Corona: Kwa mazingira ya sasa, "Waliokufa au kuugua hawakupenda, hawakuchagua wala si makosa yao"

Kwani nani kasema mikusanyiko imeanza leo?

Wizi haujaanza leo, je, tukatae kuwashitaki na kuwafunga wezi kwa sababu wizi ni kitu cha kawaida hakijaanza leo?

Mauaji hayajaanza leo, je, tukatae kuwashitaki na kuwafunga wauaji kwa sababu mauaji hayajaanza leo?
Hujanielewa,hoja yangu si ubaya au uzuri wa hilo jambo bali hoja yangu ni kwamba hilo jambo ni la muda mrefu hivyo si la kushangaa.
Ni sawa na kusikia matukio ya Bokoharam huko Nigeria,si mazuri ila huwa si ya kutushangaza maana tushazoea kusikia matukio yao.
 
Kuna mechi ya soka ya CAF timu ya South Africa (Mamelodi Sundowns) na timu ya Algeria, North Africa (CR Belouizdad) inakuja kufanyika Tanzania Jumapili ya February 28 2021.

Wote wameogopa kuongeza maambukizi ya Covid-19 kwao, sisi ndio tumeoneka wajinga tumeletewa mechi.
Daladala nazo ni shida
 
Hujanielewa,hoja yangu si ubaya au uzuri wa hilo jambo bali hoja yangu ni kwamba hilo jambo ni la muda mrefu hivyo si la kushangaa.
Ni sawa na kusikia matukio ya Bokoharam huko Nigeria,si mazuri ila huwa si ya kutushangaza maana tushazoea kusikia matukio yao.
Kwani jambo likiwa linajulikana lipo muda mrefu maana yake ni lazima liwe halishangazi?
 
Magufuli yupo Sahihi sana.kumtegemea MUNGU na muda si mrefu matokeo yataonekana .hatuna wasiwasi tutashinda

Wewe uko karibu yake kuliko hawa?

IMG_20210222_160917_282.jpg


Uliwahi kumsikia Albert Einstein kulinganisha na kinachoendelea hapa?

Uliwahi kuisikia Murphy's law?

Au ni kubwa bwaja kwenu kwa kawaida kuwa mko vizuri majini tu?
 
Kwani jambo likiwa linajulikana lipo muda mrefu maana yake ni kazima liwe halishangazi?
Kitu kikiwa kinajulikana muda mrefu kitazoeleka na kikizoeleka hakitashangaza tena huwezi kushangaa ulichozoea,siwezi kumshangaa Sheikh wa mkoa kuvaa kanzu wakati muda wote nikimuona namuona kavaa kanzu.
 
Kitu kikiwa kinajulikana muda mrefu kitazoeleka na kikizoeleka hakitashangaza tena huwezi kushangaa ulichozoea,siwezi kumshangaa Sheikh wa mkoa kuvaa kanzu wakati muda wote nikimuona namuona kavaa kanzu.
Mpemba effect, jambo la kisayansi lililoonesha maji yenye joto kuganda na kuwa barafu kwa haraka zaidi kuliko maji ya baridi, lilijulikana tangu enzi za Aristotle.

Erasto Mpemba, kijana mdogo Mtanzania aliyekuwa anasoma shule ya msingi miaka ya 1960s, akaliibua tena jambo hili kutokana na mazoezi ya darasani.

Likabaki kuwa kitendawili jinsi linqvyotokea kwa miaka mingi sana, licha ya kujulikana kuwapo.

Kitu kinaweza kujulikana kuwapo, lakini sababu za kuwapo zikawa tabu kuzielewa na hivyo likashangaza licha ya kujulikana
 
Mpemba effect, jambo la kisayansi lililoonesha maji yenye joto kuganda na kuwa barafu kwa haraka zaidi kuliko maji ya baridi, lilijulikana tangu enzi za Aristotle.

Erasto Mpemba, kijana mdogo Mtanzania aliyekuwa anasoma shule ya msingi miaka ya 1960s, akaliibua tena jambo hili kutokana na mazoezi ya darasani.

Likabaki kuwa kitendawili jinsi linqvyotokea kwa miaka mingi sana, licha ya kujulikana kuwapo.

Kitu kinaweza kujulikana kuwapo, lakini sababu za kuwapo zikawa tabu kuzielewa na hivyo likashangaza licha ya kujulikana
Issue sio kujulikana au kufahamika bali kuzoeleka,huwezi kushangaa ulichokizoea.
 
brazaj matatizo yako ni makubwa kuliko corona yenyewe. Wewe sonona naona itakuondoa Kama mtanzania mwenzangu naomba nikushauri "sio kila vita lazima upigane" Yes humpendi Magufuli lakini ndio Rais, bahati mbaya sana watanzania wengi wanampenda na wanamuamini hayo ni muhimu kufahamu na kuelewa kwa afya ya akili yako
Watanzania wengi, hapo ndipo uliponiacha mkuu
 
Watu wanajua kuwa corona ipo ila kutokuvaa barakoa ni uwamuzi wao na si kwamba hawajui kuwa kuna corona,ila watu mnashindwa kuelewa kuwa hata hiyo mwaka jana ambako serikali ilitangaza kuwepo corona na hadi kuwa inatangaza vifo vya corona hakukuwa na uzingatiaji wa kihivyo wa kujikinga na corona kikubwa kilichokuwepo wakati huo ni hofu kubwa kuliko uzingatiaji wa kujikinga na corona.

Hata leo kuna watu wanakubali kuwa corona ipo na ya sasa hivi ni hatari ila bado havai Barakoa wala kuchukua tahadhari zozote.
Jiwe kasema hakuna corona, je unapingana naye?
 
Allah Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote, watu wasingehitaji kumuomba, ulimwengu wake ungekuwa hauna magonjwa angewapa watu neema zake kabla hawajamuomba.

Ukweli kwamba tunaishi kwenye ulimwengu wenye ma pandemic unaonesha huyo Allah hayupo.
qsn: sio kila kinachotokea mwenyewe hayupo; fikiria mtihani na alietunga ntihani
Tunapomuomba tunajifariji wenyewe tu.
qns: sio kweli; faraja inatoka kwa alieombwa; wewe hujamuomba na ni mangapi unaomba kwa binadamu na yanakupa faraja? ashindwe kwako
Ndiyo maana watu wanaomba sana, halafu wanakufa sana pia.
qns: hiyo ni kanuni yake Allah; kwani wewe kila unachoomba unakipata? lakini unakidhi haja chooni!
Huyo Allah mwingi wa neema ni mkatili hivi asiwasikie waja wake?
qns: kwani ukiwa na watoto wako kisha wakakuomba katika mahitaji yao na ukashindwa kuwapa kwa sababu yeyote ile je? umekuwa katili.
Kwa nini kaumba ulimwengu unaoweza kuwa na magonjwa, wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu usioweza kuwa na magonjwa?
qns: boss umejitahidi kutumia akili za kifalsafa ambazo zina ukomo wa ubongo; hivi ni kweli kila anayetengeneza gari au kifaa amekifanya kikamilifu? au amekifanya kihitajie moja kwa kingine. ni hivyo hivyo wewe amekuumba ukiwa si mkamilifu kwanini usijibadilishe hayo maradhi yasikufike wala kukudhuru?
 
Mimi sielewi kwa nini mpaka leo watu wanajazana kwenye mpira na matamasha ya muziki.

Kuna mechi ya soka ya CAF timu ya South Africa (Mamelodi Sundowns) na timu ya Algeria, North Africa (CR Belouizdad) inakuja kufanyika Tanzania Jumapili ya February 28 2021.

Wote wameogopa kuongeza maambukizi ya Covid-19 kwao, sisi ndio tumeoneka wajinga tumeletewa mechi.

Na sisi kama mazuzu tumekubali. Na watu watajazana uwanjani.

Hao watakaojazana uwanjani, wakipata Covid-19 na kufa, utasema wamekufa bila kutaka?
Wajinga waliwao,wabongo wanapenda kuchukulia mambo kawaida tu
Asiyesikia achana naye yakatayo mkuta acha yamkute
Ila ugonjwa huu utawachukua wengi ambao afya yao mgogoro acha kila mtu apambane na hali yake

Ova
 
Kama nilivyosema.

Wengi hatuthamini uhai.

Na wewe kusema "kawaida tu" maana yake unaona watu kufa kwa wingi kutokana na mambo yanayoweza kuzuilika ni "kawaida tu".
Wabongo hatuthamini uhai ila achana nao
Akataye vuta acha avute tu kwanza sahv mtu
Akivuta wengine tunaishiaa kutoa pole tu kwa sms na unarusha mchango kama ikibidi
Kwenda kuzika hatuendi

Ova
 
Mabibi na mabwana kama ilivyo katika somo hapo juu, huo ndiyo ulio ukweli mchungu. Kwamba tupo hapa leo, kimungu mungu tu. Kweri?

No! It shouldn't be!

Anasema Prof. Bisanda, heshima kwake:

"Watanzania wengi wanadhani ugonjwa huu utawapata wengine, wasitambue kuwa hata pale wanapopata maambukizi, huwa wamekuwa wazembe kujilinda."


Ninaamini aliyasema hayo akizingatia hali yetu halisi leo (hapa nchini) kuhusiana na ugonjwa huu.

Ni aibu kubwa kuwa hata wengi wa wenye kujitambua kama Profesa huyu, wameamua kuuchuna kwa tamaa na njaa tu za matumbo yao. Kwao ni heri kufa huku wakiwa wameshiba matumboni, kuliko kuishi huku ikiwalazima kula kwa majasho yao.

Wamepotea wapendwa wetu wengi. Wapi walipokosea wao? Wapi tulipopatia sisi? Wapi tulipokosea ambapo labda tumeshaparekebisha kiasi sasa tuko salama zaidi kuliko ilivyo kuwa hapo kabla?

Wamepotea vigogo na wazito wenye majina na vyeo vikubwa vikubwa, sembuse akina yakhe?

Murphy's law inasema: "If anything can go wrong, it will go wrong."

Kwa maana kwamba kama mambo yanaweza kwenda mrama, basi ndani ya mazingira yale yale ni suala la muda tu kwani yatakwenda tena mrama!

Hivi hata katika mkuluro wa vifo vinayotukumba, kitu gani tumefanya ili tusiendelee kukumbwa navyo?

Tunaogelea mle mle na ngonjera zile zile za masaa 48 kwa siku. Barakoa za kuzuia mate, pongezi kwa wasiovaa barakoa. kejeli kwa waliovaa barakoa.

Ukweli mchungu, kwa hali hii, tayari kwa leo tumeshawatakia wapendwa wetu kupumzika kwa amani. Kesho kama si sisi wapo tena watakaofuata kwa janga hili hili kama ambavyo wengine bado wataendelea kutangulia hadi hapo 23:59.

Anasema Albert Einstein kuwa:

"Insanity is doing the same thing over and over again, expecting to get different results."

Kwa tunayoyafanya:


Ugonjwa huu utapiga hodi sana na kila mahala. Leo kwao, kesho kwangu, kesho kutwa kwako, nk nk.

Itambulike kuwa kutofautiana na mtukufu rais kwenye jambo lolote, achilia mbali kwenye jambo muhimu lenye nia ya kuwahami watu kama hili si dhambi wala uhaini.

Ninachelea kuwaalika ma pro life wote, ikiwapendeza Sirro na Mambosasa nao wakiwamo, pia wewe, yule na mimi tukutane Tahrir square katika siku muafaka kwa ajili ya kupiga kelele.

Obviously, the status quo is not an option!

United we stand.

Ninawasilisha.
Jiwe kapata chanjo ya wachina juzi. Si wa kusikiliza huyu muuaji
 
Back
Top Bottom