Corona isiondoe imani yetu kwa Mungu mponyaji, Tanzania yangu endelea kumtazama Mungu

MIMI BABA YENU

JF-Expert Member
Mar 1, 2019
295
679
By Pastor FRANK ANDERSON SIKAWA
Instagram: Pastor_Sikawa19

TANZANIA YANGU ENDELEA KUMTAZAMA MUNGU

NAMI SIKU HIYO NITATENGA NCHI YA GOSHENI, WATU WANGU WANAYOKAA, ILI HAO MAINZI WASIWE HUKO; ILI KWAMBA UPATE KUJUA WEWE YA KUWA MIMI NDIMI BWANA KATI YA DUNIA.
(Kutoka 8:22)

“BWANA YESU ASIFIWE WANA WA MUNGU ALIYE HAI”
Ni siku ya kumi na saba, tangu Machi 15, 2020 majira ya jioni ambapo alitangazwa mtu wa kwanza aliyebainika kuwa na virusi vya COVID-19 nchini Tanzania. Katika kipindi hicho tayari dunia nzima ilikuwa imejawa na hofu kuu iliyotokana na namna vyombo vya habari vya Kitaifa na Kimataifa vilivyokuwa vikitangaza idadi ya vifo ya watu katika mataifa mbalimbali (China, Italia, Hispania, n.k) vilivyotokana na ugonjwa wa CORONA.
Hofu hiyo, imezidi kuchagizwa na taarifa zinazoendelea kutolewa na vyombo mbalimbali vya habari na mitandao ya kijamii. Kuna baadhi ya mambo ambayo Mungu anaikumbusha Tanzania na kuyataka tuyafanyie kazi;

1. Virusi vya COVID-19, visisababishe tukaondoa MACHO NA TUMAINI LETU KWA MUNGU anayetulinda hadi sasa. Kwani kwa namna yeyote ile bila NEEMA YA MUNGU sisi kama Tanzania hatutawezi kukabiliana na virusi vya COVID-19. Tazama mataifa ya Ulaya ambayo yana kila kitu (teknolojia, wataalam, miundombinu, fedha n.k) bado wanaendelea kutaabishwa na virusi vya COVID-19 na watu wengi bado wanaendelea wamekufa.

“MAANA, TAZAMA, GIZA LITAIFUNIKA DUNIA, NA GIZA KUU LITAZIFUNIKA KABILA ZA WATU; BALI BWANA ATAKUZUKIA WEWE, NA UTUKUFU WAKE UTAONEKANA JUU YAKO. (ISAYA 60:2)”

Dunia imefunikwa kwa HOFU YA MAUTI...watu wamefanywa watumwa, wanalazimishwa kukaa majumbani wakikutwa wanatembea wanapigwa, wanateswa, wanauwa n.k...ukiuliza sababu utaambiwa wanazuia maambukizi ya CORONA.

Shetani kapofusha fikra za watu WAMEMSAHAU KUMTAZAMA KWANZA MUNGU WAKATEGEMEA JUHUDI NA MAARIFA YAO KATIKA KIKABILIANA NA VIRUSI VYA COVID-19.

TANZANIA TUNAYE MTU WA KUMTAZAMA, AMBAYE NI YESU KRISTO PEKEE....TUSITAZAME KINACHOTOKEA KWA MATAIFA MENGINE TUKAFANANISHA NA KWETU, HATUISHI KWA MLINGANISHO WA MAISHA BALI KWA NEEMA YA MUNGU....TAMBUENI NEEMA YA MUNGU IMETUFUNIKA NDIYO INAYOTUFANYA TUWE NAMNA TULIVYO SASA.

DUNIA INATUSHANGAA, INAONA KAMA HATUJIELEWI...WATU WANAISEMA SERIKALI, WANAMSEMA RAIS LAKINI HAWAJUI NINI AMBACHO KINACHOENDELEA KATIKA ULIMWENGU WA ROHO. LAITI TUNGETAZAMA KILICHOPO ROHONI TUNGEMTAZAMA SANA MUNGU BILA KUTAZAMA WENZETU WANAFANYA NINI


2. Suala la ugonjwa wa CORONA siyo la Kimwili kama watu wanavyolitazama; bali ni suala la KIROHO. Shetani kupitia majeshi yake anajaribu kuiweka dunia katika hofu kuu ambayo ikiingia ndani ya watu italeta madhara kwa kiwango kikubwa sana. Watu wengi hawatakufa kwa sababu ya CORONA bali kwa hofu iliyoingizwa ndani yao kwa taarifa ambazo wamekuwa wakizisikia zikitangazwa mara kwa mara; kwa MAANA HOFU INA TABIA KAMA YA IMANI.....VYOTE VIWILI VINATEGEMEA NENO/MANENO ILI VIWEZE KUSHAMIRI. Hivyo, taarifa za mara kwa mara za vifo na maambukizi zimejenga hofu kuu katikati ya dunia.

Hofu ni silaha kubwa sana ya adui ambayo amekuwa akijaribu kuitumia kuangamiza watu. Na ijulikane suluhisho pekee la kuiondoa hofu ni kuukubali UPENDO WA MUNGU (1 YOHANA 4:18) kwenye maisha yetu ya kwamba Mungu alimtoa Yesu Kristo kwa ajili ya kutuondolea hofu ya mauti iliyokuwepo na itakayokuja kwenye maisha yetu. WAEBRANIA 2:14-15 inasema; “BASI, KWA KUWA WATOTO WAMESHIRIKI DAMU NA MWILI, YEYE NAYE VIVYO HIVYO ALISHIRIKI YAYO HAYO, ILI KWA NJIA YA MAUTI AMHARIBU YEYE ALIYEKUWA NA NGUVU ZA MAUTI, YAANI, IBILISI, AWAACHE HURU WALE AMBAO KWAMBA MAISHA YAO YOTE KWA HOFU YA MAUTI WALIKUWA KATIKA HALI YA UTUMWA”


3. Kauli ya Mhe. Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt. JOHN POMBE MAGUFULI.

“Watu tusitishane, tunatishana mno. Niwaombe ndugu Wakristo na Watanzania kwa ujumla wa Madhehebu yote, huu ndio wakati mzuri sana wa kumtegemea Mungu kuliko wakati wote, tuendelee kuchapa kazi, tuendelee kuujenga uchumi wetu, hatuwezi kusalimu amri kwa ugonjwa huu wa Corona na kushindwa kumtegemea Mungu na tukashindwa kuendeleza uchumi wetu”

Wengi wanambeza Mhe. Rais, wanatumia maneno hayo kujinufaisha kisiasa, wengine kuonesha kwamba hatuko makini lakini hawaujui uzito wa kauli yake katika ulimwengu wa Roho. Wanahisi kajisemea tu, lakini nataka kuwaambia kulikuwa na msukumo wa Kimungu ndani yake ambao haukuwa wa kawaida. Maana kilichokuwa kinahitajika ni NENO LITAKALOIFUNIKA TANZANIA KATIKA KIPINDI AMBACHO DUNIA IMEKUMBWA NA JANGA HILO LA VIRUSI VYA COVID-19.

“LAKINI YEYE HUOKOA NA UPANGA WA KINYWA CHAO, HATA KUMWOKOA MHITAJI NA MKONO WAKE ALIYE HODARI - AYUBU 5:15)”

Lilihitajika neno la Mhe. Rais kuwa MUONGOZO katika ulimwengu wa Roho ambao ndio unatoa matokeo katika ulimwengu wa mwili. Angeungana na kauli na mtazamo wa dunia hali isingekuwa ilivyo hivi leo. Tazama, waliofunga mipaka, waliowataka watu wakae ndani, waliozuia ibada kufanyika....Je, Corona haiwaui? Corona imeondoka? Tunaitaji tupaze sauti zetu kwa Mungu hata kama dunia yote itaona Tanzania hatuko serious kwa maana “KAULI ILIYOTOLEWA NA KIONGOZI WA NCHI NDIO INAYOAMUA MUSTAKABALI WA MAISHA YETU”

MASUALA YA ROHONI HUWA YANAAMUA MUSTAKABALI WA MAISHA YA MWILINI

“KWA MAANA MAAGIZO HAYA NIKUAGIZAYO LEO, SI MAZITO MNO KWAKO, WALA SI MBALI. SI MBINGUNI, HATA USEME, NI NANI ATAKAYETUPANDIA MBINGUNI AKATULETEE, AJE ATUAMBIE TUSIKIE, TUPATE KUYAFANYA? WALA SI NG'AMBO YA PILI YA BAHARI, HATA USEME, NI NANI ATAKAYETUVUKIA BAHARI, AKATULETEE, AJE ATUAMBIE, TUSIKIE, TUPATE KUYAFANYA? LAKINI NENO LI KARIBU NAWE SANA, LI KATIKA KINYWA CHAKO NA MOYO WAKO, UPATE KULIFANYA. ANGALIA, NIMEKUWEKEA LEO MBELE YAKO UZIMA NA MEMA, NA MAUTI NA MABAYA; (KUMBUKUMBU 30:11-15)”
UWEZO WA CORONA KUTISHA NA KUANGAMIZA MAISHA YA WATU KWENYE NCHI YEYOTE KUNATEGEMEA UKIRI WA WATU WENYEWE PAMOJA NA IMANI ZAO KWA MUNGU WANAYEMWABUDU.
KUMBUKA: Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi (Mithali 18:21) Hivyo, matokeo ya Corona kwenye nchi yetu yanategemea ukiri wetu.

4. Kanisa la Tanzania, simameni katika zamu yetu. Ni wakati wa kumtazama nyoka wa Shaba. Ni wakati wa kunyenyekea chini ya mkono wa Bwana aliye hodari. Siyo wakati wakusikiliza kelele za dunia ni wakati wa kusikiliza kwa Mungu kuna nini. Wachungaji, Walimu, Manabii, Mitume na Wainjilisti hiki ni kipi kile ambacho Adui anajaribu kuona kama mnamtumaini Mungu au mnatumaini vitu mlivyonavyo.

“Dunia inaomboleza, inazimia; ulimwengu unadhoofika, unazimia; watu wakuu wa dunia wanadhoofika. Tena dunia imetiwa unajisi kwa watu wanaoikaa; kwa maana wameziasi sheria, wameibadili amri, wamelivunja agano la milele. Ndiyo sababu laana imeila dunia hii, na hao wanaoikaa wameonekana kuwa na hatia, ndiyo sababu watu wanaoikaa dunia wameteketea, watu waliosalia wakawa wachache tu. Divai mpya inaomboleza, mzabibu umedhoofika, watu wote waliochangamka moyo wanaugua. Sauti ya furaha ya matoazi inakoma; kelele yao wafurahio imekwisha; furaha ya kinubi inakoma. Hawatakunywa divai pamoja na nyimbo; kileo kitakuwa uchungu kwao wakinywao. (Isaya 24:4-9)

Kama Tanzania tutafute siku moja ya Kitaifa tufanye kitendo cha Imani kumshukuru Mungu kwa kutulinda na kutuponya na Corona.

5. Watanzania tuendelee kufuata maelekezo ya kitaalam yanayotolewa kila siku ili kuzuia kuenea kwa virusi vya COVID-19, lakini tukumbuke kuwa MUNGU PEKEE ndiye MPONYAJI. Ulaya wana kila kitu lakini………

NB. 07/04/2020 DUNIA INAINGIA KATIKA PHASE MPYA YA HABARI ZA COVID-19 NA KWA UPANDE WA TANZANIA KUTAKUWA NA HABARI ZA KUDHIHIRISHA KAMA SIYO MUNGU TUSINGEWEZA.

PIA WENGI WATAENDELEA KUMSEMA MHE. RAIS NA HATA KUANDIKWA KATIKA VYOMBO VYA KIMATAIFA LAKINI MWISHONI ATAIBUKA SHUJAA MKUU….OMBEA TANZANIA, MUOMBEE NA RAIS WETU…..AMEN

MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU MBARIKI RAIS WETU MAGUFULI



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom