Corona na Funzo tulipatalo toka kwa Viongozi wa afrika. Leo hii watu wote wataumwa na kutibiwa hapa

GuDume

JF-Expert Member
Jan 18, 2015
6,652
14,247
Hili ni wazo ambalo pia kuna mtu ameliwaza kwa kina.

Tunafahamu kuwa viongozi wetu wamekuwa mara nyingi wakizitumia kodi zetu kwa maslahi yao hasa wanapoumwa.

Wameacha kujali hospital zetu sababu wao wakiumwa wamekuwa wakipelekwa ulaya ,marekani na india kwa matibabu.hili limewafanya wasiwaze sana kuboresha huduma ktk hosp zetu.

Sasa kaa ugonjwa huu wa Corona. Wote tutakaoumwa tutatibiwa hapa hapa Bongo.humu humu ndani.sababu Londo,India n.k hawapokei wagonjwa wa aina hiyo.

Sasa ndo wanapogundua kuwa ni bora kuandaa mazingira bora ya matibabu hapa nchini na si kwamba wakiumwa mafua au kikohozi wakafanye check up nje ya nchi.kwa kodi zetu na zenu walalahoi.

Itufunze badala ya kusema serikali ununue magari ya thamani kubwa ya juu kumbe ilipaswa itengeneze barabara wote tupite kwa gari zetu hizi hizi na hivyo wangebana matumizi pia.

La msingi sasa ni kuhakikisha matibabu yanaboreshwa tz nzima.haiwezekan vipimo vya corona virus vinapatikana dar peke yake.

Ilipaswa iwe kila hosp ya karibu katika wilaya au manispaa.tumeona kupanda kwa bei za sanitizer leo pharmacy moja sanitizer iliyokuwa inauzwa 7,000-12,000 nimekuta inauzwa 40,000.

Masks za 500-1000 leo zinauzwa tsh 3000-4000. Tumefika huko.kufa kufaa a. Kwa wenzetu hizo wangeweza hata kugawa bure au kuuza kwa bei ya chini zaidi. Sisi tunawekeza kwenye siasa zaidi na si kwenye sayansi na watu.

Tupo tayari kurudia uchaguzi na kutumia pesa kushawishi mwanasiasa lakini si kumwendeleza daktari au mgunduzi wa jambo la manufaa kwa umma.

Ukicheka na nyani utavuna mabua.
 
Nani aliye kwambia mask wanagawa bure, kwa wenzetu, zinanunuliwa tena moja sh elfu 3 hadi 4000 hata China hizo ndio bei zake.
 
Back
Top Bottom