Corona: New Zealand siku ya 17 leo bila ya kirusi Corona nchini

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,815
35,804
Mabibi na mabwana hii ni habari njema na kumbe kweli inawezekana. New Zealand kafanikiwa kumgaragaza kirusi Corona vilivyo.

Hii leo kwa siku ya 17 hawana mgonjwa hata 1 wala maambukizi yoyote. Yote hii si kwa nyungu, maombezi wala mitishamba. Si kwa ubabarishaji wala kwa takwimu magumashi bali kwa kupambana

Wewe ni beberu kwa lugha yetu ya hapa kwetu 'ikungu lya bashashi'. Lakini kwa hakika tutake tusitake, kwa hili tunacho cha kujifunza

Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni

Kongole kwako beberu, umetuonyesha njia acha tuone kama nasi tutanyoa au tutasuka.

Source:

Tokea hapa, beberu anaondoa lockdown ndani ya nchi, macho kumchuzi, mipaka inaendelea kufungwa pia international flights zote zinaendelea kusimama.

Corona virus uletaye Covid-19 siku zako kwa waungwana wote zinaweza kuwa kweli zinahesabika!
 
Yule mwana mama wao Prime minister yupo poa sana

Wa kwetu sisi wanafurahia kuitwa mawe au mababa yao wakimaanisha kwao ununda ni sifa!

Inaweza kuwa si siku mbaya mama yetu Samia naye siku moja akikipokea kijiti.

Wamama walio waungwana, upole ni tunu!
 
Kisiwa kimewabeba na visiwa vingi coronavirus wanaisikia kwenye radio tu
Maana wao kuwa Kisiwa ni lockdown tosha kabisa

Hakuna lolote mkuu. Zanzibar je siyo kisiwa?

New Zealand wanaondoa lockdown sasa shughuli zote zinarejea rasmi. Mipaka bado inaendelea kufungwa. International flights zote zinaendelea kusimama.

Kwetu hukumwona Kigwangala akihanja hanja airport kupokea dege la kimataifa hali Corona bado ipo huru na bwerere?

Tusimlaumu dobi mkuu, kaniki mbona ni rangi yake? Mkuu hata ingekuwa je hali yetu ingekuwa hii hii tu.

Tuko kama tumerogwa au kupagawa hivi.
 
Mkuu Zanzibar pia wangefunga mapema (kama uchumi unaruhusu) wangeisikia tu
Na kwetu kusema mipaka iko wazi karibuni mimi nilikuwa najua ni ndoto tu maana kama wenye ndege hawajaziruhusu kupaa zitakujaje?
Ila mwezi huu usafiri kwa baadhi ya ndege zinaanza kusafiri ila sio kwa Amri ya waziri
Tunajiandaa kuja sasa
 
Mabibi na mabwana hii ni habari njema na kumbe kweli inawezekana. New Zealand kafanikiwa kumgaragaza kirusi Corona vilivyo.

Hii leo kwa siku ya 17 hawana mgonjwa hata 1 wala maambukizi yoyote. Yote hii si kwa nyungu, maombezi wala mitishamba. Si kwa ubabarishaji wala kwa takwimu magumashi bali kwa kupambana

Wewe ni beberu kwa lugha yetu ya hapa kwetu 'ikungu lya bashashi'. Lakini kwa hakika tutake tusitake, kwa hili tunacho cha kujifunza

Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni

Kongole kwako beberu, umetuonyesha njia acha tuone kama nasi tutanyoa au tutasuka.

Source:

Tokea hapa, beberu anaondoa lockdown ndani ya nchi, macho kumchuzi, mipaka inaendelea kufungwa pia international flights zote zinaendelea kusimama.

Corona virus uletaye Covid-19 siku zako kwa waungwana wote zinaweza kuwa kweli zinahesabika!

Ali implement WHO recommendation on combating the spread of coronavirus! It is no miracle! Just Science!
 
Back
Top Bottom