Corona imekuwa mradi wa Serikali au Mradi wa watu? Wanaowekwa karantini walalamikia bei kubwa ya hoteli wanazopelekwa

Kwa sisi Tuliopo nje ya Tanzania ukifika kiwanja cha ndege ukisha toka nje unapelekwa Hoteli ya bei ghali sana kiasi ambapo hata uwezo wa kulipia hizo hoteli huna. Mheshimiwa Rais Magufuli Mheshimiwa Waziri Mkuu Mr Majaliwa na Mheshimiwa Waziri wa Afya Bi Ummi hebu ingilieni hilo Tatizo letu jamani tunaumia . Kwa kupelekwa Hoteli zenye Bei ghali sana mutuoneni huruma. Angalia Video mama huyo akilalamika.👇👇👇😭😭

 
Museveni kapendekeza shule zitumike, kwa vile zimefungwa hakuna wanafunzi.... let’s buy the idea.
 
Maana yake ni kwamba "hawatakiwi kusafiri", lugha nyepesi kabisa hiyo.
Baadhi ya Wasafiri waliofika Uwanja wa Ndege wa Dar na kutakiwa kujiweka Karantini kwa gharama zao wakilalamika kuwa wametakiwa kukaa hoteli zenye gharama

Wasafiri hao wameomba msaada kwa Mamlaka hususan Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu kwani wametakiwa kukaa katika hoteli za Southern Sun, Rungwe, Dar Palace na Peacock Hotel

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uwezo wa kujigharamia unatofauti na mtu na mtu huwezi ukafanya kwa kukomoa kama hivyo na kumbuka hii ni dharura
Wakiwa frustrate hao watu wanaweza kujikuta wanakuwa na maamuzi yasiyo na busara mojawapo ikiwa ni kuusambaza ugonjwa kwa makusudi kwa wengine (kwa wale watakaohisi tayari wanao).
 
Sky Eclat,
Labda baadaye watasaididiwa na serikali maana kwa gharama hizo za hotel, ni wazi kuwa baada ya karantini mtu atajikuta anadaiwa fedha ambazo hawezilipa!
Hivi katika hali ya kawaida hizo hotel na hadhi zilizo nayo zimeamua ku risk biashara zao bila kuwepo na kishawishi chochote kilicho nyuma ya pazia? Tujiulize kwa kukubali kutumika kama quarantine kwa wagonjwa wa corona watakuwa wamepoteza wateja wangapi walio na uhakika wa kulipa watakaoogopa kupanga hapo huku wakiamua kupokea abiria wachache tena wengi wao wakiwa ni wale wasio na uhakika wa kuja kulipa hizo gharama za kukaa hapo? Yawezekana hayo mamilioni yaliyotolewa kwenye shughuli za mwenge yamelipwa kwenye hayo mahoteli kufidia hasara watakayopata na hivyo kuyafanya yashawishike kupokea wagonjwa hao. Na yawezekana hao abiria wanaopelekwa huko mahotelini baada ya hizo siku 14 za kuwa quarantined wakilipa au wakishindwa kulipia gharama hotel haitapata hasara na kama wakilipa hotel itarudisha hiyo pesa serikalini kimya kimya japo serikali inaweza isitangazie umma kwamba tayari imelipia hizo gharama kwenye hotel zilizoteuliwa kupokea wenye corona. Kwa vyovyote vile ilifaa hiyo quarantine iwe kwenye public health facility ambapo kunakuwa na usimamizi wa vyombo vya serikali kama watu wa afya, watoa ushauri nasaa/watu wa psychology, ulinzi n.k.
 
Hoteli wanazo takiwa kukaa wanaoingia nchini kwa siku kumi na nne ni:
Rungwe
Peacock Hotel
Dar Palace na Southern Sands

Wasafiri wanategemewa kukaa kwa gharama zao. Hoteli ni ghali sana, maamuzi haya yamekuwa mateso kwa wasafiri.
Eti dada..kwa hiyo Wateja wanakuwa ni hao tu wa karantini au na mie wa kawaida nikienda naruhusiwa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanafikiri kila anaetoka nje amekuja na pesa? Yaleyale wakati mdogo niko Kijijini nilifikiri kila mtu anaetoka mjini anapesa ata kama ni mwanafunzi katoka bweni.......Tunaongozwa na washamba
Hapo nadhani wanashindwa tu kusema mipaka imefungwa hakuna kusafiri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hotel za watu wakubwa s\kalini au za mashosti zao,sawa na dokta kukuelekeza duka la dawa la kwenda kununuwa ili kumpa ulaji jamaa yake.suluhisho s\kali kupita kuhakiki kama gharama zimepanda kuliko kawaida kusaidia kusovu.au kuwaelekeza hotel nafuu
 
Mnyororo unaoweza kusababisha maambukizi

Hawa waliowasili kutoka nje wanawasili na kuwekwa ktk hoteli za binafsi mfano hoteli ya Peacock mtaa wa Lumumba kulipo ofisi ndogo ya CCM makao makuu Dar es Salaam .


Scenario 1 :Mfanyakazi wa Peacock Hotel anaenda kupiga soga na Polepole ktk mitaa ya Lumumba jijini Dar. Baadaye Polepole anakwenda kikazi Dodoma. Ana mkutano na mawaziri kupima utekelezaji wa sera za CCM zilizomo ktk ilani ya ahadi za CCM.

Mawaziri wanaitwa na Waziri Mkuu katika kikao na mawaziri wake kupanga mikakati ya kupambana na coronavirus.




Scenario 2: Wanaowasili toka nje wanapelekwa shule ya Mgulani JKT. wanawekwa karantini siku 14 chini ya ulinzi wa kijeshi wa SUMA. Askari wa SUMA wenye nidhamu hakuna kutoka nje ya kambi korona imedhibitiwa kisawasawa isisambae.


April 5 , 2020
Mpya Hivi punde

Wasafiri kutoka nje ya nchi kupelekwa karantini Hosteli za Magufuli


Wasafiri kutoka nje ya nchi kupelekwa karantini Hosteli za Magufuli ... kukaa karantini kwa muda wa siku 14 katika hosteli za Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam maarufu hosteli za Magufuli....
Source:
Wasafiri kutoka nje ya nchi kupelekwa karantini hosteli za Magufuli .

Serikali imetangaza rasmi kwamba wasafiri wote kutoka nchi za nje zilizoathirika na ugonjwa wa Corona watalazimika kukaa karantini kwa muda wa siku 14 katika hosteli za Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam maarufu hosteli za Magufuli.

Akizungumza katika hosteli za Magufuli, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema wasafiri hao watafikia katika hosteli za Magufuli ambazo zipo katika eneo la Ubungo Jijini Dar es Salaam.

“Lengo ni kuhakikisha tunadhibiti mienendo ya wasafiri hawa.Tumeona taarifa ambazo zimetoka kule Iringa, kuna baadhi ya wasafiri tuliwaweka hotelini wakatoroka sasa ili kudhibiti mienendo ya wasafiri hawa na kuwalinda Watanzania wengi tumeona kuna ulazima wa kuwaweka sehemu moja ambako kutakuwa na ulinzi wa saa 24 na mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa wa Dar es Salaam,Bw. Paul Makonda atasimamia kwa karibu chini ya Wizara ya Afya,” amesema Waziri Ummy Mwalimu.

Waziri Ummy Mwalimu amewataka wananchi waelewe kwamba wasafiri hao si wagonjwa kwa sababu wanatoka kwenye nchi zenye maambukizi yenye virusi vya Corona (Covid-19) hivyo wasichukuliwe kama ni wagonjwa.

“Tunawachukulia kwamba miongoni mwao kuna mmoja, wawili au watu watatu wakawa na maambukizi ya virusi vya Corona.

Tutawaweka hapa kwa siku 14 kwa lengo la kuwaangalia afya zao, itakapofika siku 14, wale ambao hawajaonyesha DALILI zozote tutawaruhusu waende majumbani kwao lakini wale watakaoonyesha dalili ndani ya siku tano, sita, Saba, nane hadi siku ya 14 tutachukua sampuli na kuwapima ili kujiridhisha Kama wana virusi vya Covid-19,” amesema Ummy Mwalimu.

Waziri Ummy Mwalimu amesisitiza kuwa kwa mujibu wa taarifa za maambara Hali ya wagonjwa waliopata maambukizi ya Covid-19.“Tuko vizuri, watu waliopata maambukizi ni 20, tumepata kifo kimoja, wagonjwa watatu wamepona na wamesharudi nyumbani.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameishukuru Wizara ya Afya kwa namna ambavyo Imekuwa ikipambana kudhibiti kuenea kwa ugonjwa wa Corona nchini.


WhatsApp-Image-2020-04-05-at-07.43.38-1024x683.jpeg




“ Sisi Kama Mkoa tumejipanga kuhakikisha kwamba watu wote wanaokuja na ambao wapo wanakuwa na afya Njema kwa ajili ya kujenga uchumi wa Mkoa wetu na Taifa kwa ujumla.

“Maelekezo ambayo ameyatoa mheshimiwa waziri wa Afya ni maelekezo ambayo kila anayeingia kwenye Mkoa huu kutoka nchi yoyote, Magufuli hoteli inamuhusu,” amesema Paul Makonda.

Makonda amewataka Watanzania kufanya kazi na kwamba kuanzia kesho jumatatu atawakamata wazururaji wote wanaozunguka mjini bila kuwa na kazi maalumu watakamatwa kwa kuwa wanasababisha mikusanyiko isiyokuwa na tija.
 
Back
Top Bottom