Corona Response: Waasia walishikamana, Wazungu wamepaniki, Waafrika tusipokuwa makini tutapoteana

Kingsmann

JF-Expert Member
Oct 4, 2018
4,446
16,299
Umofia wananzengo.

Kama mnavyojua dunia nzima ni kama ipo vitani kupambana na huyu kirusi Corona anayesababisha ugonjwa wa COVID19 (Jina rasmi lililotolewa na WHO).

Hii vita ni mbaya sana kwa sababu mnapigana na kitu chenye kuweza kuwadhuru nyie ila nyie hamna njia yoyote ya kukidhuru.

Hii vita ni mbaya sana sababu kila mtu ni askari aliye uwanja wa mapambano, haijalishi wewe ni mtoto, mtu mzima, raia wa kawaida, kiongozi, waziri hata rais na mfalme wapo uwanjani kupambana.

Kwa sababu hiyo ya kuwa kila mtu ni askari, basi unahitajika umakini wa hali ya juu sana kuweza kukabiliana na huyu adui kwa sababu sio watu wote wamepitia mafunzo ya uaskari.

Uaskari ninaouzungumzia hapa sio ule wa kuweza kushika silaha, hapana. Nadhani mnanielewa.

Katika moja ya mbinu kubwa ya kushinda vita yoyote ile ni psychology ya askari towards yule adui mnayeenda kupambana naye. Ni lazima kwanza askari wajengewe imani kwamba adui wanayeenda kupambana naye ni mwepesi na anapigika kirahisi tu.

Mkifeli hapo basi jua hiyo vita mnaenda kushindwa vibaya mnoo.

Hivyo katika haya mapambano dhidi ya Covid19 cha msingi sana ni kuwajengea wananchi imani ya ushindi, watu wasiingiwe na hofu, hilo likifeli basi taifa litaingiwa na panic na mbinu zingine zote za kucontrol huu ugonjwa zitafeli.

Katika kitu ambacho tunatakiwa tuwapongeze Wachina ni kitendo cha raia wake kuwa na utulivu wa hali ya juu sana japokuwa ugonjwa ulianzia kule.

Wachina wameushinda huu ugonjwa japokuwa hamna dawa sababu ya kutopanic, wamefuata mbinu zote walizokuwa wanaelekezwa na watawala wao na hatimaye maambukizi mapya yameisha kabisa.

Wenzetu Wazungu hali ni tofauti kabisa. Wamepanic mpaka basi, kwa kifupi mzungu anaogopa kifo sana kuliko kitu chochote. Watu wanafanya manunuzi kuzidi uwezo wao.

Wanafanya overstocking kwa hofu ya kwamba wakiambiwa wabaki majumbani itakuwaje? Ukienda supermarkets hakuna kitu, watu wamesomba na kujaza majumbani mwao, nyumba zimegeuka stoo.

Sasa tujiulize Afrika tutarespond vipi? Na sisi tutapanic kama wazungu ama tutakuwa imara kama wachina?

Mungu tuepushie mbali na hili janga.
 
Naungana na wewe kuhusu suala hili. Wasije wakaamua kufunga shule zote na vyuo vyote kwani hili lita leta shida kubwa zaidi ya tunavyotegemea. Keep cool. Do not panic.
 
Back
Top Bottom