Trubarg
JF-Expert Member
- Jan 8, 2020
- 4,253
- 6,889
Sanitizer huwekwa michanganyiko mbalimbali ikiwemo marashi, rangi n.k. Component muhimu inayoua vijidudu Ni alcohol au ethanol. Kiwango Cha alcohol kinachoweza kuua vijidudu kwa ukamilifu Ni kuanzia asilimia sabini (70% vol aclohol). Kwa hiyo unapoenda kununua sanitizer Cha muhimu kuangalia ni kiwango Cha alcohol na si rangi Wala harufu (marashi) Wala Bei.
MAMBO YA KUZINGATIA KUHUSU SANITIZER
1. Sanitizer haifanyi kazi kwenye uchafu. Hakikisha unanawa mikono yako au kuosha sehemu unayotaka kusanitize na uikaushe kabla ya kuweka sanitizer.
2.Kama unatumia kwenye mikono hakikisha unaisugua kwa muda wa sekunde ishirini ili kuifanya ipenye vizuri kwenye viganja vyako.
3. Konyagi/ kvant/Kitoko haitoshi kusanitize mikono yako kwani kiwango chake Cha alcohol/ ethanol hakifiki asilimia 70. Nyingi Ni chini ya asilimia 40.
4. Sanitizer pekee haitoshi kuondoa virusi,kunawa mikono kwa sabuni na maji ya kutosha kunaweza kukusaidia kukuokoa wewe na familia yako.