Constantine Kasese awataka Wafanyakazi Shirika la Posta kubadilisha mtazamo

PendoLyimo

JF-Expert Member
Sep 30, 2014
879
956
  • Mkoa utakaotoa mshindi katika shindano la uandishi wa barua kupewa zawadi
  • Wiki ya Posta kuanza Octoba 4

Na Mwandishi wetu, Morogoro

SHIRIKA la Posta Tanzania (TPC) limewataka wafanyakazi wake kubadilisha mtazamo wao na kuendana na mfumo wa kidijitali.

Hayo yamesemwa na Kaimu Meneja Mkuu Uendeshaji Biashara wa Shirika la Posta Tanzania Constantine Kasese alipokuwa akizungumza na wafanyakazi wa Shirika la Posta Mkoa wa Morogoro katika ofisi za Posta Mkoani humo, mara baada ya kuhitimisha kikao cha siku mbili cha Baraza la Majadiliano la Shirika hilo kilochofanyika mkoani humo.

Kasese amesema, wafanyakazi wanatakiwa waendane na mikakati ya Serikali ili kuboresha huduma ndani ya taasisi.

Amesema, Serikali imewekeza fedha nyingi ndani ya taasisi ili kuboresha mfumo wa kidigitali na hilo linaenda kuongeza mapato ndani ya taasisi na hata Serikali.

Kasese amesema, wafanyakazi pia wanatakiwa kuboresha utendaji wao wa kazi hasa katika eneo la usafirishaji wa mizigo, barua na vifurushi kwa kufanya shughuli za usafirishaji kwa weledi na kwa usahihi ili kuongeza mapato ndani ya Shirika yatakayoleta tija kwa Serikali.

Ameeleza kuwa, mameneja wa mikoa watumie rasilimali zao kuwafikia wananchi na kuwapatia elimu ya huduma zinazopatikana ndani ya Shirika hilo ili kuongeza wigo wa upatikanaji wa wateja.

“Kuna huduma zimerahisishwa ikiwemo Huduma mpya ya Virtual Box ambayo namba yako ya simu ndiyo sanduku lako la Posta, Posta Kigangani na kuna huduma zingine zinakuja na zote zitapatikana ndani ya Shirika la Posta, hivyo hakilisheni mnakuwa mabalozi wazuri wa huduma zetu”. Alisema Kasese

Akizungumzia kuelekea Kilele cha Siku ya Posta duniani Oktoba 9 mwaka huu, Kasese amesema kwa mwaka huu maadhimisho hayo yatafanyika Jijini Dodoma na kila mkoa watatakiwa washiriki katika shughuli mbalimbali kuelekea siku hiyo.

Aidha, amesema kwa Mwaka huu mgeni rasmi anatarajiwa kuwa ni Makamu wa Rais Dkt Philip Mpango na tayari wanaenda kuweka historia mpya ndani ya muda mfupi toka kuanzishwa kwa Shirika hilo mwaka 1994 baada ya Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa kuzindua Huduma Pamoja mwanzoni mwa wiki hii.

Ameongeza, maad
 
Wale wazee inabidi wastaafu wote tuanze upya. Watu hata kutumia kompyuta ni shida!!!
 
Shirika la posta dunia hii ya sasa!!pls mwenye informations za kunielimisha mimi namwomba anielimishe nini majukumu ya shirika letu la posta,natanguliza Shukraani mno
 
Back
Top Bottom