kijana wa leo
JF-Expert Member
- Nov 28, 2011
- 2,916
- 7,164
Sera ya Elimu Bure kwa shule za msingi na Sekondari iliyoanzishwa na Serikali ya awamu ya tano imeleta mwamko mkubwa kwa wazazi kuwaandikisha watoto wao hasa katika shule za msingi.
Licha ya kuwepo jitihada mbalimbali ongezeko la wanafunzi kwenye shule za Serikali limekuwa na changamoto mbalimbali ikiwemo uhaba wa madawati, madarasa n.k
Sasa kwa kuliona hilo Diwani kata wa Kata ya Mbagala Kuu, Yusuf Manji kwa kupitia mfuko wa maendeleo wa Mbagala Kuu wamekuja na jitihada za muda mfupi ambapo wametoa msaada wa mahema makubwa 12 na viti 800 kwa shule zote za Serikali zilizopo kwenye kata yake
Msaada huo ni kwa ajili ya wanafunzi ambao walikuwa wanasoma nje ya madarasa na kukaa chini na kuingia kwa zamu madarasani pia shule hizo ndizo shule pekee za Serikali Dar es saalam zinazopata lishe bure.
Mratibu Elimu kata ya Mbagala Kuu, Magreth Anjetile anamshukuru Diwani kwa kutupia macho sekta ya Elimu na kwamba misaada hiyo itaamsha hali ya wanafunzi kupenda shule ………..
>>>’Utakuta darasa lina wanafunzi kuanzia 130, 180 wanafunzi 200 inategemea na miaka ya uandikishaji, hivyo kuondoa umakini wa wanafunzi kuwasikiliza walimu wao changamoto hii diwani aliiona akaamua kutupatia maturubai‘
#MillardAyoUPDATES Diwani kata ya Mbagala Kuu, Yusuf Manji kwa kupitia mfuko wa maendeleo wa Mbagala Kuu ametoa msaada wa mahema makubwa 12 na viti 800 kwa shule zote za Serikali zilizopo kwenye kata yake katika kusaidia wanafunzi ambao waliokuwa wanasoma nje ya madarasa na kukaa chini na kuingia kwa zamu madarasani pia shule hizo ndizo shule pekee za Serikali Dar es saalam zinazopata lishe bure.