Corona: Japo ni janga, pia ni fursa. Tanzania bado hakuna maambukizi, tupunguze panic, tuongeze Elimu. WB kumwaga mihela, tuchangamkie fursa

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
36,297
2,000
Wanabodi,

Kuna msemo wa Kiswahili usemao "Kufa Kufaana", wakati watu wanahangaika na janga la Corona, wengine wanaangazia namna ya kutumia changamoto kuzibadili kiwa fursa, yaani turning problems, obstacles, challenges or adversaries into opportunities.

Tangu dunia na taifa letu kukumbwa na janga la ugonjwa wa Corona, Tanzania kama Taifa, tumepanic, kila mtu ni mtaalam wa Corona, Viongozi wa serikali wakiwemo wataalamu wetu wa afya wanatoa contradictory statements kwenye media tena mbele ya Waziri wa Afya, elimu ya jinsi ya kujikinga inayotolewa ni elimu duni, hatuna vifaa vya usafi kwenye public places zetu ni mwendo wa vitisho na panic kwa kwenda mbele huku hakuna elimu yoyote proper inayotolewa na chombo chochote cha habari zaidi ya uhamasishaji wa kinga ili kuzuia.

Bandiko langu sio la kuelimisha umma kuhusu ugonjwa wa Corona au jinsi ya kujikinga, bali mimi naangazia fursa za Corona.

Kwenye kila changamoto, pia huwa kunajitokeza fursa. Concentration kubwa sasa ni kinga watu wame panikishwa na kuiona Corona kama balaa kubwa la ajabu hivyo tuko kwenye chaos hivyo kazi yangu mimi ni kuwatuliza na kuwapa michongo ya fursa mbalimbali zinazoletwa na janga hilo la Corona kwa hoja kuws japo Corona ni janga, lakini pia ni fursa, Watanzania tusiishie tuu ku concentrate kwenye janga la Corona tukajisahau kabisa na kushindwa kuziangazia fursa za Corona. Janga la Corona linaandamana na fursa mbalimbali, mfano tayari Benki ya Dunia, WB na Shirika la Fedha la Kimataifa, IMF, imemwaga mihela ya kufa mtu kwa ajili ya kufidia mdororo wa kiuchumi unaosababishwa na Corona, shurti pekee kwa fedha hizi ni lazima ziombwe, na pili, hazitolewi bure kama sadaka au grants, zitatolewa kama fursa za kukopa kwa masharti nafuu na riba ndogo. Tanzania tuchangamkie fursa hizi, vinginevyo Corona itatuumiza sana kiuchumi!.

Kwavile tangu kulipuka kwa ugonjwa huu wa Corona, so far hakuna Mtanzania yoyote aliyeambukizwa virusi vya Corona akiwa nchini Tanzania, waathirika wote 6 waliogungulika Tanzania so far, hakuna hata mmoja aliyeambukizwa Corona nchini Tanzania, wote wameambukizwa virusi vya Corona huko waliko ambukizwa, na kuvileta hapa nchini lakini licha ya ku interact na watu wote walio changamana nao, hakuna hata Mtanzania mmoja aliyeambukizwa virusi vya Corona, hivyo at this moment naweza kusema, ugonjwa wa Corona ni ugonjwa wa wazungu huko huko nchi za ulaya zenye baridi na hata mgeni akija Tanzania na virusi vyake, atabaki navyo mwenyewe, Watanzania hatuambukiziki, hivyo sasa tupunguze panic ya ugonjwa wa Corona, lets compose ourselves tuchangamkie fursa mbalimbali zinazoletwa na ugonjwa huu wa Corona.

Fursa hizi ni za aina mbili, fursa za kimataifa kwa Tanzania kama nchi kuchangamkia fursa hii ya World Bank
World Bank Group Increases COVID-19 Response to $14 Billion To Help Sustain Economies, Protect Jobs

Fursa za kitaifa kama hizi
Hapa sasa naomba Watanzania wenzangu wenye jicho la kiangazia fursa mbalimbali
 1. Fursa za uandaaji wa vipindi vya redio, television na online vya uelimishaji umma kuhusu ugonjwa wa Corona, yaani public information Programs, sasa ni kila mtu anasema lake, nilimshuhudia mtaalamu wa Afya, Daktari bingwa akiwa mbele ya Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, akizungumzia uvaaji wa mask, kiukweli alichemsha na analiingiza chaka taifa zima, hivyo nikaona hapa kuna fursa, kama hata Waziri wa Afya hajui kuhusu masks na anaingizwa chaka, vipi kuhusu sisi akina kajamba nani?.
 2. Serikali inasisitiza kutumia running water lakini hatuna vifaa vya running water kwenye public places kama hivi​
 3. images (2).jpeg
 4. Hivyo ukitengeneza hivi na kuviuza, afisi zote, public palaces zote, maduka yote, vituo vyote vya mabasi, stendi zote, vituo vya dala dala, masokoni etc, what an opportunity?
 5. Watanzania tunahimizwa kutumia hand sanitizers, hatuna sanitizers za kutosha Watanzania wote. Hivyo hii ni fursa kwa simple home made sanitizers kutumika, the simplest ni maji ya chumvi, chumvi ya kawaida ina clorine, tengeneza maji ya chumvi, pack, piga pesa!.
 6. fursa ya watu kununua ma dumu makubwa ya real sanitizers na kuyapack kwenye vichupa vidogo na kuuzia watu, japo kwenye hili, huwezi zuia matapeli kujaza maji mengi na kuweka vitone tuu vya sanitizers kuweka harufu.
 7. Soon mtashuhudia wale wauza ukwaji wa Bhakresa wakiuza sanitizers.
 8. Tuendelee kuweka fursa mbalimbali nitakuwa nazi update hapa.
Kwa wale wa Ibada leo, Ijumaa Kareem,
Kwa wale wenzangu na mimi, nawatakia Furahi Dei njema, sisi wa maji makali, Corona haituhusu!.

Paskali.
Corona Update
Tuna wagonjwa 19
Kati ya hao 16 wamekuja nayo kutoka inje.
3 wameambukizwa direct na hao waliotoka nje kutokana na close interactions
So far bado hakuna Maambukizi yoyote ya Corona locally, yaani local to local transmissions, Corona yote nchini kwetu ni imported.
Ki epidemiology vurusi vya Corona bado havijaweza kufanya mutation locally, hivyo Watanzania tuendelee kufuata ushauri wa kitaalamu wa jinsi ya kujikinga na tuendelee kufuata ushauri wa rais wetu Magufuli, tusitishane, Watanzania tuendelee kuchapa kazi.

P.
Hii ni fursa.
Nnakumbuka kipindi kile Mmarekani alipoibukia kiuchumi wakati nchi zingine zikipambana, sasa hivi nchi nyingi wanajifungia ndani, uzalishaji unapungua, sisi kama watanzania tuliopewa hii neema, angalau Covid-19 haijasambaa, ingekuwa fursa kwetu, kuangalia hawa watu waliojifungia huko ndani katika nchi zao, watakutana na hali ngumu mtaani hasa katika chakula.

Mvua bado zipo, tungelima sana sasa hivi, chakula kitauzika sana nje, wabongo tumelifikiria hili kweli, huu ndio wakati wetu wa kupanda kiuchumi SWOT Analysis, tukishindwa kutumia advantage ya corana basi tena.

(Ni wachache sana wananielewa) ninarudia tena ( huwezi nielewa kama unauwezo mdogo wa kufikiri)

Hivyo yaani!
Rejea za Mandiko ya The Same Author Kuhusu Janga la Corona
 1. Mtu kama huyu ni binadamu au shetani? Anaombeaje Corona ifike Tanzania. Kuiombea nchi yako majanga, sio zaidi ya uendawazimu? Huu sio ushetani? - JamiiForums
 2. Corona: Japo ni janga, pia ni fursa. Tanzania bado hakuna maambukizi, tupunguze panic, tuongeze Elimu. WB kumwaga mihela, tuchangamkie fursa - JamiiForums
 3. Corona inatufundisha Tanzania tuna tatizo kuchanganya siasa na professionalism. Hongera Prof. Janabi kwa elimu uliyotoa, so far you are the best! - JamiiForums
 4. RC Makonda, Dar ni jiji la wote, vyama vyote. Mbowe sio mwanasiasa uchwara aliyefilisika, Zitto sio mshirikina. Tunakupenda, heshimu wote uheshimiwe - JamiiForums
 5. Je, ni kweli kuna Waziri anaugua Corona inafanywa Siri? Tunaficha nini? Hala hala kisa cha mficha maradhi! Truth & Transparency the only way out! - JamiiForums
 6. Star TV: Msemaji Mkuu wa Serekali, Dr. Hassan Abbas, azungumzia wajibu wa vyombo vya habari kuripoti janga la Corona - JamiiForums
 7. Ama kweli nabii hakubaliki nyumbani!. Je Magufuli ni nabii? Tanzania wanambeza, Afrika wanamlilia! Tanzania yapigiwa mfano Magufuli awe Rais wa Afrika - JamiiForums
 8. Vita Janga la Corona: Msemaji Mkuu wa Serikali, Dr. Hassan Abbas, Naibu Waziri wa Afya, Dr. Faustine Ndungulile, kesho watakuwa live JLNH-Star TV - JamiiForums
 9. Star TV: Msemaji Mkuu wa Serikali, Dr. Hassan Abbas na Naibu Wazuri wa Afya Dr. Faustine Ndungulile, Wanazungumzia Corona - JamiiForums
 10. Mungu ni Omnipresent. Kufuatia Local Transmission ya Corona. Je, Sasa Tushinikize Watu Wasalie Majumbani Mwao, ila Sadaka Ndio Itumwe Kwa M-Pesa? - JamiiForums
 11. Nabii Malisa: Mungu ameniambia Corona ni April tu, May hakuna Corona na hakuna atakayekufa!. - JamiiForums
 12. Kwa Kasi Sasa, Jee Tuendelee Ushujaa wa Ka-Corona, Tusitishane, Tuchape Kazi Tukiteketea, Au Sasa Tubadili Msimamo Tusitisishe Mikusanyiko Tuokoke? - JamiiForums
 13. TBC - Mjadala wa Role of The Media kwenye mapambano ya Corona, Je, Media Inatimiza Wajibu Wake Ipasavyo? - JamiiForums
 14. Live on Star TV: Corona Kushika Kasi Ndio Habari Kubwa Tanzania, Jee Media ya Tanzania, Inatimiza Wajibu Wake Ipasavyo? - JamiiForums
 15. Corona: Tusinyoosheane vidole. Kama unaweza kusaidia, please do. Usisubiri uombwe - jitokeze saidia, vinginevyo nyamaza! - JamiiForums
 

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
36,297
2,000

matunduizi

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
2,430
2,000
Usiite fursa majanga mkuu.
Nilitegemea uombe serikali iingilie kati ili kila maeneo ya lazima hivyo vitu vipatikane.
Ikiwezekana viuzwe kwa wananchi bila kodi, au viwanda vitengeneze kwa bila faida ili kuokoa maisha ya wateja wao wa baadae.


umeandika viu vya hovyo bwana mkubwa.
Ila shikamoo
 

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
36,297
2,000
Unafungua kantini yako maana wengi wenye koroma huwekwa kantini,unawaekea Bajia,chai ya mdalasini nk.
Tujifunze kujitoa kusaidia janga lipite sio kutafutia utajiri kwenye vifo!!
Kuchangamkia fursa sio kutafuta utajiri,but making the best out of the opportunities offered.
Mfano hizo fedha za WB, kama Tanzania hatutaziomba, watatumwa ma consultants Wazungu kuja kufanya needs and assessment ya mahitaji ya Tanzania kupambana na Corona, half the money zinarudi kwao interms of consultancy fees na imported supplies, wakati kila kitu tunaweza!.
P
 

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
36,297
2,000
Usiite fursa majanga mkuu.
Nilitegemea uombe serikali iingilie kati ili kila maeneo ya lazima hivyo vitu vipatikane.
Ikiwezekana viuzwe kwa wananchi bila kodi, au viwanda vitengeneze kwa bila faida ili kuokoa maisha ya wateja wao wa baadae.
Hivyo vitu vipatikane wapi?, vishushwe kutoka mbinguni kama mana?. Ile kuvitengeneza tuu ni fursa!. Tuna viwanda kibao vya madawa, sasa tunasubiri ndege ya kutoka China ituletee sanitizers na masks za kututosha wakati tuna fursa ya kuzitengeneza wenyewe!.
P
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom