Moja kwa moja kwenye hoja. Itifaki zote zimezingatiwa.
Kwa rais msomi mwanasayansi wa kiwango cha mzee baba, haiingii akilini kuwa kuna wakati wowote alitegemea kuzuia ugonjwa huu kuingia nchini au hata kuzuia kusambaa kwa maombi, miti shamba au kujifukiza nyungu.
Haiingii akilini pia nyomi ya madaktari na ma Profesa alionao serikalini ati kuwa wote nao walikubaliana kwenye u Kinjekitile huu. Kuwa eti juu ya kunawa nawa na kuvaa mabarakoa, huku tukitumia madaladala, nyomi kama vile masokoni, kwenye ferry, nk, u Kinjekitile huo ungeondosha ugonjwa huu.
Ninadhani itakuwa kutowatendea haki wazamivu hawa kutotambua kuwa karata pekee aliyonayo mkuu huyu kwa kweli iko kwenye kutegemea kuwa hatimaye Beberu atagundua dawa au chanjo!
Hata hivyo kutegemea Beberu usiye na mawasiliano naye, usiye na ushirika naye kwenye hilo, unayemtuhumu kukuchawia kila uchao, nk; ni suala fikirishi kweli kweli kama si kipimo kamili cha uz***wa.
Mengine yote:
1. Kutosikiliza ushauri wowote mwingine
2. Kukataa kupokea simu za marais wenziwe
3. Kumwaga misukule humu jamvini
4. Kurusha jiwe gizani kuwa ligi inakuja
5. Kurusha jiwe gizani kuwa uchaguzi mkuu unakuja
6. Kutuma ndege Antananarivo kufuata kikombe cha babu
7. Kufuka nyungu
8. Maombezi
9. Mapapai, mbuzi, oil nk kupimwa Corona
10. Nk, nk
Yote ni janja ya nyani, akisubiria dodo kwenye mnazi huku akiendelea sisi kutochomesha mahindi.
Akiyafanya yote haya yeye yuko salama Chatto nyumbani kwake, mbali na hilu epicenter la huu ugonjwa.
Sisi katuachia jiji letu tuukabili muziki wake huku tukipukutika!