#COVID19 Corona ni ugonjwa halisi

EngutanK

Member
May 3, 2021
99
244
Corona, au uviko ni ugonjwa halisi na upo duniani kote hadi sasa umeingia hadi Alaska nchi zenye baridi sana.

Magonjwa yote yatokanayo na virusi hukabiliwa(huzuiwa) na Chanjo (vaccine) tangu enzi za Nuhu. hakunaga anti-virus kama vile Anti-biotics ambazo huuwa Bacteria.

Baadhi ya magonjwa yatokanayo na Virus ambayo yamedhibitiwa na chanjo hadi sasa
1. buba (yowes)
2. Ndui ( small -pox
3. Surua (miseales)
4. Ugonjwa wa kupooza (polio)

na sasa COVID-99 kanuni ni ile ile.

Jamani Sayansi huwa haidanganyi, ila Imani au ulimwengu wa kiroho ni mambo ya kufikirika na kusadikika tu huwezi kuyadhibitisha kwa kanuni yoyote.

Mfano MV Bukoba ilizama kwa sababu ya kupakia mzigo mwingi hadi kuvunja kanuni fulani iitwayo ARCHIMEDES PRINCIPLE LAW OF FLOATATION. ambapo ili kitu kielee inabidi density ya maji iwe kubwa kuliko kitu kenyewe kikiizidi kitazamaa tu. Hivyo basi ikitokea MV Bukoba ingine ijaze mzigo kama ile iliyozama nayo itazama tu hata mkeshe mkiomba, Sayansi huwa haidanganyi.

CORONA ipo, na ni halisi imetafutiwa chanjo aina mbali mbali kuikabili mfano wa chanzo za Corona ni kama Modenna, Payunk, Ziteccazitecaa, Johnsons-Johnsons ni hivyo.Mungu kasaidia jitahada za walimwengu wamepata chanjo ya CORONA walimwengu Mkachanje, Ukipata virus wa Corona waingie mapafuni utakufa tu hata ukeshe ukiomba

Aksanteni -Dr. Engutan-K
 
Mwili wa mtu mzima hauna ufanisi wa kukabili tiba ya chanjo_ni uhuni wa mchana kweupe.

Anyway ni hiari ya mtu kuchanja ama kutochanja
 
Hakuna njia nyingine zaidi ya kuchanja kupunguza vifo vinavyotokana na corona. Na usisubiri mpaka unaona dalili za corona, ndio ukimbie kuchanja, chanjo haitafanya kazi. Umri ukiwa umeenda kidogo, una magonjwa, KACHANJE.
 
Mwili wa mtu mzima hauna ufanisi wa kukabili tiba ya chanjo_ni uhuni wa mchana kweupe.

Anyway ni hiari ya mtu kuchanja ama kutochanja
Chanjo ya ndui (small-pox vaccine) walikuwa wanachanja watu wazima, chanjo hiyo ilitamalaki kweli kweli nakumbuka wachanjaji waliwafuata wateja minadani, walikuwa wanawasubiri nje kwenye nyumba za ibada mfano kanisani, misikitini, walikuwa wanawafuata wateja kwenye stesheni za reli nakumbuka , njiani kwenye njia panda n.k . jitihada hizo zimezaa matunda ugonjwa huo umetoweka kabisa hasa nchi za Afrika.

Mgonjwa wa ndui alikuwa akipona basi anakuwa anabaka mabaka ya makovu usoni walikuwepo sana miaka ya sitii na sabini mwanzoni hivi sasa nafikiri wahanga wote wa ugonjwa ndui wamekufa sioni tena wenye mabaka

Wewe ulikwa wapi? hukuona watu wazima hadi wazee wakichanjwa chanjo ya ndui? Tiba ni fani kama fani zingine kama haiwahusu msiingilie mnawapotosha wanachi.
 
Kwani nani kakukataza.! Nenda kachanje

Hii ni 2021 age of Aquarius kuwa mjinga ni uamuzi
 
Back
Top Bottom