Corona inaua Wamarekani takribani 1,300 kwa siku

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,987
17,860
Corona inaua Wamarekani takribani 1300 kwa siku

Dec 18, 2021 13:16 UTC

Idadi ya watu wanaofariki dunia kutokana na COVID-19 nchini Marekani ni takribani watu 1,300 kwa siku.

Kwa mujibu wa gazeti la New York Times, katika siku za hivi karibuni baada ya aina mpya ya COVID -19 ijulikanayo kama Omicron kuingia Marekani, mgogoro wa kiafya umezidi kukithiri nchini humo. Idadi ya watu wanaolazwa hospitalini kutokana na corona imeongezeka jambo ambalo limezidisha wasiwasi nchini humo.

Taarifa zinasema idadi ya waliolazwa hospitalini kutokana na COVID-19 nchini Marekani imeongezeka kwa asilimia 20 katika kipindi cha wiki mbili zilizopita.

New York Times limeandika kuwa, wakati ambao hospitali za Marekani zimejaa wagonjwa wa COVID-19, kirusi aina ya Omicron kinaendelea kusambaa na sasa hospitali za nchi hiyo zinasemekana kuwa katika 'mgogoro wa daima'.

Gazeti hilo pia limeandika kuwa, katika siku ya Ijumaa pekee watu 21,000 waliabukizwa COVID-19 katika mji wa New York.

Licha ya kuwa Marekani ilijirundukia chanjo tokea mwanzo wa janga la COVID-19 na kukataa kuzipelekea katika nchi zingine duniani, watu milioni 51 na nusu wameambukizwa ugonjwa huo na wengine 826,000 wamepoteza maisha nchini umo kutokana na COVID-19. Idadi kubwa ya Wamarekani wanapinga chanjo na hiyo imetajwa kuwa moja ya sababu za kuenea maambukizi nchini humo.

Hayo yanajiri wakati ambao mawaziri wa afya wa nchi za kundi la G7 wametangaza kuwa, kutokana na kasi yake kubwa ya usambaaji, spishi ya kirusi cha corona ya Omicron ndio tishio kubwa zaidi kwa usalama wa afya duniani.

Katika taarifa yao ya pamoja, mawaziri hao wa afya wa Marekani, Uingereza, Canada, Japan, Ujerumani, Ufaransa, Italia pamoja na Umoja wa Ulaya wametilia mkazo umuhimu wa watu kupiga chanjo ya kuimarisha kinga.

Shirika la Afya Duniani (WHO) nalo pia limeitaja aina ya corona ya Omicron kuwa ni kirusi kinachotia wasiwasi.
 
KWa taarifa yako kwa kila watu 5 wanaokufa kwa covid-19, 4 wamepata chanjo dozi 3 hadi 4. Hapa wakuu na-declare my interest mimi sio mwanasiasa ni Muuguzi kwa taaluma(sasa hivi ni mchimbaji mdogo wa dhahabu) takwimu hazisemagi uongo!
image-240.png
image-243.png
 
KWa taarifa yako kwa kila watu 5 wanaokufa kwa covid-19, 4 wamepata chanjo dozi 3 hadi 4. Hapa wakuu na-declare my interest mimi sio mwanasiasa ni Muuguzi kwa taaluma(sasa hivi ni mchimbaji mdogo wa dhahabu) takwimu hazisemagi uongo!
View attachment 2049974View attachment 2049976
nani atamfunga paka kengele?
 
KWa taarifa yako kwa kila watu 5 wanaokufa kwa covid-19, 4 wamepata chanjo dozi 3 hadi 4. Hapa wakuu na-declare my interest mimi sio mwanasiasa ni Muuguzi kwa taaluma(sasa hivi ni mchimbaji mdogo wa dhahabu) takwimu hazisemagi uongo!
View attachment 2049974View attachment 2049976
Umefanya vema kutujuza,umetumia taaluma yako vema.
 
America Binadamu wabishi sana wakiambiwa wasichanjwe .
Wanaenda kuchanjwa
 
Back
Top Bottom