Corona: Japo ni janga, pia ni fursa. Tanzania bado hakuna maambukizi, tupunguze panic, tuongeze Elimu. WB kumwaga mihela, tuchangamkie fursa

Rejea za Mandiko ya The Same Author Kuhusu Janga la Corona
  1. Mtu kama huyu ni binadamu au shetani? Anaombeaje Corona ifike Tanzania. Kuiombea nchi yako majanga, sio zaidi ya uendawazimu? Huu sio ushetani? - JamiiForums
  2. Corona: Japo ni janga, pia ni fursa. Tanzania bado hakuna maambukizi, tupunguze panic, tuongeze Elimu. WB kumwaga mihela, tuchangamkie fursa - JamiiForums
  3. Corona inatufundisha Tanzania tuna tatizo kuchanganya siasa na professionalism. Hongera Prof. Janabi kwa elimu uliyotoa, so far you are the best! - JamiiForums
  4. RC Makonda, Dar ni jiji la wote, vyama vyote. Mbowe sio mwanasiasa uchwara aliyefilisika, Zitto sio mshirikina. Tunakupenda, heshimu wote uheshimiwe - JamiiForums
  5. Je, ni kweli kuna Waziri anaugua Corona inafanywa Siri? Tunaficha nini? Hala hala kisa cha mficha maradhi! Truth & Transparency the only way out! - JamiiForums
  6. Star TV: Msemaji Mkuu wa Serekali, Dr. Hassan Abbas, azungumzia wajibu wa vyombo vya habari kuripoti janga la Corona - JamiiForums
  7. Ama kweli nabii hakubaliki nyumbani!. Je Magufuli ni nabii? Tanzania wanambeza, Afrika wanamlilia! Tanzania yapigiwa mfano Magufuli awe Rais wa Afrika - JamiiForums
  8. Vita Janga la Corona: Msemaji Mkuu wa Serikali, Dr. Hassan Abbas, Naibu Waziri wa Afya, Dr. Faustine Ndungulile, kesho watakuwa live JLNH-Star TV - JamiiForums
  9. Star TV: Msemaji Mkuu wa Serikali, Dr. Hassan Abbas na Naibu Wazuri wa Afya Dr. Faustine Ndungulile, Wanazungumzia Corona - JamiiForums
  10. Mungu ni Omnipresent. Kufuatia Local Transmission ya Corona. Je, Sasa Tushinikize Watu Wasalie Majumbani Mwao, ila Sadaka Ndio Itumwe Kwa M-Pesa? - JamiiForums
  11. Nabii Malisa: Mungu ameniambia Corona ni April tu, May hakuna Corona na hakuna atakayekufa!. - JamiiForums
  12. Kwa Kasi Sasa, Jee Tuendelee Ushujaa wa Ka-Corona, Tusitishane, Tuchape Kazi Tukiteketea, Au Sasa Tubadili Msimamo Tusitisishe Mikusanyiko Tuokoke? - JamiiForums
  13. TBC - Mjadala wa Role of The Media kwenye mapambano ya Corona, Je, Media Inatimiza Wajibu Wake Ipasavyo? - JamiiForums
  14. Live on Star TV: Corona Kushika Kasi Ndio Habari Kubwa Tanzania, Jee Media ya Tanzania, Inatimiza Wajibu Wake Ipasavyo? - JamiiForums
  15. Corona: Tusinyoosheane vidole. Kama unaweza kusaidia, please do. Usisubiri uombwe - jitokeze saidia, vinginevyo nyamaza! - JamiiForums
P
 
Nilikushangaa zaidi uliposema Corona ni fursa. High IQ hupimwa kwa uwezo wako wa kuiona kesho.

Hivi unaionaje hali ya Covid 19 wiki 1, 2 au mwezi mmoja ujao? Majibu ya swali hilo yanatenganisha watu katika makundi mawili, high IQ na low IQ.

Wengine toka mwanzo tuliiona Covid 19 ni janga. Rais Magufuli, Makonda na wewe Pascal, mliiona Covid 19 ni fursa. Nadhani mpaka sasa mnaona ujio wa Covid 19 ni fursa.

Uhalisia utatenganisha, nani katika haya makundi mawili ni low na high IQ.
 
Nnakumbuka kipindi kile Mmarekani alipoibukia kiuchumi wakati nchi zingine zikipambana, sasa hivi nchi nyingi wanajifungia ndani, uzalishaji unapungua, sisi kama watanzania tuliopewa hii neema, angalau Covid-19 haijasambaa, ingekuwa fursa kwetu, kuangalia hawa watu waliojifungia huko ndani katika nchi zao, watakutana na hali ngumu mtaani hasa katika chakula.

Mvua bado zipo, tungelima sana sasa hivi, chakula kitauzika sana nje, wabongo tumelifikiria hili kweli, huu ndio wakati wetu wa kupanda kiuchumi SWOT Analysis, tukishindwa kutumia advantage ya corana basi tena.

(Ni wachache sana wananielewa) ninarudia tena ( huwezi nielewa kama unauwezo mdogo wa kufikiri)

Hivyo yaani!
Sidhani kama Uganda wamefungia wakulima ndani; ni wale wa mjini hasa KAMPALA
 
Nilikushangaa zaidi uliposema Corona ni fursa. High IQ hupimwa kwa uwezo wako wa kuiona kesho.

Hivi unaionaje hali ya Covid 19 wiki 1, 2 au mwezi mmoja ujao? Majibu ya swali hilo yanatenganisha watu katika makundi mawili, high IQ na low IQ.

Wengine toka mwanzo tuliiona Covid 19 ni janga. Rais Magufuli, Makonda na wewe Pascal, mliiona Covid 19 ni fursa. Nadhani mpaka sasa mnaona ujio wa Covid 19 ni fursa.

Uhalisia utatenganisha, nani katika haya makundi mawili ni low na high IQ.
Fuatilia Jeff Bezos wa Amazon alikuwa wapi ki uchumi kabla ya corona na yuko wapi banda ya corona halafu linganisha na alichoshauri mleta uzi.
 
Wakati Wa Hotuba,rais Magufuri alidai mashine za kupimia virusi vya Corona zimehujumiwa na mabeberu katika kutoa majibu .Sio kwamba mabeberu hawamsikii wanamsikia matokeo yake ndio haya sasa.
Mkuu Chifu Kabi, hizo fedha za IMF na WB, japo zinatajwa kama assistance, sio grants,hizo ni mkopo na zimeombwa kama mkopo, zitalipwa na riba!. Sisi kwetu rais Magufuli amegoma kukopa, amewataka mabeberu kama wana nia njema, watusamehe riba au wasitishe marejesho ya mikopo hadi janga la Corona lipite.

Hii fursa ya IMF na WB kukopa tuliisema humu jukwaani kitambo

P

Wanabodi,
Watanzania tusiishie tuu ku concentrate kwenye janga la Corona tukajisahau kabisa na kushindwa kuziangazia fursa za Corona. Janga la Corona linaandamana na fursa mbalimbali, mfano tayari Benki ya Dunia, WB na Shirika la Fedha la Kimataifa, IMF, imemwaga mihela ya kufa mtu kwa ajili ya kufidia mdororo wa kiuchumi unaosababishwa na Corona, shurti pekee kwa fedha hizi ni lazima ziombwe, na pili, hazitolewi bure kama sadaka au grants, zitatolewa kama fursa za kukopa kwa masharti nafuu na riba ndogo. Tanzania tuchangamkie fursa hizi, vinginevyo Corona itatuumiza sana kiuchumi!.
Paskali
P
 
Wanabodi,

Kuna msemo wa Kiswahili usemao "Kufa Kufaana", wakati watu wanahangaika na janga la Corona, wengine wanaangazia namna ya kutumia changamoto kuzibadili kiwa fursa, yaani turning problems, obstacles, challenges or adversaries into opportunities.
Wandugu, hapa nafanya tuu follow up ya Corona nikipitia kujikumbusha niliwahi kuandika nini au kusema nini kuhusu Corona na hiki kinacho endelea sasa. Corona is real tusifanye masihara, tujilinde kwa kufuata ushauri wa kitaalamu.

Kila Jumamosi asubuhi kuanzia saa 1:30 hadi saa 3:00 asubuhi , Star TV, huwa ninakuwa live kwenye kipindi cha TV cha Jicho Letu Ndani ya Habari ambacho huwa kinatangwa live na Star TV kila siku za Jumamosi asubuhi, kwa Jumamosi ya kesho, mgeni wetu ni Waziri wa Habari, Dr. Harrison Mwakyembe tukijadili kuhusu athari za Corona kwenye sekta ya Habari, nini kifanyike.

Ukipata nafasi karibu utufuatilie.

P
 
Wanabodi, kama nilivyoeleza hapo mwanzo, japo Corona ni janga lakini pia ni fursa, Tanzania tumechangamkia furaa, leo IMF wametoa msamaha wa madeni.

Pia tumeendelea kufanya mengi kwa kutumia mtandao badala ya physically.

Mungu Ibariki Tanzania
P
 
Fursa hizi ni za aina mbili, fursa za kimataifa kwa Tanzania kama nchi kuchangamkia fursa hii ya World Bank
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU YATOKANAYO NA RIPOTI YA KAMATI MAALUMU YA MHESHIMIWA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA KUFANYA TATHMINI YA UGONJWA WA COVID-19 NCHINI
DAR ES SALAAM 17 MEI, 2021

Ndugu wanahabari, mtakumbuka kwamba kupitia hotuba ya Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, aliyoitoa tarehe 6 Aprili, 2021 wakati akiwaapisha viongozi mbalimbali Ikulu jijini Dar es Salaam kuhusu kuunda Kamati ya kitaalamu ya kufanya tathimini ya ugonjwa wa COVID-19 na baadaye msisitizo alioutoa tarehe 22 Aprili, 2021 wakati akilihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Dodoma, naomba kuwajulisha kuwa Kamati hiyo imewasilisha rasmi ripoti yake kwa Mheshimiwa Rais leo tarehe 17 Mei, 2021.

Ndugu Wanahabari, Kamati ilifanyia kazi hadidu za rejea 12 zilizohusu maeneo mbalimbali ya tathmini ya mwenendo wa ugonjwa pamoja na afua za udhibiti wa COVID-19 ikiwemo chanjo hapa nchini, kikanda na kimataifa.
Ndugu Wanahabari, Tangu kuingia kwa ugonjwa wa COVID-19 nchini mwezi Machi 2020, Tanzania imekumbwa na mawimbi mawili makubwa na hivi sasa kutokana na mwenendo wa ugonjwa huo katika mataifa mengine duniani na kuna tishio la kutokea kwa wimbi la tatu hapa nchini.

Ndugu Wanahabari, Baada ya uchambuzi wa kina Kamati imependekeza yafuatayo:
1. Serikali ihuishe mipango ya dharura (Contigency and Response Plans) katika ngazi zote kwa ajili ya kukabiliana na majanga likiwemo janga la ugonjwa wa COVID-19.
2. Serikali itoe taarifa juu ya uwepo wa ugonjwa wa COVID-19 na ichukue hatua madhubuti kuimarisha hatua zote za afua za kinga (interventions) katika ngazi zote ili kuepusha wimbi la tatu la ugonjwa huo.
3. Wataalamu wa afya watimize wajibu wao kitaalamu, kwa kuzingatia weledi, miiko na maadili katika kuelimisha, kukinga na kutibu ugonjwa wa COVID-19 nchini.
4. Tanzania ishiriki ipasavyo katika maamuzi na itekeleze maazimio ya kikanda na kimataifa iliyoridhia katika jumuiya za EAC, SADC, AU na WHO.
5. Kuhusu chanjo dhidi ya ugonjwa wa COVID-19:
a. Kamati inashauri Serikali kwa kutumia vyombo vyake iendelee na hatua kuelekea kuruhusu matumizi huru ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa COVID-19 kwa kutumia chanjo zilizoorodheshwa na Shirika la Afya Duniani ili kuwapa fursa ya kinga wananchi wake kwa kuwa kupitia uchambuzi wa Kamati, chanjo hizo zina ufanisi na usalama unaokubalika kisayansi;
b. Pamoja na mapendekezo haya, Kamati Huru ya Kitaifa ya Ushauri wa Chanjo (NITAG) na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) ziendelee kushirikishwa katika kutoa ushauri na kudhibiti chanjo hizo;
c. Kipaumbele cha utoaji wa chanjo dhidi ya COVID-19 nchini kwa kuanzia kiwe katika makundi yafuatayo kwa umuhimu:
i. Wahudumu katika vituo vya kutolea huduma za afya na watumishi walio katika mstari wa mbele wa utoaji wa huduma (frontline workers) mathalani watumishi sekta ya utalii, hoteli, mipakani, viongozi wa dini na mahujaji;
ii. Wazee na watu wazima kuanzia umri wa miaka zaidi ya 50;
iii. Watu wazima wenye maradhi sugu mengine (comorbidities) mathalani kisukari, shinikizo la damu, maradhi ya mfumo wa upumuaji, magonjwa ya figo n.k.;
iv. Watumishi wa vyombo vya ulinzi na usalama; na
v. Wasafiri wanaokwenda nje ya nchi.
d. Kufanya uhamasishaji na maandalizi ya upokeaji, utunzaji, usafirishaji na utoaji wa chanjo na wananchi wawe huru kuamua kuchanja au la.
e. Serikali iratibu upatikanaji wa chanjo kwa watumishi wa taasisi za kimataifa walioko nchini.
6. Serikali ya Tanzania ijiunge na COVAX Facility kwa kuwasilisha andiko la kupatiwa chanjo, kwa kutumia fursa inayotolewa na GAVI.
7. Serikali itumie fursa zilizopo wakati huu wa janga la COVID-19 kuanza mchakato wa uanzishaji wa viwanda vya kutengeneza chanjo.
8. Serikali iimarishe huduma za uchunguzi kwa kuijengea uwezo Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii na maabara nyingine nchini ili kupanua wigo wa upimaji wa ugonjwa wa COVID-19.
9. Serikali ijenge uwezo wa ndani wa utambuzi wa virusi anuai vinavyosababisha ugonjwa wa COVID-19 na magonjwa mengine ya kuambukiza.
10. Serikali itoe takwimu sahihi za ugonjwa wa COVID-19 kwa umma na Shirika la Afya Duniani ili wananchi wapate taarifa sahihi toka Mamlaka za Serikali na kuheshimu makubaliano na kanuni ambazo nchi iliridhia.
11. Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ikamilishe mwongozo mpya wa matibabu ya ugonjwa wa COVID-19.
12. Serikali iendelee kuhakikisha kuwa matumizi ya tiba asili na tiba mbadala katika mfumo rasmi wa tiba za kisasa yanazingatia misingi ya kisayansi.
13. Serikali iendelee kutoa fursa na kuwawezesha wanasayansi kufanya tafiti kwa kufuata miiko, maadili na taratibu zilizowekwa ili kuimarisha kinga, tiba, uchunguzi wa ugonjwa wa COVID-19 na athari zake katika jamii nchini.
14. Serikali iendelee kuzingatia mazingira ya kitanzania katika udhibiti wa ugonjwa wa COVID-19 katika kuamua kuweka au kutokuweka shuruti ya kujifungia (lockdown) na kuwa na ubunifu ili kuruhusu ukuaji wa uchumi na kuimarisha sekta zinazochangia katika uchumi.
15. Wizara yenye dhamana ya fedha na uchumi ifanye tathmini ya kina ya athari za janga la COVID-19 na kuweka mpango madhubuti wa haraka wa sasa, wa muda wa kati na wa muda mrefu unaotekelezeka ili kukuza uchumi wa nchi.
16. Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ziendelee kushirikiana ipasavyo katika hatua zote za kukabiliana na janga la COVID-19 pamoja na majanga mengineyo ikiwemo utoaji wa nyaraka za kimataifa kama vile Travel Advisory Note.
17. Idara ya Maafa katika Ofisi ya Waziri Mkuu iendelee kutekeleza ipasavyo jukumu la uratibu na kutoa rasilimali husika wakati wa majanga ya kitaifa na kimataifa kama ugonjwa wa COVID-19 kwa kushirikisha ngazi na sekta zote.
18. Serikali ikamilishe malipo ya madeni ya watoa huduma na watumishi waliokuwa mstari wa mbele katika kukabiliana na ugonjwa wa COVID-19 ili kuongeza ari na tija ya udhibiti wa ugonjwa huo.
19. Serikali iendelee kushirikisha wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa dini, wadau wa maendeleo, sekta binafsi na vyombo vya habari katika mapambano dhidi ya janga la ugonjwa wa COVID-19.

Ndugu Wanahabari,

Asanteni kwa kunisikiliza.
Hii ni C&P

Thanks for this!. Alale pema peponi!, sisi tulio duniani, lazima tuendelee kuishi, kama ili kuishi ni pamoja na kupindua misimamo ya kijima ya mtangulizi, then ni bingiribingira mpaka Makka!. Kuna mambo kwenye mapendekezo hayo akina sisi tulishauri, na sasa ndio yameshauriwa na wataalamu, tuachage siasa kwenye proffesionalism, tupige siasa kwenye siasa, tuache wataalam kwenye issues za kitaalamu. Corona inatufundisha Tanzania tuna tatizo kuchanganya siasa na professionalism. Hongera Prof. Janabi kwa elimu uliyotoa, so far you are the best!
P.
 
Wanabodi,

Kuna msemo wa Kiswahili usemao "Kufa Kufaana", wakati watu wanahangaika na janga la Corona, wengine wanaangazia namna ya kutumia changamoto kuzibadili kiwa fursa, yaani turning problems, obstacles, challenges or adversaries into opportunities.

Tangu d
Hizi fursa za kupata pesa za Benki ya Dunia ya dunia ndio zinaifa Kenya iwe nyumbani kwa virusi vya corona,tafakari.
 
Wanabodi,

Kuna msemo wa Kiswahili usemao "Kufa Kufaana", wakati watu wanahangaika na janga la Corona, wengine wanaangazia namna ya kutumia
Wanabodi, japo hili ni bandiko la zamani, lakini bado liko valid, japo Corona ni janga, lakini ndani ya janga hili kuna fursa.

Naangalia TBC, saa hizi kuna mwana mama wa Kitanzania ametangaza kuwa Tanzania sasa inatengeneza barakoa zetu wetu, za kuweza kujitosheleza na ziada tukauza nje.

Mteja mkuu wa kwanza ni MSD, nashauri sasa serikali yetu upige marufuku uagizaji wa barakoa kutoka nje, sasa tutumie barakoa zetu za ndani.
Hongera Vailet kuchangamkia fursa, hongera Tanzania kutengeneza barakoa zetu.
Mungu Ibariki Tanzania.

Barakoa 1 ni 1,000. Kwa wastan ukiwa na mishe,unashauriwa barakoa 3.

Itabidi watu wasile wala kuweka bando.

Kimsingi hizi barakoa ilibidi ziuzwe 200.
 
Wanabodi, japo hili ni bandiko la zamani, lakini bado liko valid, japo Corona ni janga, lakini ndani ya janga hili kuna fursa.

Naangalia TBC, saa hizi kuna mwana mama wa Kitanzania ametangaza kuwa Tanzania sasa inatengeneza barakoa zetu wetu, za kuweza kujitosheleza na ziada tukauza nje.

Mteja mkuu wa kwanza ni MSD, nashauri sasa serikali yetu upige marufuku uagizaji wa barakoa kutoka nje, sasa tutumie barakoa zetu za ndani.
Hongera Vailet kuchangamkia fursa, hongera Tanzania kutengeneza barakoa zetu.
Mungu Ibariki Tanzania.
P
Umeshapata chanjo,wewe mzee?
 
Back
Top Bottom