#COVID19 Corona Tanzania ni vita kati ya Mungu na wasiomwamini kuwa aweza shinda Corona Mungu atashinda hajawahi shindwa

Basi kila MTU haamini anachoamini.
Mimi na magufuli tumemuamini MUNGU ANaweza kutuponya..
Na wewe unayemuamini mzungu na chanjo zake endelea kumuamini kikubwa UHAI
Kazi ya chanjo sio kuponya
 
Wapo wanaokataa uwepo wa Mungu katika Taifa hili kwa sababu katika taifa hili sio lazima kuamini Mungu au kuwa na dini. Tuachane na hizi kauli za kubembelezana sana, tujikite kudai ujuzi na taaluma katika kuliongoza taifa sio Imani za watu.
Uko sahihi, hayo yote inatakiwa yaende pamoja
 
Kwani chanjo katengeneza Mzungu tu? Wewe vipi! Kachukue za Wachina kama tatizo ni wazungu
Basi kila MTU haamini anachoamini.
Mimi na magufuli tumemuamini MUNGU ANaweza kutuponya..
Na wewe unayemuamini mzungu na chanjo zake endelea kumuamini kikubwa UHAI
 
Corona Tanzania ni vita kati ya Mungu na wasiomwamini kuwa aweza shinda Corona Mungu atashinda hajawahi shindwa

Wasiomwamini wanachekelea wakisikia tetesi kuwa kuna Corona wanahoji Mungu kuwa nyie mliojitia kuomba kiko wapi ? Shetani mleta Corona kamshinda Mungu huyo Mungu wenu bure kabisa!!!

Hii vita Mungu wa Tanzania ataibuka mshindi tena kwa knock out

Wazungu wajiandae kutushangaa Watanzania kwa ushindi mnono awamu hii tena

Tanzania kwa sasa ndio taifa teule limeibwaga Maka na Medina na Vatican na Israel kwenye vita dhidi ya Corona kwa kumtumia Mungu yaani using God factor on war against Corona a weapon that other countries have rejected
Kuchukua tahadhali ni kutokuamini, kupiga nyungu ni kuamini, hata hao maaskofu wapo upande na shetani rusifa.
 
Tanzania kwa sasa ndio taifa teule limeibwaga Maka na Medina na Vatican na Israel kwenye vita dhidi ya Corona kwa kumtumia Mungu yaani using God factor on war against Corona a weapon that other countries have rejected

Huo ni Ujinga mtupu bila shaka hujui kanuni za Mungu zipoje, huko ni kumjaribu Mungu, naye huwa hajaribiwi kamwe.

Ipo hivi; kumtegemea Mungu katija shida bila kufanya jitihada ya kibinadamu katika shida huko ni kumjaribu Mungu na kutegemea jitihada za kibinadamu pekee bila kumtegemea Mungu hicho ni kiburi. Kinachotakiwa ni mambo yote hayo mawili yaende sambamba yaani kufanya jitihada za kibinadamu na kumtegemea Mungu, ukifanya jitihada za kibinadamu na ukamtegemea Mungu, Mungu hubariki hizo jitihada zako na sio kukaa tu bila kufanya jitihada yoyote huku ukisubiri Miujiza kutoka kwa Mungu.

Mungu katupatia akili na uwezo wa kujisaidia sisi wenyewe katika shida zetu sasa kwanini tusitumie uwezo na akili hizo alizotupatia kutanzua shida zetu au hivyo vipawa ni kwa ajili gani???---- Mungu humsaidia yule anayejisaidia na kumuomba.

Nyie mnataka hadi tufe wangapi ndipo mjue juhudi za kibinadamu zinatakiwa zifanywe kwanza sambamba na kumtegemea Mungu.

Masheikh na Maaskofu wetu wameonyesha udhaifu mkubwa sana katika suala hili, wamekaa kimya wakimuacha Muheshimiwa Rais akitekekeza wajibu wao wa kidini kimakosa, yawezekana nadhani hata hao masheikh na Mapadre wanaamini kwamba Mungu "NI MUWEZA WA KILA JAMBO BILA KANUNI"---- Mungu ni muweza wa kila jambo jema ndani ya kanuni, Kanuni ni hii; lazima kwanza tufanye juhudi za kibinadamu zilizondani ya uwezo wetu halafu ndipo tumtegemee Mungu atie baraka katika juhudi zetu.
 
Kiimani, kusema covid-19 ipo ni kukubali kushindwa. Ndiposa Imani inaelekeza kukataa mabaya (yaani hata kama yapo unasema hakuna kitu kama hicho). Ndio tofauti ya Sayansi na Imani!
Unaona imeandikwa 4 unakemea unanena kwa lugha oooooo naona 7. Tofautisha ukweli na uongo. Covid19, 20 na 21 ipo. Ongea na MUNGU wako kwa imani mwambie watu wangu wanaangamia kwa corona, nae atakuonyesha mlango wa kutokea. Yaaan unaona corona afu unasema pnemonia.
Huyo Mungu gani sasa unamchezea ivo.
Unaona mkate afu unasema ni kuku.
Walokole mmetufikisha hapa aiseeee
 
Umeelewa hoja vizuri sana
 
Ndio aweza hama nchi akaenda nchi inayomtegenea ndio maana alikuwa Mungu wa Ibrahim na Isaka na Yakobo wakati kulikuwa na mamilioni ya watu duniani akiwemo farao lakini hakuitwa Mungu wa Farao

Mungu sio wa kila mtu ni wa wale tu wamtegemeao
Sisi Watanzania ni Mungu weti sababu tunantegemea kwenye vita dhidi ya Corona wakati wengine hawamtegemei
What a joke!! Ninyi mikono inavuja damu kwa udhalimu, wizi, zinaaa, kuminya haki za watu, ushirikina etc ndiyo muwe na Mungu??? Endeleeni kumdhihaki mtapata majibu yake...
 
Tatizo ni kuwa haya maneno makuu kuhusu Mungu tunayasema kama matokeo ya kujifariji dhidi ya hofu iliyo ndani yetu,hatuyasemi kutokana na imani yetu na vile tunavyomjua Mungu,na tunvyompenda,
Hizi ni zama ambazo jina la Mungu linatumika vibaya sana kwa faida binafsi,
Well said
 
Mbona malaria,ukimwi na mengine mengi hayajatokomea ilihali watu wanamwomba mungu awaponyeshe.....sasa kwanini leo asaidie kwenye Corona..... mungu hafanyi kazi kwa njia unayoitaka wewe.....
 
Corona Tanzania ni vita kati ya Mungu na wasiomwamini kuwa aweza shinda Corona Mungu atashinda hajawahi shindwa

Wasiomwamini wanachekelea wakisikia tetesi kuwa kuna Corona wanahoji Mungu kuwa nyie mliojitia kuomba kiko wapi ? Shetani mleta Corona kamshinda Mungu huyo Mungu wenu bure kabisa!!!

Hii vita Mungu wa Tanzania ataibuka mshindi tena kwa knock out

Wazungu wajiandae kutushangaa Watanzania kwa ushindi mnono awamu hii tena

Tanzania kwa sasa ndio taifa teule limeibwaga Maka na Medina na Vatican na Israel kwenye vita dhidi ya Corona kwa kumtumia Mungu yaani using God factor on war against Corona a weapon that other countries have rejected
Acha ujinga,Kama Mungu ndivyo anavyotumika kutatua matatizo ya watu,unaonaje tumtumie hivyo kutatua vifo vya watoto kwa malaria,umaskini,ukosefu wa ajira,kwanini tunajenga zahanati,hospitari,tunasomesha madakitari,si tupige dua tu,Mungu atafsnya miujiza?!
Watoto wadogo wakizaliwa,wanapewa chanjo za polio,korona hatutaki chanjo,tunataka Mungu aponye kimiujiza,sasa tusipereke watoto kupewa chanjo,tuombe Mungu tu!!
"Usiende kwa Mungu. Kuomba furniture,Mungu ameishatengeneza Miti,kazi ya kutengeneza furniture ni kazi ya Mwanadamu.
Hizi akili za kijinga za kilikole,zinapotosha sana,
Hazitofautiani na ile familia inayoamini mtu akiiugua malaria asiende hospitari,apige maombi tu,Kuna washenzi wengine walipiga kambi airport wakitaka kwenda ulaya bila kufata taratibu,wakiamini imeandikwa wataenda duniani kote kutangaza injili.

Sent from my TECNO CD6 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom