Corona; Mapambano dhidi ya gonjwa hili, "retreat is no surrender"

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,822
35,817
Mabibi na mabwana nimemsikiliza Dr. Mpango na ushuhuda wake.

Mtu nzima, mtu mzito, kigogo na waziri wa serikali hii machozi yamemdondoka.

Pamekuwa na ngonjera nyingi kuhusu gonjwa hili:

1. Mara WHO ni nani?
2. Mara tunafuata melekezo ya WHO.
3. Mara tuachakata takwimu.
4. Mara ni vita vya kiuchumi ambavyo adui ameshindikana kutambulishwa kwetu.
5. Mara maombi, nyungu, dawa za ki Madagascar vitatuvusha.
6. Mara barakoa za nje zinaleta Corona.
7. Mara hatuna Corona.
8.Mara si kila kifo ni Corona huku hakuna anayeweka wazi kama vya Corona havipo.
9. Mara kuchukua tahadhari haijakatazwa ila kama shambani kwa bibi kila mtu na lake.
10. Mara kwani zamani watu walikuwa hawafi, wakati ni kweli kuwa zamani watu walikuwa hawafi kwa Corona.
11. nk nk.

Jamani eeh ukweli mchungu Dr. Mpango hakuwahi kupitiwa na kikombe kama hiki. Si Dr. Mpango pekee bali kote hata walikofikia kuweza hatua kali kabisa kuhusiana na ugonjwa huu zikiwamo kuwafungia watu majumbani.

Katika kutapatapa kote huku kitu kimoja ni dhahiri. Watu wanaendelea kufa na hali yetu inazidi kuwa mbaya zaidi.

Lockdown si fashion. Kuchukua hatua kali kabisa kama hiyo ya kuhami maisha si fashion bali uwepo wa ulazima wa kufanya maamuzi magumu kweri kweri.

Tutakuwa tusiojielewa tukidhani waliofika kuweka ma lockdown ni kwa sababu ya ujinga au kupenda kwao tu.

Haina maana yoyote kuendelea na uelekeo ambao haulipi. Uelekeo usio na tija. Uelekeo ambao leo ni Dr. Mpango kesho waziri, kigogo, au mlalahoi fulani nk pasipo na kuchukua hatua yoyote.

Ni wazi kuwa kwa mwendelezo kama huu wengi waliomo na wasiokuwamo tuko njia moja. Ni suala la muda tu.

Kiungwana tu: "Retreat is no surrender." Wanasema pia, "kuteleza si kuanguka."

Kufikiria ku reboot au hata kuchomoa betri mbona nayo ni sehemu ya mchezo?

Eeh mola wetu hebu uwajalie viongozi wetu kutambua kuwa wanayo dhamana kwa maisha ya watu wao ambayo hayawezi kuikwepa.

Kwamba maisha yote ya wakubwa na wadogo, wenye vyeo na hohehahe, masikini na Matajiri, wasukuma na wachaga nk yanapaswa kulindwa kwa gharama yoyote.

Kwamba maisha ni bora mno kuliko Mali, vyeo, miradi nk.

Kwamba "wa kufa na afe. Wa kuishi na aishi' ni sera machukizo mno kwako.

Ninawasilisha.
 
Lockdown hapana, ila kuna mikusanyiko mingi isiyo ya muhimu inayoweza kuzuiwa pamoja na amri ya watu wote kuvaa barakoa, level seats, ventilators ziwepo, na mengineyo
 
Lockdown hapana, ila kuna mikusanyiko mingi isiyo ya muhimu inayoweza kuzuiwa pamoja na amri ya watu wote kuvaa barakoa, level seats, ventilators ziwepo, na mengineyo

Lockdown unaisoma wapi mkuu?

Wa kufa na wafe wa kuishi na waishi kwamba tumemwachia Mungu. Hiyo ni aera machukizo kwa Mungu.

Hatua zote zinatakiwa kufanywa kuyalinda maisha yote.

Kwanini wasiachiwe wataalamu wa afya kutuongpza mwelekeo sahihi? Wanasiasa na wachumia matumbo wakakaa pembeni?
 
Israel na Saudi wanawwpa chanjo za Corona raia wao huku wakimwomba Mwenyezi Mungu awanusulu na balaa la maambukixi, wakati huku uswekeni kwetu full majanga, yaani ni mwendo wa nyungu na tangawizi.
 
Israel na Saudi wanawwpa chanjo za Corona raia wao huku wakimwomva Mwenyezi Mungu awanusulu na balaa la maambukixi, wakati huku uswekeni kwetu full majanga, yaani ni mwendo wa nyungu na tangawizi.....

Kuna mijamaa sasa hivi imeaminishwa siku moja ina masaa 48. Imeamini na huiambii kitu:

IMG_20210218_174254_207.jpg
 
Kuna mijamaa sasa hivi imeaminishwa siku moja ina masaa 48. Imeamini na huiambii kitu:

View attachment 1711120
Wewe ndo wakala wa Corona kwenye hii nchi.
Kila ukiamka wewe ni corona corona!!

Tumeisha sema huu ugonjwa tutapambana nao kwa namna tunayoona ina faa kwetu sio kwao.
Hao waliowatuma mpaka sasa bado wanakufa.
 
Wewe ndo wakala wa Corona kwenye hii nchi.
Kila ukiamka wewe ni corona corona!!

Tumeisha sema huu ugonjwa tutapambana nao kwa namna tunayoona ina faa kwetu sio kwao.
Hao waliowatuma mpaka sasa bado wanakufa.

Mmeishasema wewe na nani jombi?

Au wenzio ni hawa hapa?
IMG_20210218_174254_207.jpg
 
Back
Top Bottom