Corona haina kinga kwa maana ya Chanjo - Jikinge kwa hali na mali chukua tahadhari

Shocker

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
1,942
3,819
Ndugu wananchi wenzangu napenda kuwaambia tu na huko mitandaoni kumejaa habari na jipya,jamaa amepata chanjo za dozi mbili kasafiri amerudi kupimwa ameoneka positive almanusura azimie.

Hizi chanjo zipo kwenye majaribio na safari hii zinapelekwa direct kwa binadamu, ndio ikasemwa haata ukichanjwa na kupata hizo dozi iwe moja au mbili bado unatakiwa ufuate taratibu zote,barakowa na baharikowa (Kowa kule Kisiwa cha pemba mjini ni konokono). Uwe mwangalifu sana sana, kwa ufupi uwe msafi wa kunawa nawa kila wakati.

Jipya ni kuwa sasa inatakiwa baada ya barakaowa uongeze na miwani kirusi kinapita hata kwenye macho.

Chukua tahadhari usingonje uambiwe Tatizo karne hizi hata ukitamani kufa haufi. Wacha John aitwe Magufuli.
 
Hapo mkuu sidhani kama ni kweli. Dunia yote wanahangaika na corona, je wote wana SGR?

HAPO UMECHANGANYA KARATASI KWENYE MAFAILI.
Ndivyo wanavyomshauri Mtemi wetu mpendwa

Mpaka amekuwa paranoid

Sasa sijui mshauri mpya ni Pasco Mayalla?😂
 
Ndugu wananchi wenzangu napenda kuwaambia tu na huko mitandaoni kumejaa habari na jipya,jamaa amepata chanjo za dozi mbili kasafiri amerudi kupimwa ameoneka positive almanusura azimie....
Wewe naona ni mjukuu wa kibwetere
 
Ndugu wananchi wenzangu napenda kuwaambia tu na huko mitandaoni kumejaa habari na jipya,jamaa amepata chanjo za dozi mbili kasafiri amerudi kupimwa ameoneka positive almanusura azimie...
Asante kwa kutoa tahadhari.

Napenda tu nikupe taarifa ni kuwa unapopata chanjo, haimaanishi kuwa wewe hautopata Corona, Corona utaipata, na unaweza kumwambukiza mwingine, lakini chanjo inakusaidia kuwa na Kinga mwilini hivyo kwako wewe haitakusumbua,

Muhimu ujue kuwa Chanjo haikuzui wewe kutopata Corona bali itasaidia mwili wako kupambana na virusivya corona haraka Sana na havitapata nafsi ya kukuletea madhara makubwa.. Kwako wewe utakuwa ni ugonjwa WA kawaida kama kupata mafua tu.

Ujue Chanjo ya Corona au ni Virus vya Corona ambavyo viko hai lkn havina madhara kwako au vilivyokufa..
 
Ndugu wananchi wenzangu napenda kuwaambia tu na huko mitandaoni kumejaa habari na jipya,jamaa amepata chanjo za dozi mbili kasafiri amerudi kupimwa ameoneka positive almanusura azimie...
Hivi dunia hii ya sasa , mtu unaamuwaje kuwa na sura ya mbuzi kiasi hiki, kwa kuleta propaganda kiasi hiki? Hata ksma MATAGA wengi huwa sio wafuatiliaji wa vyombo vya habari vya kimataifa, lakini sio kwa hatua hiyo.hivi unafahamu maana ya chanjo? Tofautisha dawa na chanjo, nani alikwambia kuwa ukipata chanjo unaweza kwenda kupimwa na ukakutwa na huna ugonjwa husika?

Elewa kwanza kazi ya chanjo mwilini na jinsi inavyofanya kazi.hizi ni taaluma za watu.fuatilia israel jinsi walivyoona maajabu ya chanjo ilivyofanya kazi, baada ya asilimia kubwa ya wananchi wake kupata chanjo, sasa leo jitu linaamka tu na kuanza propaganda eti mbona nchi walizochanja watu wao bado wanaendelea kufa tu??bila kuwa na takwimu halisi!!!
 
Back
Top Bottom