Corona: Meneja wa Diamond na Mwana FA watangaza kuugua Corona baada ya kupimwa

Viol

JF-Expert Member
Dec 15, 2009
25,426
18,228
Mwanamuzi Khamis Mwinjuma maarufu kama MwanaFA amekutwa na maambukizi ya Virusi vya Corona. Kupitia akaunti yake ya Instagram, amepakia video na kuweka ujumbe unaosema

Majibu ya vipimo vyangu vya Covid 19 yamerudi chanya. Inaudhi. Siumwi KABISA. Nipo sawa 100%. Na nimejitenga toka niliporudi ili kuepuka kuathiri wengine. Na kwa bahati hata watoto wangu sijakutana nao kabisa. Hawapo nyumbani.

Nawaomba tu tuchukue tahadhari kwa kadri ya uwezo wetu kukwepa usitupate na hata tukipatwa nao sio tatizo la kivile hata,virusi wake wanaondoka wenyewe baada ya siku kadhaa tu. So yah,sisi wa nchi hizi tulioandamwa na migonjwa mikubwa mikubwa katika kukua kwetu,haya ‘mafua’ wala sio kitu cha kututisha. ITAKUWA TU SAWA. Tuweni na amani tu mioyoni.





































=====

Manager wa Diaomond Platnumz ametangaza kuwa amepata maambukizi ya virusi vya Corona na yupo kwenye uangalizi mzuri.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Salam ameandika:

HABARI...!! Napenda kuwajulisha na kuwatoa hofu ndugu, jamaa na marafiki kuwa nimepata majibu ya vipimo na nimeonekana nikiwa na Corona Virus, kwa sasa nipo chini ya uwangalizi mzuri na afya yangu inaendelea vizuri, pia niishukuru serikali kwa maandalizi mazuri na huduma nayopata wodini, Kwenye kituo toka juzi nipo peke yangu kama nimekikodisha vile 😅, wahudumu wanaushirikiano mzuri Mungu awalinde na awape afya njema maana wamejitolea nafasi zao kutupatia huduma sisi waathirika, hili janga la kimataifa linakwepeka kama tutafuata ushauri nasaha kutoka kwenye Wizara husika, naomba kwa wote tuwe salama na familia zetu, tuchukue tahadhari mapema. Be Strong and Be Safe Everyone out there #AllahBlessUsAll

2342353_Salam.jpg

Meneja wa Diaomond Patnumz, Salam SK
 
Duh! Wagonjwa hadi wanatype wodini what the https://jamii.app/JFUserGuide is corona?

Huu sasa ujinga ona sasa nachoma 70k kurudi nyumbani kisa chuo kufungwa wakati wagonjwa wanapiga simu na kusema wanaendelea vizuri.


Aaah
 
Back
Top Bottom