Corona imethibitisha bila shaka Zanzibar ni mkoa wa Tanzania, haina haja ya Serikali mbili, ni kupoteza hela

Johnny Sack

JF-Expert Member
Jan 21, 2017
8,814
18,803
Sakata la Corona limethibitisha bila shaka kabisa kuwa Zanzibar ni mkoa wa Tanzania ama Tanganyika Kama wenyewe wanavyopenda kuita.

Sababu ni Zanzibar ilikuwa ikitoa updates za Corona tofauti na Tz Sababu suala la Afya sio la Muungano, Tanzania ilipoacha kutoa updates, Zanzibar waliendelea kutoa update zao, nikajisemea kweli hawaingiliwi kwenye mambo Yasiyo ya Muungano.

Lakini baadae Tz ilitangaza kufunga maabara yake kwa madai kuwa mashine za kupimia haziaminiki,

Zanzibar wakatangaza kununua mashine yao ili wasiitegemee Tz Tena Wala maamuzi yao kuhusu namna ya ku handle Corona yasiwaathiri.

Lakini Cha ajabu licha ya kununua ile mashine imebidi tu wacheze ngoma ya Tanzania kuhusu Corona, nadhani Shein alipigiwa simu na kuamrishwa ampige stop Waziri wake wa Afya, hakuna Cha suala la Muungano au la.

Naona huu Muungano na Serikali mbili umebaki tu kwenye makaratasi, Zanzibar hawana power yoyote real ya kuamua chochote Cha muhimu hata kusipokuwa Cha Muungano, ni muda Sasa wa ku-integrate fully tuwe kitu kimoja tuachane na huu mchezo.
 
Jifunze tofauti ya Zanzibar na Tanganyika pia jifunze maana ya Tanzania maana naona ume mix mafile kwenye huu uzi wako.
Tanganyika hakuna, ilishakufa 1964, Kuna Tanzania,

Unaweza kuniambia Rais wa Tanganyika ni Nani? Bendera yake? Katiba ya Tanganyika?
 
Sakata la Corona limethibitisha bila shaka kabisa kuwa Zanzibar ni mkoa wa Tanzania ama Tanganyika Kama wenyewe wanavyopenda kuita.

Sababu ni Zanzibar ilikuwa ikitoa updates za Corona tofauti na Tz Sababu suala la Afya sio la Muungano, Tanzania ilipoacha kutoa updates, Zanzibar waliendelea kutoa update zao, nikajisemea kweli hawaingiliwi kwenye mambo Yasiyo ya Muungano.

Lakini baadae Tz ilitangaza kufunga maabara yake kwa madai kuwa mashine za kupimia haziaminiki,

Zanzibar wakatangaza kununua mashine yao ili wasiitegemee Tz Tena Wala maamuzi yao kuhusu namna ya ku handle Corona yasiwaathiri.

Lakini Cha ajabu licha ya kununua ile mashine imebidi tu wacheze ngoma ya Tanzania kuhusu Corona, nadhani Shein alipigiwa simu na kuamrishwa ampige stop Waziri wake wa Afya, hakuna Cha suala la Muungano au la.

Naona huu Muungano na Serikali mbili umebaki tu kwenye makaratasi, Zanzibar hawana power yoyote real ya kuamua chochote Cha muhimu hata kusipokuwa Cha Muungano, ni muda Sasa wa ku-integrate fully tuwe kitu kimoja tuachane na huu mchezo.
Watu wanaohojigi hili suala huwa wanapotezwa.
 
mleta mada ni uthibitisho kwamba nyerere alikua na akili,ngoja nikatazame ile hotuba ya Mwalimu huko youtube
 
Back
Top Bottom