ya nyuma nikisoma sekondari ,wengine walikuwa wanaandika insha ndefu na wanapata maksi 10 kwa mia na wengine wanaandika kidogo wanapata maksi kuanzia 90%.
Ngumu kumeza eeh? Kimpumu ulichokunywa wewe usidhani kila mtu anywa.

Eti mlikuwa mnapata 90% wengine 10% kwa utopolo kama huu ulioandika hapa usiokuwa na mbele wala nyuma? Hivi jiwe analipa hata kodi? Au ndiyo hawa hapa?

Hahaaa. Mataga umekwisha taga?

Hatudanganyiki!

Mnavunga kufa hamkuelewa? Kuwa ndefu?

Ni kwa sababu mmesema utopolo mwingi. Mkadhani tutawaacha. Mna merit juu ya Bill Gates? Magufuli hana cha kufanya na afya zetu Ila kutukamua kodi kweri kweri? Chanjo hii mnalengwa kuambukizwa?

Mamburula nyie. Mna nini?

Hatutawaacha tutauweka wote hadharani!
 
ASHAKUM SI MATUSI.

Umeandika kwa hisia sana ila bado umeandika ujinga, na unatumia hisia zako ili ueleweke katika upuuzi wako.

NB: mimi naamini hao mabeberu wangekua wana nia ya kutusaidia wangeleta hiyo chanjo bure, maana here we are talking about the survival of the human race!, hiyo chanjo nyi mnaisikia tu lakini ni very expensive! refere SOUTH AFRICA,.

Pia kisa tulipokea chanjo zingine haimaanishi ndo tupokee zote, nadhani katika huu ugonjwa(corona) umekaa kisiasa na maslahi sana ndo maana hata raisi amechukua maamuzi magumu katika matamko aliyoyatoa(sio kazi rahisi kua raisi) .

MUAMAR GADDAFI AMEWAHI KUYATABIRI HAYA YOTE, kipindi cha uhai wake! kua yatakuja magonjwa ya virusi na tutauziwa chanjo zaidi na zaidi!

USISAHAU KUNAWA MIKONO KWA MAJI TIRIRIKA, KUVAA BARAKOA NA KUJITAKASA MIKONO YAKO KWA SANITAIZA, pia fanya mazoezi na kula matunda kuboresha kinga ya mwili, Huku ukiendelea kuchapa kazi kukuza kipato chako kwa ajili ya wanao na taifa kiujumla!

kumbuka:- Afya yako ni jukumu lako namba moja, usiibebeshe serikali kwa asilimia kubwa!.

Kwamba una matusi dhidi ya mleta hoja? Hiyo ni kuonyesha jinsi ulivyokuwa huna hoja. Waungwana hujadili hoja si mleta hoja.

Ukweli mchungu huu hapa:

1. Si mataga wala magufuli waoweza kuwa wakatoliki kuliko papa. Au nasema uongo ndugu zangu?

2. Si mataga wala magufuli wanaoweza kusimama popote katikq dunia hii waka "claim supremacy" yoyote dhidi ya Bill Gates. Kwani hawana lolote waliloifanyia dunia wala jamii yoyote zaidi ya wizi wa kura, kupora haki za watu, kupora uhuru wa watu na huku wao wakiwa hata hawalipi kodi yoyote. Au nasema uongo ndugu zangu?

3. Magufuli kama rais wa nchi anawajibika moja kwa moja na dharura hii inayolipiga taifa kwa sasa.

Hawezi kuukwepa wajibu huo. Vinginevyo kama kaamua kiungwana kuachana na kazi hii ya urais ambalo kwa mujibu wa katiba hiyo ni kazi yake ya moja kwa moja. Au nasema uongo ndugu zangu?

4. Umeona tuna shida na kunawa mikono au kubwa barakoa mburula wewe?

Tunashida na kuepuka misongamano na kubakia majumbani kama ilivyo shauriwa na mataga mwenzenu hapa kama alivyojitambulisha mwenyewe:

Tuna epuka vipi misongamano au hata kubakia nyumbani wakati kodi zinaongezwa dhidi yetu?

Hivi huwa mnatumia akili za vichwani kufikiria mambo mamburula nyie?

Makeke mengi huna lolote!

Jikiteni kwenye mada jombi matusi peleka kwa Lumumba utalipwa buku 7.
 
Afya yako ni jukumu lako namba moja, hizo kodi ni za kutumika katika usalama wako na kurahisisha maisha kiujumla, aghalabu miundombinu, huduma nafuu za kimaisha kama umeme, afya(hospitali) n.k japo bado hawajafanikiwa kwa asilimia mia ila nina imani mambo yatakuja kua mazuri huko mbeleni haijalishi ni nani atakaekua madarakani!

Huwezi kuacha kulinda afya yako kisa ukijua kua serikali itakuja kukulindia na kukutibu!.

Afya yangu ni jukumu langu. Wao jukumu lao kunikamua kodi.

Jombi ulichokisema kimsingi ni kuwa watu hawa ni mzigo tu kwetu, hawatufai na wala hatuwahitaji. Kwamba wanaendelea na maisha business as usual. Wanatupandishia na kutuongezea kodi ila yanayotupata hayawahusu?

Hujui unachokisema.
 
Afya yako ni jukumu lako namba moja, hizo kodi ni za kutumika katika usalama wako na kurahisisha maisha kiujumla, aghalabu miundombinu, huduma nafuu za kimaisha kama umeme, afya(hospitali) n.k japo bado hawajafanikiwa kwa asilimia mia ila nina imani mambo yatakuja kua mazuri huko mbeleni haijalishi ni nani atakaekua madarakani!

Huwezi kuacha kulinda afya yako kisa ukijua kua serikali itakuja kukulindia na kukutibu!.
Rudi shule ,hujui chochote
 
Kuna ndugu yako yeyote au jirani yako amekufa kwa Corona?

Swali la kijinga lisilohusiana na mada kabisa.

"Typically irrelevant and out of context."

Hata hivyo kwa kukusaidia wewe ambaye ungependa kujitoa ufahamu, nilikwisha jibu swali hili way back July mwaka jana:

Ukipenda na updated list uniambie.
 
Ukipenda na updated list uniambi

Swali la kijinga lisilohusiana na mada kabisa.

"Typically irrelevant and out of context."

Hata hivyo kwa kukusaidia wewe ambaye ungependa kujitoa ufahamu, nilikwisha jibu swali hili way back July mwaka jana:

Ukipenda na updated list uniambie.
Unapelekeshwa na habari za mitandaoni Kama li ng'ombe ,una evidence wewe Kama wewe?haujiulizi kwa Nini Kia January ndo Mambo hayo yanaibuka?
 
Hahaaahaa ha ha. Umesahau swali lako lilikuwa lipi?

Umekuja na mapya eeh? Taabu ni kuwa hamna hoja!

Actually ling'ombe ni wewe na mataga wenzio ambao hadi sasa tunao ushahidi huu:

1. Mmejitahidi kutuonyesha kuwa mu waumini zaidi kuliko viongozi wenu wa dini.
2. Mmejitahidi kutuonyesha kuwa mu bora sana kuliko wafadhili wa dunia hii ambao aghalabu ni wana credibility zao.
3. Mmejitahidi kugombelezea kuwa serikali haina wajibu wowote kwa raia kwenye gonjwa kama hili linalotukabili sasa.
4. Mmejitahidi kuonyesha chanjo ya ugonjwa huu haina nia njema kwetu. Mkipoka sauti za walio wahanga wa wazi wenye uhitaji mkubwa nayo.

Kama ming'ombe hamna hoja na majiribio yenu yote yamegonga mwamba.

Mapya ya January uliyokuja nayo rejea nayo Lumumba unaweza jipatia buku 7 huko.

Huu ndiyo ulio ukweli mchungu.

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Kwa hiyo huo ugonjwa umekua wa kisiasa ,unayetofautiana nae kimtazamo ni ccm? rubbish.kiladakika siku zote anazaliwa na kufa mtu.haijalishi Nani,acha kukurupuka kiduanzi,
 
Rubbish ni huu utopolo ulioandika hapa. Kumbe chama kinachoguswa na bandiko hili ni CCM? Umejuaje mkuu?

Kwa kutambua uwepo wa "taga" kama wewe bandiko limekuwa wazi kuiangazia:

"Nguvu kubwa inayotumika kuhalalisha vifo hata kama ni wazi kuwa vimetokana na ugonjwa huu huu, kuwa ni vifo vya kawaida na eti ni mapenzi ya Mungu tu."

Ubinafsi na udhalimu mkubwa. Mtajibu nini kwa Mungu mumiani wakubwa nyie?

Ndiyo maana si ajabu kumsikia mtu mzima akisema "corona hamna, corona ilkwisha, hapana, ipo kidogo tu."

Sentensi moja toka kwa mtu mmoja itolewayo kwa wakati mmoja na mtu yule yule? Aaaah wapi. Fumbo fumbieaneni wenyewe Lumumba. Kwetu sisi si kwa utopolo kama huo!

Utopolo kama huo pelekeni Lumumba utalipwa buku saba.

Ni wazi kuwa mmetambua hamna hoja. Mtakuwa mmefahamu ulaghai wenu huu hauuziki.

Mi-taga yote imerejea mashimoni mwao kama mipanya kama iliyomwagiwa maji. Haina hoja!

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
ASHAKUM SI MATUSI.

Umeandika kwa hisia sana ila bado umeandika ujinga, na unatumia hisia zako ili ueleweke katika upuuzi wako.

NB: mimi naamini hao mabeberu wangekua wana nia ya kutusaidia wangeleta hiyo chanjo bure, maana here we are talking about the survival of the human race!, hiyo chanjo nyi mnaisikia tu lakini ni very expensive! refere SOUTH AFRICA,.

Pia kisa tulipokea chanjo zingine haimaanishi ndo tupokee zote, nadhani katika huu ugonjwa(corona) umekaa kisiasa na maslahi sana ndo maana hata raisi amechukua maamuzi magumu katika matamko aliyoyatoa(sio kazi rahisi kua raisi) .

MUAMAR GADDAFI AMEWAHI KUYATABIRI HAYA YOTE, kipindi cha uhai wake! kua yatakuja magonjwa ya virusi na tutauziwa chanjo zaidi na zaidi!

USISAHAU KUNAWA MIKONO KWA MAJI TIRIRIKA, KUVAA BARAKOA NA KUJITAKASA MIKONO YAKO KWA SANITAIZA, pia fanya mazoezi na kula matunda kuboresha kinga ya mwili, Huku ukiendelea kuchapa kazi kukuza kipato chako kwa ajili ya wanao na taifa kiujumla!

kumbuka:- Afya yako ni jukumu lako namba moja, usiibebeshe serikali kwa asilimia kubwa!.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahaaahaa ha!

Nisiache kukumbusha kuwa kwa huu utopolo ulioandika hapa ungewahi kwenda kuondoa uungaji mkono wako faster kwenye comment #2.

Kama #2 umeunga mkono na hapa haya ndiyo maoni yako katika ubora wako, kwa hakika mmekwisha chachawa. Mmetepeta.

Hamjui wala hamna habari ya wapi ni kulia au kushoto. No wonder mna comment bila kusoma hoja:

IMG_20210130_014536_943.jpg

Utopolo wenu kama ulioandika kwenye bandiko lako, ni wa maana kwenye himaya ya mfalme juha pekee.

Wajameni Mgogohalisi, Sky Eclat, Mkaruka hebu oneni hii mbuzi.
 
Afya yangu serikali haiusiki ila kodi inayotokana na kipato changu inahusika sivyo?. Akili za mataga hizi.
Watu wa ajabu ajabu hawa ndiyo wamejimilikisha maamuzi ya namna ya kutobishana kwenye ugonjwa huu.

Eti kuwa na kwa hilo ni whether we like it or not.

Hongereni sana maaskofu kanisa katoliki kwa kuuweka utu na maslahi ya taifa mbele.

Hauko usahihi wala uhalali wa kulitelekeza gonjwa hili kwa wananchi na kuwaachia kufa nalo.

Na tuzipate sauti vilivyo:

We can't breathe!

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Back
Top Bottom