Corona ikisambaa kwenye Mikoa inayozalisha chakula kwa wingi, Maisha yatakuwa magumu mara kumi ya hapa

mtotomtamuu

JF-Expert Member
Dec 4, 2016
602
1,454
Leo nimenunua sukari kilo moja 4000, wakati siku kumi zilizopita nilinunua 2600, wauzaji wanasema sukari ya nje imehadimika na ya ndani ni chache nayo ni adimu, maana yake nchi zilizokuwa zinatupiga tafu kutuuzia sukari kubalance soko la ndani zipo kwenye lockdown au zimeathirika vibaya na corona hivyo hata kwao bidhaa hii ni adimu kwani viwanda havifanyi kazi

Hivyo hata hapa nchini huu ugonjwa unaweza ukaleta njaa na vyakula vikapanda bei ambayo hatujawahi kuishuhudia

Mikoa inayolisha taifa inatakiwa ilindwe kwa vyovyote, endapo huu ugonjwa ukisambaa kutoka hapa Dar ukaenea hadi huko, wakulima wataathirika na kazi za kilimo zitasimama kila mkulima atakuwa anahangaikia roho yake na wengine kwa uwoga watasimamisha kilimo kuogopa huu ugonjwa

Kama kilimo kikiathirika kinachofuata ni ukosefu wa chakula , hali itazidi kuwa mbaya zaidi, hadi sasa Dar inatakiwa iwekwe kwenye karantini asitoke mtu kwenda mikoani na mtu asiingie Dar kwa sasa, la sivyo ugonjwa utasambaa nchi nzima na ukiingia kwenye mikoa inayolisha taifa njaa itatusogelea.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yote tumwachie Mola.
Awape maarifa wenye Kuzishikilia dola watoe maamuzi mazuri na mema kwa nchi yetu..

But mnalia lia kusema kukaa kwenye lockdown,

Hivi wewe ukihiweka In lockdown na familia yako..Corona itakupataje ,Acha kulalama ..yani kila kitu usimamiwe au upewe maamuzi..
Jitambue wewe unayelilia lockdown..
Jifungie wewe na koo zako..

Na kama hutaki,basi ukiugua au uki acquire usimlaumu mtu..
 
Leo nimenunua Sukari kilo moja 4000 , wakati siku kumi zilizopita nilinunua 2600, wauzaji wanasema sukari ya nnje imehadimika na ya ndani ni chache nayo ni adim, maana yake nnchi zilizokuwa zinatupiga taff kutuuzia sukari kubalance soko la ndani zipo kwenye lockdown au zimeathirika vibaya na corona hivyo hata kwao bidhaa hii ni adim kwani viwanda havifanyi kazi

Hivyo hata hapa nchini huu ugonjwa unaweza ukaleta njaa na vyakula vikapanda bei ambayo hatujawahi kuishuhudia

Mikoa inayolisha taifa inatakiwa ilindwe kwa vyovyote, endapo huu ugonjwa ukisambaa kutoka hapa Dar ukaenea hadi huko, wakulima wataathirika na kazi za kilimo zitasimama kila mkulima atakuwa anahangaikia roho yake na wengine kwa uwoga watasimamisha kilimo kuogopa huu ugonjwa

Kama kilimo kikiathirika kinachofuata ni ukosefu wa chakula , hali itazidi kuwa mbaya zaidi, hadi sasa Dar inatakiwa iwekwe kwenye karantini asitoke mtu kwenda mikoani na mtu asiingie Dar kwa sasa, la sivyo ugonjwa utasambaa nchi nzima na ukiingia kwenye mikoa inayolisha taifa njaa itatusogelea.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuwa na uhakika itafika huko pia.
 
Kwani kuna uhakika gani kama huko mashambani ugonjwa haujafika mkuu?

Kipindi hiki cha pasaka nimeshuhudia watu wengi tu wakisafiri kutoka dar kwenda kujipumzisha mikoani hasa kanda ya kaskazini. Tutegemee ongezeko kubwa la maambukizi nje ya dar ndani ya wiki chache zijazo..
 
Sure ni swala la muda tu.
 
Back
Top Bottom