Corona ni jambo lenye mkanganyiko sana, Watanzania wengi wamelipotezea

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
7,293
2,000
Tangu Serikali ya Tanzania kuacha kutoa taarifa za Corona hadharani kuna mambo mengi sana yanayosemwa na wanaharakati hasa mitandaoni kuhusu kuwepo kwa Corona kila inapotokea taarifa ya kifo cha ghafla.

Bahati mbaya sana hakuna njia mbadala zaidi ya chanjo na mfumo thabiti wa afya ya mwili kupambana na huu ugonjwa. Hii ni kuzingatia muktadha wa nchi yetu kwamba hakuna anayetaka au angependelea kile kinachoitwa "lockdown".Hii ni kwa kuzingatia kwamba hata sehemu zilizoweka lockdowns bado kumekuwepo na vifo vingi.

Hivyo basi watu waache kushadadia vifo vinavyohusishwa na Corona kwa sababu hakuna mtu mwenye mawazo tofauti yenye unafuu ya kupambana sawa sawa na ugonjwa huu.

Jambo la muhimu ni watu wahakikishe wanajenga afya zao vyema kupambana na ugonjwa huu kwa sababu haitakuwa rahisi Waafrika kupata chanjo kwa ufanisi.Na maisha mengine yaendelee kama kawaida.
 

TODAYS

JF-Expert Member
Apr 30, 2014
7,340
2,000
NOTE:
Hapa jambo la muhimu ni watu wahakikishe wanajenga afya zao vyema kupambana na ugonjwa huu kwa sababu haitakuwa rahisi waafrika kupata chanjo kwa ufanisi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom