Corona: Kwa mazingira ya sasa, "Waliokufa au kuugua hawakupenda, hawakuchagua wala si makosa yao"

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,823
35,828
Mabibi na mabwana kama ilivyo katika somo hapo juu, huo ndiyo ulio ukweli mchungu. Kwamba tupo hapa leo, kimungu mungu tu. Kweri?

No! It shouldn't be!

Anasema Prof. Bisanda, heshima kwake:

"Watanzania wengi wanadhani ugonjwa huu utawapata wengine, wasitambue kuwa hata pale wanapopata maambukizi, huwa wamekuwa wazembe kujilinda."

Ninaamini aliyasema hayo akizingatia hali yetu halisi leo (hapa nchini) kuhusiana na ugonjwa huu.

Ni aibu kubwa kuwa hata wengi wa wenye kujitambua kama Profesa huyu, wameamua kuuchuna kwa tamaa na njaa tu za matumbo yao. Kwao ni heri kufa huku wakiwa wameshiba matumboni, kuliko kuishi huku ikiwalazima kula kwa majasho yao.

Wamepotea wapendwa wetu wengi. Wapi walipokosea wao? Wapi tulipopatia sisi? Wapi tulipokosea ambapo labda tumeshaparekebisha kiasi sasa tuko salama zaidi kuliko ilivyo kuwa hapo kabla?

Wamepotea vigogo na wazito wenye majina na vyeo vikubwa vikubwa, sembuse akina yakhe?

Murphy's law inasema: "If anything can go wrong, it will go wrong."

Kwa maana kwamba kama mambo yanaweza kwenda mrama, basi ndani ya mazingira yale yale ni suala la muda tu kwani yatakwenda tena mrama!

Hivi hata katika mkuluro wa vifo vinayotukumba, kitu gani tumefanya ili tusiendelee kukumbwa navyo?

Tunaogelea mle mle na ngonjera zile zile za masaa 48 kwa siku. Barakoa za kuzuia mate, pongezi kwa wasiovaa barakoa. kejeli kwa waliovaa barakoa.

Ukweli mchungu, kwa hali hii, tayari kwa leo tumeshawatakia wapendwa wetu kupumzika kwa amani. Kesho kama si sisi wapo tena watakaofuata kwa janga hili hili kama ambavyo wengine bado wataendelea kutangulia hadi hapo 23:59.

Anasema Albert Einstein kuwa:

"Insanity is doing the same thing over and over again, expecting to get different results."

Kwa tunayoyafanya:

Ugonjwa huu utapiga hodi sana na kila mahala. Leo kwao, kesho kwangu, kesho kutwa kwako, nk nk.

Itambulike kuwa kutofautiana na mtukufu rais kwenye jambo lolote, achilia mbali kwenye jambo muhimu lenye nia ya kuwahami watu kama hili si dhambi wala uhaini.

Ninachelea kuwaalika ma pro life wote, ikiwapendeza Sirro na Mambosasa nao wakiwamo, pia wewe, yule na mimi tukutane Tahrir square katika siku muafaka kwa ajili ya kupiga kelele.

Obviously, the status quo is not an option!

United we stand.

Ninawasilisha.
 
Mimi sielewi kwa nini mpaka leo watu wanajazana kwenye mpira na matamasha ya muziki.

Kuna mechi ya soka ya CAF timu ya South Africa (Mamelodi Sundowns) na timu ya Algeria, North Africa (CR Belouizdad) inakuja kufanyika Tanzania Jumapili ya February 28 2021.

Wote wameogopa kuongeza maambukizi ya Covid-19 kwao, sisi ndio tumeoneka wajinga tumeletewa mechi.

Na sisi kama mazuzu tumekubali. Na watu watajazana uwanjani.

Hao watakaojazana uwanjani, wakipata Covid-19 na kufa, utasema wamekufa bila kutaka?
 
Tusichoke kupaza sauti. Tatizo kubwa ni elimu.

Wanapopongezwa hadharani wasiovaa barakoa na kuwakebehi hadharani wale waliovaa barakoa, inapeleka taswira kinzani hasa kwa wasio elewa.

Nani ajuaye sauti zetu hata kama ni ndogo zinaweza kuokoa nafsi ngapi.

Alisikika msemaji wa Simba SC kwenye mechi zao walizohusianisha na timu za Sudan na TP Mazembe:

"Tukaujaze uwanja ili tuionyeshe dunia kuwa sisi Tanzania hatuna Corona"

Hii ndiyo Tanzania ya leo. Hapa ndipo tulipo.

Unbelievable!
 
Hatari sana.

Ni kama nchi haijali uhai inafanya utani kwenye suala la life or death.
 
Wameondoka vingunge kwenye nafasi zao.

IMG_20210220_190747_757.jpg

Wengine wanakodolea macho nafasi hizo za nini? Kwani hata zina usalama gani katika mazingira ya sasa?

Angalia hawa:

Kweli tuko vizuri:

IMG_20210218_174254_207.jpg
 
Mimi sielewi kwa nini mpaka leo watu wanajazana kwenye mpira na matamasha ya muziki.

Kuna mechi ya soka ya CAF timu ya South Africa (Mamelodi Sundowns) na timu ya Algeria, North Africa (CR Belouizdad) inakuja kufanyika Tanzania Jumapili ya February 28 2021.

Wote wameogopa kuongeza maambukizi ya Covid-19 kwao, sisi ndio tumeoneka wajinga tumeletewa mechi.

Na sisi kama mazuzu tumekubali. Na watu watajazana uwanjani.

Hao watakaojazana uwanjani, wakipata Covid-19 na kufa, utasema wamekufa bila kutaka?
kwani utaenda mpirani jamaa angu!!!
 
brazaj matatizo yako ni makubwa kuliko corona yenyewe. Wewe sonona naona itakuondoa Kama mtanzania mwenzangu naomba nikushauri "sio kila vita lazima upigane" Yes humpendi Magufuli lakini ndio Rais, bahati mbaya sana watanzania wengi wanampenda na wanamuamini hayo ni muhimu kufahamu na kuelewa kwa afya ya akili yako
 
Kumbe unajua kuna kuumwa?
Mimi nikajua hauamini hata kuumwa
Mimi sielewi kwa nini mpaka leo watu wanajazana kwenye mpira na matamasha ya muziki.

Kuna mechi ya soka ya CAF timu ya South Africa (Mamelodi Sundowns) na timu ya Algeria, North Africa (CR Belouizdad) inakuja kufanyika Tanzania Jumapili ya February 28 2021.

Wote wameogopa kuongeza maambukizi ya Covid-19 kwao, sisi ndio tumeoneka wajinga tumeletewa mechi.

Na sisi kama mazuzu tumekubali. Na watu watajazana uwanjani.

Hao watakaojazana uwanjani, wakipata Covid-19 na kufa, utasema wamekufa bila kutaka?
 
Watu wanachukulia poa ,watu still wanajua hakuna korona kwahiyo wanajiachia sana,kwenye madaladala watu wamejazana halaf hawana barakoa!! Ipigwe marufuku kwenda kwenye mikusanyiko bila barakoa na kupanda daladala bila barakoa...Wafnyabiashara waweke bdoo za kunawia,shule wanafunzi wawe na barakoa.
 
Kawaida tu maana toka mwaka jana tulikuwa tunajazana kwenye mikutano ya kampeni na kushindanisha nyomi kati ya Lissu na Magufuli,wakati huo wenzetu bado wanaendelea na mapambano ya corona kupunguza maambukizi kwa kuepusha mikusanyiko.
 
Watu wanajua kuwa corona ipo ila kutokuvaa barakoa ni uwamuzi wao na si kwamba hawajui kuwa kuna corona,ila watu mnashindwa kuelewa kuwa hata hiyo mwaka jana ambako serikali ilitangaza kuwepo corona na hadi kuwa inatangaza vifo vya corona hakukuwa na uzingatiaji wa kihivyo wa kujikinga na corona kikubwa kilichokuwepo wakati huo ni hofu kubwa kuliko uzingatiaji wa kujikinga na corona.

Hata leo kuna watu wanakubali kuwa corona ipo na ya sasa hivi ni hatari ila bado havai Barakoa wala kuchukua tahadhari zozote.
 
Kawaida tu maana toka mwaka jana tulikuwa tunajazana kwenye mikutano ya kampeni na kushindanisha nyomi kati ya Lissu na Magufuli,wakati huo wenzetu bado wanaendelea na mapambano ya corona kupunguza maambukizi kwa kuepusha mikusanyiko.
Kama nilivyosema.

Wengi hatuthamini uhai.

Na wewe kusema "kawaida tu" maana yake unaona watu kufa kwa wingi kutokana na mambo yanayoweza kuzuilika ni "kawaida tu".
 
Hii Vita mafanikio yetu yatakuwa kwa ugumu kwa sababu Rais, ambaye ndiye kiongozi mkuu ndiye pia ni kipingamizi katika jitihada zetu.

Hiki kizingiti, kwa nafasi aliyo nayo, athari yake ni kubwa sana. Tuendelee kumpigia kelele, na kumfikishia ujumbe bila woga na bila ya unafiki. Ikilazimu, iwe yeye au wasaidizi wake wakitoa kauli tata au zinazolenga kuwapumbaza watu, watu wazomee dhidi ya kauli yake. Siyo kosa, na siyo dhambi.
 
Pamoja na kuwa uhai ni kitu cha thamani ila pia ndio kitu ambacho tunakipoteza mamia kwa maelfu kila siku iwe kwa uzembe ama si kwa uzembe,watu hapa wanazungumzia vifo vya corona ila wanajua kuna vifo vyengine vya maradhi mengine na vifo vyenye kusababishwa na sababu zengine pia vinaendelea kutokea kwa wingi tu ila watu kutofungulia nyuzi humu kuvizungumzia haina maana hawathamini uhai.

Hoja yangu hii mikusanyiko sasa hivi iwe ya mechi za mpira au vyovyote ni kwamba haijaanza leo ni tokea mwaka jana na ndio maana nikasema ni kawaida na si kwamba sithamini uhai.
 
Nina mpango wa kumtaarifu rasmi kuwa ninatoka karantini niliko jilockdown. Nizunguke nchi nzima na counter book langu nikusanye sahihi 5,000,000/= kumtaarifu kuwa tupo wengi ambao hatukubaliani naye kwenye hili.

Huyu si wa kuacha hivi hivi.
 
Kilichomuhimu ni watu kuchukua tahadhari; wakati tunaomba msaada kwa Allah huku tukikoma na kuacha madhambi yanayomuudhi mola wetu
 
Pamoja na kuwa uhai ni kitu cha thamani ila pia ndio kitu ambacho tunakipoteza mamia kwa maelfu kila siku iwe kwa uzembe ama si kwa uzembe,watu hapa wanazungumzia vifo vya corona ila wanajua kuna vifo vyengine vya maradhi mengine na vifo vyenye kusababishwa na sababu zengine pia vinaendelea kutokea kwa wingi tu ila watu kutofungulia nyuzi humu kuvizungumzia haina maana hawathamini uhai.

Hoja yangu hii mikusanyiko sasa hivi iwe ya mechi za mpira au vyovyote ni kwamba haijaanza leo ni tokea mwaka jana na ndio maana nikasema ni kawaida na si kwamba sithamini uhai.
Kwani nani kasema mikusanyiko imeanza leo?

Wizi haujaanza leo, je, tukatae kuwashitaki na kuwafunga wezi kwa sababu wizi ni kitu cha kawaida hakijaanza leo?

Mauaji hayajaanza leo, je, tukatae kuwashitaki na kuwafunga wauaji kwa sababu mauaji hayajaanza leo?
 
Kilichomuhimu ni watu kuchukua tahadhari; wakati tunaomba msaada kwa Allah huku tukikoma na kuacha madhambi yanayomuudhi mola wetu
Allah Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote, watu wasingehitaji kumuomba, ulimwengu wake ungekuwa hauna magonjwa angewapa watu neema zake kabla hawajamuomba.

Ukweli kwamba tunaishi kwenye ulimwengu wenye ma pandemic unaonesha huyo Allah hayupo.

Tunapomuomba tunajifariji wenyewe tu.

Ndiyo maana watu wanaomba sana, halafu wanakufa sana pia.

Huyo Allah mwingi wa neema ni mkatili hivi asiwasikie waja wake?

Kwa nini kaumba ulimwengu unaoweza kuwa na magonjwa, wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu usioweza kuwa na magonjwa?
 
Back
Top Bottom