Corona ilivyosababisha ununuzi mwingi wa Bunduki USA

Black Sniper

JF-Expert Member
Dec 10, 2013
28,373
45,583
Tatizo la Corona huko USA limeleta taharuki kubwa ya wananchi kukimbilia na kununua silaha zaidi

Kutokana na vifo vingi vya maambukizi haya na kufungiwa ndani (lockdowns)
Wananchi wameamua wengi wao kununua bunduki
Ingawa wataalamu wanasema sio woga tu

March 2020 FBI walileta takwimu zao za manunuzi ya bunduki tangu mwaka 1998 walipoanza takwimu hizi
21 March 2020 pekee imeonekana bunduki 210,000 zilinunuliwa na hii ni rekodi kubwa sana kwa manunuzi ya siku moja.

Data za FBI zinaonyesha bunduki zaidi ya million mbili zilinunuliwa kwa mwezi wa tatu tu mwaka huu, ongezeko la 1.1m ukilinganisha na mwezi wa tatu mwaka 2019

Illinois ndio inaongoza kwa manunuzi ya karibia nusu million ikifuatiwa na Texas, Kentucky, Florida na California

Nini kimewafanya watu wanunue sana bunduki wakati huu?

Professor wa Georgia State university law school bwana Timothy Lytton alipoulizwa akasema kuna mambo mawili makubwa, moja watu wanaogopa huenda siku moja idara na taasisi zikazidiwa uwezo wa kufanya kazi na kusababisha vurugu kubwa

La pili kujihami au survival tools kama wanavyoiita
Makala haya yameandikwa na majarida mengi na BBC pia

Kwa kumalizia, kama lockdown inaleta taharuki hivi katika taifa kubwa kama USA na watu wanafanya haya Kweli tujitafakari sana


Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Sijui mataifa mengine yanafeli wapi, sisi Tanzania tumefanikiwa kuidhibiti corona kabisa bila kutumia nguvu sana:oops:

Mengi hatujui Mkuu sio kuwa tumedhibiti bali halijatupata kihivyo
Huu ugonjwa ni balaa usiombe

Ila nao wanaliona joto
Hapo naona Mchina kashinda vita ya 3 bila kutupa kombora


Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Kwa bongo bunduki ndio zitahitajika zaidi ikija hii lockdown shida ni sheria kuwa tight tu.

Sababu uporaji utakuwa juu zaidi kwenye makazi ya wenye nacho ili kupata chakula.

BTW:Ina maana ule mpango wa kuwepo sheria kali za kumiliki silaha ziligonga mwamba huko states?

Maana inaonesha ni kama kununua vocha tu kwa Mangi.

This country needs guns too!
 
Kabisa mkuu, mambo yame badilika ghafla sana

Huku tunashangaa zaidi tuko lockdown na watu wanakufa sana
Uchumi unaporomoka kwa kasi hela haina thamani tena
Sijui maisha yatakuwaje maana kila mmoja anapambana na hali yake
Kumbe vacations bila kusafiri inawezekana
Matibabu bila kwenda nje yanawezekana
Ubabe umeisha kwa mataifa makubwa


Sent from my iPhone using Tapatalk
 
US wako overrated sana.. lile battle na Iran & haya mapambano na corona ndio yamekuja kuwaumbua.

Kweli kabisa waliaminisha wengi kuwa wao ndio superpower
Sasa ndege za vita zinapigwa vumbi na billion of $s zimelala
Kweli biological warfare ndio kiboko yao


Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Kwa bongo bunduki ndo zitahitajika zaidi ikija hii lockdown shida ni sheria kuwa tight tu.

Sababu uporaji utakuwa juu zaidi kwenye makazi ya wenye nacho ili kupata chakula.

BTW:Ina maana ule mpango wa kuwepo sheria kali za kumiliki silaha ziligonga mwamba huko states?

Maana inaonesha ni kama kununua vocha tu kwa Mangi.

This country needs guns too!

Sisi bunduki ni kazi kupata maana haziuzwi dukani
Ni mapanga tu na visu, rungu na sumu ya panya

Ukisoma report ya manunuzi ya bunduki hata wao serikali na FBI yao hawajui takwimu kamili maana wengine wanazo mpaka bunduki 200 kama collection zao na sasa wamepata fursa za kuziuza tena ni process ndogo sana kununua
Wengine unampa hela unasepa nayo tu

Mkuu hawawezi kuacha hii baishara maana Ina wakubwa wengi ndani yake kama biashara ya sigara
Ni mradi wenye hela sana


Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Inawezekana wana predict chaos au social unrest, sijajua kwa nini bongo raia kumiliki silaha ni mtihani mzito

Wanajua hata fire brigades zitafeli na police watazidiwa kama chakula kitakuwa pungufu
Sasa Hebu fikiria kikinuka huko naona itakuwa Iraq cha mtoto
Naona karma inataka ku play part yake sijui


Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Back
Top Bottom