Corona Tanzania: Naiomba serikali itoe tahadhari iwapo kuna siku marufuku za kusafiri na kulala lodge zinaweza kuwepo

kibaravumba

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
6,635
7,005
Hii ni kwa sababu baadhi ya watanzania tuna safari muhimu sana humu humu nchini ila ikitokea kama inayotokea Uganda, Rais anaamka na kutangaza marufuku ya kulala lodge, ama kutoka nje,italeta shida sana.

Maana unakuwa umesafiri na upo lodge.Ghafla inatoka marufuku ya kulala lodge,halafu kama haitoshi inakuja marufuku ya kusafiri, mbaya zaidi pia ipo marufuku ya kutoka nje. Hali hii italeta maumivu na adha kubwa sana.

Naomba serikali yangu kama kuna dalili za kuongezeka kwa matukio ya kupata wagonjwa wapya,ama kuna wasi wasi wa kuenea kwa ugonjwa huu, ianze kutoa tahadhari mapema ili watu walio safari warudi ama walio na mpango wa kusafiri mikoani waache.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni angalizo zuri, sisi Tanzania hatuigi yoyote, wananchi endeleeni kupiga kazi huku mkizingatia maelekezo ya jinsi ya kujikinga na Corona.
P
Mkuu hizi kauli zako utakuja kuzijutia, tuombe uzima tu.

Hivi kuna maagizo ya wataalam ambayo yanapaswa kupuuziwa kwenye ugonjwa huu wa corona?

Mtakuja kujutia kauli zenu. Trump mwenyewe anataka watu wapige kazi, lakini wataalam wamempiga pini, na kwasababu siyo mambo ya kisiasa, he just swallowed his pride and moved on! Nothing he could do about it! Pamoja na ukweli kwamba uchumi unadidimia siku baada ya siku.
 
Serikali ni lazima iwe wazi ili maeneo yaliyoathirika zaidi yawekewe vikwazo vya movement ili kuokoa wananchi wengine na Taifa kwa ujumla.
 
Spika wa Bunge kasema muda huu, Tanzania haitaiga kutoka nchi nyingine namna ya kujikinga na corona. Hivyo lodge zitafanya kazi kama kawaida, kusafiri kama kawa na bar zitatuburudisha kama ilivyozoeleka. Ondoa hofu mkuu, wewe endelea na mishe zako. LAKINI zingatia maelekezo ya kujikinga na corona.
 
Mkuu hizi kauli zako utakuja kuzijutia, tuombe uzima tu.

Hivi kuna maagizo ya wataalam ambayo yanapaswa kupuuziwa kwenye ugonjwa huu wa corona?

Mtakuja kujutia kauli zenu. Trump mwenyewe anataka watu wapige kazi, lakini wataalam wamempiga pini, na kwasababu siyo mambo ya kisiasa, he just swallowed his pride and moved on! Nothing he could do about it! Pamoja na ukweli kwamba uchumi unadidimia siku baada ya siku.
Marekani ni Marekani, Italy ni Italy, China ni China, na Tanzania ni Tanzania.
Kwenye Corona wenzetu wanapambana na kirusi tuu, sisi we have gone further, tumekishtukia kirusi cha Corona sio kirusi tuu bali ni shetani disguised as kirusi hivyo sisi tumemkabidhi Mungu ambaye ni kiboko wa shetani, na tayari Mungu anatenda, ameisha tukingia mkono wake, hakuna lockdown wala nini, tunazingatia maelekezo ya wataalamu na kuendelea na shughuli zetu kama kawaida.
Ukilikabidhi jambo kwa Mungu, umemaliza
Mungu hawezi kutuangusha.
P
 
Night curfew ikitangazwa kuna uwezekano idadi ya watu wanaokulana kimasihara ikaongezeka maana mtu atajifanya curfew ilimkuta akiwa kwenye utafutaji basi ikabidi alale huko huko
 
Namh'ala Mayalla
Nimekuelewa vyema kabisa

Tena tusitishane tishane bana...KOLONA kitu gani bana
...tuchape kazi kama mchwa

Tunaishukuru awamu ya 5 kwa kukipiga vita hiki kishetwani
Marekani ni Marekani, Italy ni Italy, China ni China, na Tanzania ni Tanzania.
Kwenye Corona wenzetu wanapambana na kirusi tuu, sisi we have gone further, tumekishtukia kirusi cha Corona sio kirusi tuu bali ni shetani disguised as kirusi hivyo sisi tumemkabidhi Mungu ambaye ni kiboko wa shetani, na tayari Mungu anatenda, ameisha tukingia mkono wake, hakuna lockdown wala nini, tunazingatia maelekezo ya wataalamu na kuendelea na shughuli zetu kama kawaida.
Ukilikabidhi jambo kwa Mungu, umemaliza
Mungu hawezi kutuangusha.
P

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii ni kwa sababu baadhi ya watanzania tuna safari muhimu sana humu humu nchini ila ikitokea kama inayotokea Uganda, Rais anaamka na kutangaza marufuku ya kulala lodge, ama kutoka nje,italeta shida sana.

Maana unakuwa umesafiri na upo lodge.Ghafla inatoka marufuku ya kulala lodge,halafu kama haitoshi inakuja marufuku ya kusafiri, mbaya zaidi pia ipo marufuku ya kutoka nje. Hali hii italeta maumivu na adha kubwa sana.

Naomba serikali yangu kama kuna dalili za kuongezeka kwa matukio ya kupata wagonjwa wapya,ama kuna wasi wasi wa kuenea kwa ugonjwa huu, ianze kutoa tahadhari mapema ili watu walio safari warudi ama walio na mpango wa kusafiri mikoani waache.

Sent using Jamii Forums mobile app
Marufuku kama hizi zinatolewa na madikteta wa kiafrika huwezi kuona Dikteta mwema kama Wa Urusi, china au Korea akifanya upumbavu wa namna hii.
 
Back
Top Bottom