WAKO WAPI WATU WAKO
JF-Expert Member
- Sep 26, 2017
- 2,356
- 3,114
Uzembe wa serikali ya awamu ya Tano, lazima usemwe....uzalendo ni kuwa mkweli sio unafiki..Wanabodi,
Kila nipatapo fursa, huwaletea mfululizo wa makala zangu elimishi za kuhamasisha uzalendo zinazoitwa "Kwa Maslahi ya Taifa" ambazo huwa ziko kwa mtindo wa maswali. Makala ya leo sio ya swali bali ni wito.
Tanzania ni nchi yetu sote, na imetokea sisi Watanzania tuko wengi na tumetapakaa duniani kote. Kutokana na kutapakaa huku, Watanzania tofauti tofauti tuna uwezo tofauti na exposure tofauti kutokana na experiences tofauti tofauti ya huku tulipo, lakini bado tunawajibu wa kuelekeza uzalendo wetu kwa nchi yetu, Tanzania yetu au Mama Tanzania, hivyo kama kuna yeyote mwenye uwezo wowote wa kusaidia, asaidie.
As the Corona situation ya maambukizi ya local transmissions is escalating, nimenote huku kwenye mitandao ya kijamii, baadhi yetu tumeanza kunyoosheana vidole vya kulaumu, kuwa hatukufanya hiki au kile ndio maana maambukizi yamefikia kiwango hiki.
Tangu kuibuka kwa janga hili la Corona Mwezi December mwaka jana, kila nchi ilichukua hatua za kuzuia na kujiandaa kukabiliana nayo ki vyake vyake. Sisi Tanzania pia kupitia serikali yetu nasi tulichukua hatua kivyetu. Ziko nchi za jirani zetu wao waliamua kuchukua hatua zao kwa copy and paste ya nchi nyingine walichofanya ikiwemo hatua ya lockdown, Tanzania tukaamua hatuigi, hakuna lockdown na rais wetu Magufuli kutuondoa wasiwasi kwa kusema Tusitishane, na kutuhimiza Watanzania tuendelee kuchapa kazi kwa kuzingatia maelekezo ya kitaalamu na kusema haka ka Corona ni ka ugonjwa kadogo, ni kashetani, tuka mkabidhi Mungu, na kwenye Mungu akatenda. Tatizo la Corona wa kulaumiwa ni Serikali kwa asilimia 100% - JamiiForums
Mwanzoni Mungu ametenda na mpaka sasa anaendelea kutenda, jana tumemaliza siku 3 za maombi ya kitaifa dhidi ya janga la Corona, hivyo tunamuomba Mungu huku tunajisaidia.
Kufuatia kuongezeka kwa kasi ya maambukizi ya Corona, huku kwenye mitandao ya kijamii, tunaanza kulaumiana na kunyoosheana vidole kuwa Corona inasambaa kwasababu hatukufanya abcd.
Hii ni mifano
Mkuu Nguruvi3 at this juncture, lets stand as one kusaidia. Je, Watanzania wenye uwezo wa kusaidia, jee tuisaidiaje serikali yetu ili ishindindwe?.
Kwa vile sasa ni April na umma haupukutiki bali unaambukizwa, na kwa vile umeishajua kuwa mwezi May umma utapukutuka, hivyo unashauri tujiandae kuona umma unavyopukutika!, kwanini usisaidie kuzuia umma wa Watanzania usipukutike?
Usaidizi huo, sio lazima uwe kama ule wa Rostam Aziz or Mo Dewji, bali hata kwa kuandika tuu humu jf na vyombo vyetu vya maamuzi watasoma na kufanya uamuzi wafuate au waache, ili itakapofika hiyo May, tutakapo anza kuona na kushuhudia jinsi watu wanavyopukutika, angalau tutasema, tuliona kabla, tukaonya, tukashauri, tukapuuzwa na sasa haya ndio matokeo.
Kwenye situation hii tuliofikia, swali langu hili
WanaJF, Je tuisaidie Serikali yetu inaposhindwa au tusubiri ishindwe, tuibeze na kuizomea kuwa haiwezi? - JamiiForums
Mkuu Retired, if you can help, just help out, kama una ushauri mzuri wa jinsi ya kusaidia, wewe toa tuu huo ushauri, sasa issue ya kama ushauri wako utapokelewa utakubaliwa au utafanyiwa kazi au laa, hili sio letu, hili ni la ngazi za maamuzi, whether ushauri wako utatekelezwa au utapuuzwa, hili sio lako, wewe utakuwa umetimiza wajibu wako na huu ndio uzalendo wako kwa nchi yako.
Hitimisho
Nimalizie kwa kutoa wito, janga la Corona ni janga letu sote sisi Watanzania, haijalishi uko wapi na unaishi nchi gani, as long as wewe ni Mtanzania, hata kama umejilipua, lakini kwenu ni Tanzania, una wajibu wa kuisaidia nchi yako kwenye nyakati kama hizi. Huu sio wakati wa kulaumiana na kunyoosheane vidole vya we didn't do this and that, huu ni wakati wa kusimama pamoja, kushikamana na kusaidiani, kama unaweza kusaidia kwa lolote, chochote, hali na mali au hata ushauri tuu to help out the situation, please just do!, usisubiri uombwe, msaada na yeyote. Jitokeze tuu saidia!. Vinginevyo...Nyamaza!
Nawatakia Jumatatu Njema
Paskali
Korona serikali ilipata nafasi ya kuizuia isienee kwa kasi hii...ikazembee
Wacha watu watapike nyongo...tufe kwa Korona lkn ukweli usemwe na hatua za kujihami na kuenea kwa ugonjwa zichukuliwe...
Pitia Kauli za Makonda toka ugonjwa unaingia Nchini na muendelezo wake..
Tuko ktk mahangaiko haya, sababu ya uzembe wa Viongozi wa Serikali na Chama kama Ndg Polepole... Kuifananisha korona na Upinzani.. Ni stupidity
Uzalendo ni Ukweli.. Korona inaua na inazidi kuenea nchini....sababu ya kushindwa mapema kuchukua hatua.
Sent using Jamii Forums mobile app