Corona: Hatimaye Watanzania wameanza kutumia lugha inayotumika duniani kote

MK254

JF-Expert Member
May 11, 2013
22,045
2,000
Tangu hili janga liikumbe dunia, Watanzania wamekua wakiichukulia poa, wamekua wanaita "kaugonjwa", tukajaribu sana kuwahubiria humu kwamba kuna mataifa watu wanakufa kwa maelfu, sisi huku tunachukua tahadhari na kujichimbia, wakawa wanabeza kila juhudi zetu.

Hata kupima wamekua wanapima watu wachache sana na kutubeza humu JF kwamba wao maambukizi ni machache kisa wamepima wachache, sisi tunapima mamia ya watu kwa siku, namba zetu zikipandisha wanachekelea.

Jana waziri wao wa afya kwa mara ya kwanza nimeona anatoa hotuba liiyosheheni maneno kama yanayotumika na viongozi wa mataifa mengine duniani, ametoa elimu kwa Watanzania na kutahadharisha kuhusu uwezekano wa wao kuambukizana ndani kwa ndani na jinsi kirusi kinaweza kuwa kinasambaa kwa kasi humo humo.

Sasa hivi hapa Kenya tunaibukiwa na watu wanatokea Tanzania na hiki kirusi, yaani mpaka wanafika huku hujui huko wameambukizana kivipi. Juzi wanaachia Mtanzania anatokea Dubai na kutinga Dar siku kadhaa kisha anasafiri hadi Mwanza, ndio baadaye wanamfuata na kumkuta na kirusi, muda wote anakiachia kwa ndugu, marafiki, majirani na wasafiri wenzake.

2363991_IMG-20200409-WA0238.jpg

-------------------------------------

Tanzania could soon be dealing with local transmission of
 
Bufa

JF-Expert Member
Mar 31, 2012
6,742
2,000
Lockdown nchi nzima kama mlivyojaribu Kenya ni uzwazwa.

Lockdown yenu Kenya imewafikisha wapi na kila siku vifo vinaongezeka, ona bongo watu wanadunda tu.

Kenya na Rwanda mnapenda kushabikia kila kitu wanachofanya mabwana zenu mizungu na nyie mnajiona mizungu.
 
Kwanza neno lockdown mnalitumia bila kuelewa maana yake, na ndio maana nasema muhimu sana mkapewa elimu, asilimia kubwa ya nyie watu wala hamjui nini kinaendelea, mpo mnatoa kauli zinazodhihirisha kutokuelewa chochote, waziri wenu aendelee na elimua aliyoanza jana, labda ipo siku mtamuelewa, japo amechelewa sana lakini akomae tu.

Pili, Kenya watu hawafi kila siku, hiyo mumeaminishwa visivyo, wanaowapa hizi taarifa wanawapotosha sana nyie watu, mpaka sasa vifo vimesajirwa vya watu sita huku, na wote walikua na matatizo mengine ya kiafya, kwa kifupi hiki kirusi hakijaonyesha makali yake Afrika, maambukizi yansambaa lakini vifo bado vichache mno ukilinganisha na Ulaya wanakopigwa chini kwa maelfu.

Lakini hatufai kubweteka kisa tumekoswa koswa kwenye idadi ya vifo, mpaka siku itolewe jibu kisayansi, tunafaa kuendelea kujichimbia, kuchukua kila aina ya tahadhari, nye hapo mnapima watu wachache sana kwa siku, yaani wiki tatu mlikua mumepima watu 300 wakati sisi hao 300 tunapima kwa siku moja. Hivyo mahesabu ya haraka kwa mtoto wa chekechea za Kikenya ataelewa kwanini namba zetu za maambukizi zinapandisha, sijui kama hii elimu inaeleweka kwa Mtanzania wa kidato cha nne au hata chuo kikuu maana siku zote hizi bado hamuonekani kuelewa kwanini namba zetu zinasomeka juu kushinda majirani wote. Mpo mnachekelea tu.

Ni kama UKIMWI, uwe hutaki kupima, ila unawafyatua masista du kavu kavu huku ukichekelea wenzako wanaopimwa UKIMWI, kwamba wewe unajijua mzima kisa hupimwi. Sasa unakuta masista du uliowahi kulala nao wamepimwa na kupatikana na ngoma, ndio kama inavyotendeka huku, tunaibukiwa na watu wanaotokea Tanzania, tukiwapima wanapatikana na kirusi, ila huko kwenu kimyaaa mkijiaminisha kwamba kipo tu kwa watu 20
 
Bufa

JF-Expert Member
Mar 31, 2012
6,742
2,000
Sijamaliza kusoma ngonjera yako; call it whatever you like lockdown, isolation, halt, quarantine, kusimamisha shughuli nk. Ni kitu kile kile.

Panic mode yenu haijazaa matunda yeyote badala yake mnaonekana wajinga tu kwa kuiga mizungu kila kitu bila kuzingatia mazingira yenu. Hadi leo wakenya waliokufa kwa shurti ya polisi ni wengi kuliko waliokufa kwa corona, hilo huoni sio! How stupid can one be?

Msome mkenya mwenzio akisifia approach ya Magufuli badala ya kuiga mabwana zenu mizungu ili tu na nyie muonekane duniani:
The Good, the Bad and the Worse in Africa's Anti Corona Crusades; Lessons from Tanzania

Bongo tunadunda hayo mafua ya mizungu yatawaua mizungu hao hao na wanaojifanya mizungu wa Africa, KE.
 
Mbolabilika

JF-Expert Member
Jul 30, 2019
1,967
2,000
Elimuyako ndogo ,kila kitu kinachofanyika duniani mipango yake hata hiyo simu unayotumia ni mipango yake umeipata iwe mtihani kwako ushukuru ama ukufuru kwa kuangalia porn na mengineyo Kama maneno yako hivyo unavyoandika
Mungu hakuweka mipaka, ilichorwa na mzungu, labda kama mzungu ndiye unamuona mungu wako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
joto la jiwe

JF-Expert Member
Sep 4, 2017
19,439
2,000
Habari za Ijumaa kuu ndugu na wanafamilia wa JF. Ningependa kuwakumbusha jambo muhimu sana la kuzingatia wakati tukienda kushuhudia kifo cha mpendwa wetu Yesu Kristo:

SCORE BOARD

Kenya. 184, 7deaths
Rwanda. 110, 0 death
Uganda 53, 0 death
Tanzania 25, 1 death
Burundi 3, 0 death
South Sudan. 3, death

Wale wanaoendelea kupiga domo, wasisahau kwenda kuzika wafu wao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Numbisa

JF-Expert Member
Dec 12, 2016
194,948
2,000
Wakenya bana humu JF wanajipaisha sana wakati nchini mwao rais anakurupuka kuongeza pesa kwa wasanii bila sababu za msingi

Ruto anaropoka balaa

Raila ndo kama hivi

Speaking to Citizen TV on Friday, Raila said when coronavirus ends, the music will begin.

"...COVID-19 ikiisha, wimbo utaendelea..hii janga imetukatia pumzi kidogo.. tunafanya mipango.. ikiisha tutarudi... wale ambao wanahusika na haya maneno wanaendelea na wako karibu kumaliza," he said.

(When coronavirus comes to an end, reggae will continue. This disease has cut our lives short but we are planning. Those who were dealing with BBI are still working and are about to finish)

Raila further noted that there was no budget for Building Bridges Initiative.

"...we were getting money from friends who were helping. Tumefanya mkutano karibu nane.. kila mkutano ilikuwa inakula pesa kidogo sana.." he said.

The AU envoy said the amount of money that they were using was not reaching Sh100m.

"....ilikuwa pesa kidogo na mingi ilikuwa inatoka kwa watu binafsi so serikali," he added.
 
Mikopo Chefuchefu

JF-Expert Member
May 15, 2017
3,380
2,000
Hata watanzania wote tukifungiwa kwenye ka chumba kadogo, hatuwezi kuisha kwa Corona! Ugonjwa huu hauna uwezo wa kuua watu wengi kiasi hicho.
 
MK254

JF-Expert Member
May 11, 2013
22,045
2,000
Wakenya bana humu JF wanajipaisha sana wakati nchini mwao rais anakurupuka kuongeza pesa kwa wasanii bila sababu za msingi

Ruto anaropoka balaa

Raila ndo kama hivi

Speaking to Citizen TV on Friday, Raila said when coronavirus ends, the music will begin.

"...COVID-19 ikiisha, wimbo utaendelea..hii janga imetukatia pumzi kidogo.. tunafanya mipango.. ikiisha tutarudi... wale ambao wanahusika na haya maneno wanaendelea na wako karibu kumaliza," he said.

(When coronavirus comes to an end, reggae will continue. This disease has cut our lives short but we are planning. Those who were dealing with BBI are still working and are about to finish)

Raila further noted that there was no budget for Building Bridges Initiative.

"...we were getting money from friends who were helping. Tumefanya mkutano karibu nane.. kila mkutano ilikuwa inakula pesa kidogo sana.." he said.

The AU envoy said the amount of money that they were using was not reaching Sh100m.

"....ilikuwa pesa kidogo na mingi ilikuwa inatoka kwa watu binafsi so serikali," he added.

Andika ila kuwa makini usikutwe na Makonda unazurula

2359224_abdulnondo1_2___B-ncLjHnmkR___.jpeg
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom